Pichani ni Mgombea Ubunge wa chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Tanga Mjini, Kassim Amary Mbaraka, akiwaeleza wananchi wa Ngamiani kusini, pindi mkinipatia ridhaa, atakwenda kusimamia ujenzi wa barabara 'Ring road' itakayotumika na magari makubwa 'malory' ikipita nje ya Mji kwa lengo la kuepusha msongamano kutoka maeneo ya Bandari.
MGOMBEA Ubunge wa chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Tanga Mjini, Kassim Amary Mbaraka, amesema kwamba, pindi wananchi wakimpatia ridhaa, atakwenda kusimamia ujenzi wa barabara 'Ring road' itakayotumika na magari makubwa 'malory' ikipita nje ya Mji kwa lengo la kuepusha msongamano kutoka maeneo ya Bandari.
Mbarak almaarufu Makubel ameyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Ngamiani Kusini katika halmashauri ya Jiji la Tanga, huku aliwasihi wananchi kumpatia kura nyingi Rais atokanaye na CCM, yeye Mbunge na madiwani wake.
Katika mkutano huo wa kampeni, Makubel alisema kwamba, mgombea urais wa CCM Dk. Samia kutua Tanga amekusudia kuifanyia Tanga mambo makubwa mazuri kwa wananchi.
Makubel ametaja mambo hayo kuwa ni pamoja na utekelezwaji ujenzi wa miundombu ya barabara kutoka Bandarini kupitia nje ya Mji ambayo itatumiwa na malori hatua ambayo itasaidia kupunguza msongamano.
"CCM imekusudia kuifanyia Tanga mambo makubwa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amekusudia makubwa,kutajengwa 'ring road' kuingia na kutoka Bandarini,mkinichagua nitaenda kulisimamia hili" alisema Kassim Amary Mbaraka almaarufu Makubel.
Kwa mujibu wa Makubel miradi mingine inayoenda kutekelezwa Tanga iwapo Serikali ya CCM itapata ridhaa kuingia madarakani ni ujenzi wa reli ya SGR kutoka Tanga, Kilimanjaro,Arusha hadi Singida na ujenzi wa uwanja wa ndege uliyo wa kisasa.
Mbali na hayo, Makubel alisema, iwapo Wananchi watawachagua Rais ,Mbunge na Madiwani wa CCM na kuwawezesha kushika dola jitihada mbalimbali zitafanyika ili kufufua Viwanda hatua ambayo itafufua Uchumi wa Tanga.
Aidha Mgombea Udiwani kupitia CCM Kata ya Ngamiani Kusini, Mtanga Aweso alisema,kilichomsukuma kuwania wadhifa huo kwa awamu nyingine ni kwa vile Ilani ya Chama chake imetekelezwa kikamilifu.
Mtanga amejivunia kufanikiwa kwenye usimamizi upatikanaji wa mikopo kwa Wanawake ,Vijana na walemavu ambapo kwenye nyanja ya elimu alisema ameweza kusukuma upatikanaji wa shule yenye ghorofa ndani ya kata yake.
Awali Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM wilayani Tanga, Meja mstaafu Hamisi Mkoba alimuombea kura mgombea uRais wa CCM Dk. Samia Suluhu Hassan akisema,ni Kiongozi aliyemudu kusimamia haki, umoja na mshikamano, aliwasihi wananchi kuwachagua wagombea wa Chama tawala.
Mwisho.

Pichani katikati mwanamke ambaye amevaa kilemba na sare ya CCM ni Mgombea Udiwani kupitia CCM Kata ya Ngamiani Kusini, Mtanga Aweso akiwasili eneo la mkutano akisindikizwa na wananchi wa kata hiyo.
No comments:
Post a Comment