Friday, 12 September 2025

UZINDUZI WA KAMPENI JIMBO LA KOROGWE MJINI ILIKUWA HIVI,,,


 Picha mkono wa kulia ni Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Korogwe Mjini,Thobias Nungu  akiwataka Wananchi kupiga kura nyingi za heshima kwa mgombea Urais Dk. Samia Suluhu Hassa,madiwani huku akimnadi Mgombea  Ubunge wa Jimbo la Korogwe Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Charles Njama (kushoto ambaye anawasalimia wananch) hafla iliyofanyika katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika uwanya wa Manundu sokoni uliopo wilayani hapo.





Pichani ni Katibu wa Chama cha Mapinduzu CCM jimbo la Korogwe mjini,Evarts Mluge akiwahutubia wananchi wa Korogwe akiwanadi mgombea Urais Dk. Samia Suluhu Hassan Mbunge na madiwani.




Pichani ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Korogwe mjini,Mujibu Wandi,akiwataka wananchi kuchagua wagombea wa chama cha mapinduzi ili kuendelea kuleta maendeleo.


MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Korogwe Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Charles Njama akiomba wananchi kupiga kura nyingi kwa wagombea wa Chama tawala huku akiahidi kwamba kwa kufanya hivyo kutatoa fursa uwepo wa Korogwe ya Viwanda.




 
Pichani juu ya bajaji ni MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Korogwe Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Charles Njama akiwasili katika uwanja wa Manundu sokoni hafla ya uzinduzi kuwanadi wagombea wa Chama tawala .

Wednesday, 10 September 2025

UWT KOROGWE MJINI WAJITOKEZA KUFANYA USAFI MAANDALIZI UZINDUZI WA KAMPENI KUWANADI WAGOMBEA WAKE,,,

Pichani ni Katibu wa Umoja wa wanawake (UWT)Korogwe Mjini,Suzana Mandia akitoa maelezo mpango mkakati uliopo katika maandalizi ya uzinduzi wa kampeni kuwanadi wagombea wa CCM ili kuwezesha kupata kura za kishindo,alitoa kauli hiyo katika zoezi la kufanya usafi uwanja wa sokoni uliopo kata ya Manundu. wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga.
 







Wednesday, 27 August 2025

NJAMA ACHUKUA FOMU TUME YA UCHAGUZI INEC,,,

Msafara ,,Wananchi na wafanyabiashara wa bajaji na pikipiki wamsindikiza mgombea wa CCM kiti cha Ubunge jimbo la Korogwe mjini kuchukua fomu.

Msafara ukipita kata zote za jimbo la Korogwe mjini.
Picha katikati ni Mgombea kiti cha Ubunge jimbo la Korogwe Mjini,Charles Njama akionyesha fomu ya uteuzi baada ya kukabidhiwa katika ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi (INEC) Jimbo la Korogwe mjini mkoani Tanga.  

 











Friday, 11 July 2025

WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI WATAKIWA KUWA WAVUMILIVU,,

Picha katikati ambaye amesimama anazungumza kwa ishara ni Mwenyekiti wa CCM Korogwe Vijijini,Ally Waziri akiwataka wanaCCM waliotia nia ya kuwania Udiwani kuwa wavumilivu, kikao ambacho kilifanyika Ofisi za CCM Wilayani ya Korogwe mkoani Tanga.

 WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walitia nia ya kuwania Udiwani kupitia chama hicho tawala Jimbo Korogwe Vijijini,wametakiwa kuwa watulivu huku wakiwaamini viongozi wao katika kipindi hiki cha mchakato wa ndani wa uchaguzi unaoendelea kwa maelezo kuwa haki itatendeka.


Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Korogwe Vijijini ,Ally Waziri kwenye kikao na wanaCCM waliotia nia ya kuwania Udiwani, kikao ambacho kilifanyika Ofisi za CCM Wilayani humo amhapo watia nia zaidi ya 100 kutoka Kata 29 waliweza kuhudhuria.

Waziri alisema, wakati mchakato wa uchaguzi wa ndani ukiendelea ni vyema watia nia wakaishi katika imani ya chama chao huku wakifuata kanuni,katiba na sheria na kwamba anayehisi ameshindwa kuyafuata hayo ni vyema akaandika barua kujiengua.

Waziri aliwaasa wale wenye tabia ya kwenda kinyume na taratibu za uchaguzi kwamba kwa yeyote atakayebainika hatua za kisheria hazitosita kuchukuliwa dhidi yake akisisitiza subira na mshikamano kwa dhumuni la kufanikisha uchaguzi mkuu. 
Mwisho.

Wednesday, 2 July 2025

MJUMBE MKUTANO MKUU CCM TAIFA,ASIA KINGONGO AMEJITOKEZA KUCHUKUWA NA KURUDISHA FOMU KUWANIA KITI CHA UDIWANI KWAMNDOLWA,,


 

Pichani mkono wa kulia mwanamke ni Mjumbe mkutano mkuu taifa,Mjumbe kamati ya wazazi utekelezaji Mkoa wa Tanga na katibu mwenezi tawi la Kwameta na katibu wa vijana kata ya Kwamndolwa,Asia Ally Kingongo akichukua fomu ya kuwania nafasi ya Udiwani kata ya Kwamndolwa kwa Katibu kata  ya Kwamndolwa iliyopo Korogwe Mjini,Samweli Mbuguje mkono wa kushoto ambaye ni mwanaume.

Picha ni Mjumbe mkutano mkuu CCM taifa,Mjumbe kamati ya wazazi utekelezaji Mkoa wa Tanga na katibu mwenezi wa CCM tawi la Kwameta na katibu wa vijana kata ya Kwamndolwa,Asia Ally Kingongo akichukua fomu ya kuwania nafasi ya Udiwani kata ya Kwamndolwa akionyesha fomu mara baada ya kuchukua nje ya ofisi ya CCM tawi la Kwameta.

Pichani ni Katibu kata  ya Kwamndolwa,Samweli Mbuguje mkono wa kushoto ambaye ni mwanaume.akikagua fomu ya Mjumbe wa mkutano mkuu taifa,Mjumbe kamati ya wazazi utekelezaji Mkoa wa Tanga na katibu Mwenezi CCM tawi la Kwameta na katibu wa vijana kata ya Kwamndolwa,Asia Ally Kingongo alichukua fomu na kurudisha ya kuwania nafasi ya kiti cha Udiwani kata ya Kwamndolwa


Pichani ni Mjumbe wa mkutano Mkuu CCM taifa,Mjumbe kamati ya wazazi Utekelezaji Mkoa wa Tanga na katibu Mwenezi CCM tawi la Kwameta na katibu wa vijana kata ya Kwamndolwa,Asia Ally Kingongo Mara baada ya kuchukua fomu na kurudisha ya kuwania nafasi ya kiti cha Udiwani kata ya Kwamndolwa akiwa na familia yake.

ZOEZI LA MTANGAZAJI WA REDIO UHURU,REHEMA LUSEWA KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU KUWANIA KITI CHA UDIWANI VITI MAALUM ILIKUWA HIVI,,,


Picha mkono wa kulia ni Mjumbe wa baraza la UWT Korogwe Mji na Mtangazaji nguli wa ITV na Uhuru redio ya chama cha Mapinduzi CCM,Rehema Lusewa akichukua fomu ya kuwania nafasi ya Udiwani viti maalum Korogwe mjini kwa Katibu wa UWT Korogwe mjini,Suzan Mandia (mkono wa kulia). 


Picha mkono wa kulia ni Mjumbe wa baraza la UWT Korogwe Mji na Mtangazaji nguli wa ITV na Uhuru redio ya chama cha Mapinduzi CCM,Rehema Lusewa akirudisha fomu ya kuwania nafasi ya Udiwani viti maalum Korogwe mjini kwa Katibu wa UWT Korogwe mjini,Suzan Mandia (mkono wa kulia). 

Picha mkono wa kulia ni Mjumbe wa baraza la UWT Korogwe Mjini na Mtangazaji nguli wa ITV na Uhuru redio ya chama cha Mapinduzi CCM,Rehema Lusewa akisaini mara baada ya kurudisha.






Sunday, 29 June 2025

CHRISTINA AJITOKEZA KUCHUKUWA FOMU KUWANIA NAFASI YA UDIWANI VITI MAALUM,,,


 Picha mkono wa kulia ni Christina Fransis Kabelwa akichukua fomu ya kuwania nafasi ya Udiwani Viti maalum Korogwe vijijini kwa Katibu wa UWT Korogwe vijijini,Nuru Jacob Mwaibako.