- Picha ni Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Jimbo la Korogwe Mjini,Moses Birumo katika mkutano wa kampeni akiwataka Vijana kutokuwa Chanzo cha kuharibu amani ya nchi.
MWENYEKITI wa Vijana wa CCM Korogwe Mjini,Moses Birumo amewataka Vijana kutokuwa Chanzo cha kuharibu amani ya nchi badala yake amewasihi kuwa mstari wa mbele katika kuilinda Amani.
Birumo ametoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara wa kampeni kuwanadi wagombea wa chama cha Mapinduzi CCM uliofanyika Kata ya Magunga iliyop Korogwe Mkoani Tanga.
Katika mazungumzo yake kwa wananchi,Birumo alisema: '' Vijana hatuwezi kuwa chanzo cha kuharibu amani ya nchi, tutailinda amani kwa nguvu zote'' alisema Mwenyekiti huyo wa Vijana Moses Birumo.
Katika mkutano huo wa kamepni alitumia nafasi hiyo kuwaasa vijana kutokubali kurubuniwa na baadhi ya watu wenye Nia ya kuvuruga amani huku akiwataka kuhakikisha kwamba ifikapo Oktoba 29 mwaka huu wanapiga kura.
Kwa upande wake mgombea Udiwani wa Magunga, David Mbwilizi aliwaeleza Wananchi kwamba CCM ndio chama pekee chenye uwezo wa kuharakisha maendeleo ya Wananchi wa Tanzania.
Kutokana na hali hiyo aliwaomba wananchi wa kata ya Magunga kuhakikisha kwamba wanapiga kura nyingi kwa Chama Cha Mapinduzi wakimchagua mgombea wa nafasi ya uRais,Ubunge pamoja na madiwani wa chama hicho.
Kwa mujibu wa mgombea Udiwani kata ya Magunga kupitia,David Mbwilizi,amesema wananch kuipa ridhaa CCM kuendelea kushika dola kutawezesha kufanikisha utekelezwaji wa miradi mingi ya maendeleo kwenye maeneo yao.
Kwa upande wa sekta ya afya ,Mgombea Mbwilizi alisema, pindi chama hicho kufanikiwa kuingia madarakani kupitia Ilani iliyopo watahakikisha kunajengwa Zahanati za kutosha kwa lengo la kupunguza mzigo kwa hospitali ya Magunga.
Mbali na hayo Mbwilizi ameishukuru Serikali ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kuwezesha upatikanaji wa huruma za nishati ya umeme kwenye maeneo mengi na hivyo kuharakisha maendeleo ya Wananchi wa Korogwe.
Hata hivyo,alisema,ni imani yake kwamba Wananchi wakikichagua Chama hicho tawala itakuwa rahisi kwa maeneo wachache yaliyosalia kufikishiwa huduma ya umeme kuweza kuondoa changamoto hiyo.
Mwisho.
Pichani ni vikundi mbalimbali vya sanaa vikiburudisha katika mkutano wa kampeni kata ya Magunga wilayani Korogwe.
No comments:
Post a Comment