Saturday, 18 October 2025

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KOROGWE MJINI''CHARLES NJAMA AWAOMBA WANANCHI OKTOBA 29 CHAGUENI WAGOMBEA WA CCM KUHARAKISHA MAENDELEO,,


Picha ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Mjini kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Charles Njama akiomba kura kwa wananchi huku akiwaeleza wananchin sifa za Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kutekeleza miradi mingi ya maendeleo.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Mjini kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Charles Njama amesema,Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kutekeleza miradi mingi ya maendeleo hivyo kuna kila sababu ya kulipwa mema kwa kupigiwa kura nyingi za kishindo.
Njama ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika shule ya msingi Kwakombo kata ya Kwamsisi iliyopo Korogwe mkoani Tanga,,amesema Rais Dkt Samia ametoa fedha nyingi kwenye Kata hiyo kwa ajili ya miradi ya maendeleo hivyo akipatiwa Kura nyingi kwenye uchaguzi ujao itamsukuma kuongeza kasi ya kusukuma miradi mingi kwa wananchi .

'' Ikifika Oktoba 29 mjitokeze kwenda kupiga kura,tena muwashawishi na kuwahimiza wenzenu wengine kwenda kupiga kura,tukampe kura nyingi za kishindo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ''alisema mgombea huyo wa ubunge Jimbo la Korogwe Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM.

Mbali na hayo Njama alisema kwamba,atakapoingia madarakani miongoni mwa vipaumbele vyake ni pamoja na kushirikiana na vijana katika kuinua uchumi kwa kuwawezesha mitaji sanjari na matumizi ya sekta ya michezo na sanaa lengo kuongeza kipato.

Aidha aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya sita imetoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi huku akitaja ujenzi mradi wa Kilimo cha umwagiliaji kwa wakazi wa Kata ya Kwamsisi, mradi ambao utasaidia kukuza uchumi kwa wananchi.

''Shilingi bilioni 24.5 zimeletwa na Rais Dkt Samia kwa ajili ya bonde la kilimo.Kupitia bonde hili mtalima na kuvuna kwa wingi na kuuza kwenye soko la ndani na hata nje''alisema Njama huku akishangiliwa na Wananchi waliohudhuria mkutano huo wa kampeni.

Aidha Njama alisema,pindi mradi huo utakapoanza kutekelezwa atahakikisha kwamba kipaumbele cha ajira hususani zile za muda wanazungumza na kukubaliana na mkandarasi ili shughuli hiyo kupewa wenyeji.

Amewasihi Wananchi wa Kata ya Kwamsisi kuhakikisha kwamba ifikapo Oktoba 29 mwaka huu wanamchagua Rais Dkt Samia Suluhu, Mbunge Charles Njama na diwani Nassoro Mohamed.

Mwisho.

Pichani ni Mgombea Udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Kwamsisi,Nassoro Mohamed  alitumia wasaa huo kumuombea Kura Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akisema ni Kiongozi aliyefanikiwa kutekeleza ilani ya CCM kwa asilimia 100.


Pichani ni miongoni mwa wasanii wa kikundi cha kwaya wakionyesha burudani katika mkutano wa kampeni za chama cha Mapinduzi CCM kuwanadi Wagombea wake.




No comments:

Post a Comment