Mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Mjini kupitia CCM, Charles Njama amesema, Mgombea urais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kutekeleza miradi mengi mingi ya maendeleo ya Wananchi hivyo kuna kila sababu ya kulipwa mema kwa kupigiwa kura nyingi za kishindo.
Njama ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kwamsisi,amesema Rais Dkt Samia ametoa fedha nyingi kwenye Kata hiyo kwa ajili ya miradi ya maendeleo hivyo akipatiwa Kura nyingi kwenye uchaguzi ujao itamsukuma kuongeza kasi ya kusukuma miradi mingi kwa wananchi .
'' Ikifika Oktoba 29 mjitokeze kwenda kupiga kura,tena muwashawishi na kuwahimiza wenzenu wengine kwenda kupiga kura,tukampe kura nyingi za kishindo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ''alisema mgombea huyo wa ubunge Jimbo la Korogwe Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM.
Mbali na hayo Njama alisema kwamba,atakapoingia madarakani miongoni mwa vipaumbele vyake ni pamoja na kushirikiana na vijana katika kuinua uchumi kwa kuwawezesha mitaji sanjari na matumizi ya sekta ya michezo na sanaa kuongeza kipato.
Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya sita imetoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi huku akitaja ujenzi mradi wa Kilimo cha umwagiliaji kwa wakazi wa Kata ya Kwamsisi, mradi ambao utasaidia kukuza uchumi kwa wananchi.
''Shilingi bilioni 24.5 zimeletwa na Rais Dkt Samia kwa ajili ya bonde la kilimo.Kupitia bonde hili mtalima na kuvuna kwa wingi na kuuza kwenye soko la ndani na hata nje''alisema Njama huku akishangiliwa na Wananchi waliohudhuria mkutano huo wa kampeni.
Aidha Njama alisema,pindi mradi huo utakapoanza kutekelezwa atahakikisha kwamba kipaumbele cha ajira hususani zile za muda wanazungumza na kukubaliana na mkandarasi ili shughuli hiyo kupewa wenyeji.
Picha ni Mgombea wa kata ya Kwamsisi wilayani Korogwe,Nassoro Mohamed akiwa kwenye mkutano wa kampeni, akimuombea Kura Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akisema ni Kiongozi aliyefanikiwa kutekeleza ilani ya CCM kwa asilimia 100.
Picha ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya Korogwe Mjini,Omari Mahanyu akizungumza kwenye mkutano wa kampeni shule ya msingi Kwakombo kata ya Kwamsisi alisema,Wananchi wanakila sababu kuwachagua wagombea wanaotoka Chama Cha Mapinduzi CCM kwa maelezo kuwa ndicho chenye Ilani inayotekelezeka.
Aidha,amewasihi Wananchi wa Kata ya Kwamsisi kuhakikisha kwamba ifikapo Oktoba 29 mwaka huu wanamchagua Rais Dkt Samia Suluhu, Mbunge Charles Njama na diwani Nassoro Mohamed.
Pichani ni mashabiki wakiburudika kwenye mkutano wa kampeni wa CCM.
No comments:
Post a Comment