Picha katikati ambaye amesimama anazungumza kwa ishara ni Mwenyekiti wa CCM Korogwe Vijijini,Ally Waziri akiwataka wanaCCM waliotia nia ya kuwania Udiwani kuwa wavumilivu, kikao ambacho kilifanyika Ofisi za CCM Wilayani ya Korogwe mkoani Tanga.
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walitia nia ya kuwania Udiwani kupitia chama hicho tawala Jimbo Korogwe Vijijini,wametakiwa kuwa watulivu huku wakiwaamini viongozi wao katika kipindi hiki cha mchakato wa ndani wa uchaguzi unaoendelea kwa maelezo kuwa haki itatendeka.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Korogwe Vijijini ,Ally Waziri kwenye kikao na wanaCCM waliotia nia ya kuwania Udiwani, kikao ambacho kilifanyika Ofisi za CCM Wilayani humo amhapo watia nia zaidi ya 100 kutoka Kata 29 waliweza kuhudhuria.
Waziri alisema, wakati mchakato wa uchaguzi wa ndani ukiendelea ni vyema watia nia wakaishi katika imani ya chama chao huku wakifuata kanuni,katiba na sheria na kwamba anayehisi ameshindwa kuyafuata hayo ni vyema akaandika barua kujiengua.
Waziri aliwaasa wale wenye tabia ya kwenda kinyume na taratibu za uchaguzi kwamba kwa yeyote atakayebainika hatua za kisheria hazitosita kuchukuliwa dhidi yake akisisitiza subira na mshikamano kwa dhumuni la kufanikisha uchaguzi mkuu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment