Monday, 27 March 2017

RC TANGA,SHIGELA AKIFUNGUA WODI ZA WAZAZI LUSHOTO

  Picha ambaye ameshika kipaza sauti ni mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Lushoto Dk. Charles Mkombacheka alimweleza RC kuwa hali ya upatikanaji wa dawa kwa sasa ni asilimia 85 huku ukiwepo mpango wa kuwezesha dawa kupatikana.

Katika taarifa hiyo,Dk. Mkombachemba alisema,ili chumba hicho ‘Bufferstock’ kuanzishwa zinahitajika sh 113 milioni zilizopatikana kutoka KFW ili kuandikisha familia za akina mama wajawazito ambapo ‘Buferstock’ hiyo itakuwa tayari ndani ya wiki tatu kutoka sasa kukabiliana na upungufu wa dawa.
Pichani katikati ambaye ameshika kipaza sauti ni mkuu wa mkoa wa tanga,Martine Shigela akiongea na wauguzi na wananchi katika ufunguzi wa wodi za wazazi ambapo amempongeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Kazimbaya Makwega kwa ukarabati na kuahidi kutoa mifuko 100 moja ya saruji kwa ajili ya upanuzi wa hospital hiyo.

NA SOPHIA WAKATI,LUSHOTO
HALMASHAURI ya wilaya ya Lushoto mkoani Tanga imefanikiwa kutenga chumba maalum ‘Buffer sock’ lengo likiwa kukifanyia ukarabati hatua ambayo itasaidia kuwepo kwa uhakika wa dawa kwenye hospitali ya wilaya na vituo vya kutolea huduma kwa asilimia 100 na hivyo kuondosha kero iliyopo.

Taarifa hiyo ya idara ya afya imetolewa juzi kwa mkuu wa mkoa wa Tanga,Martine Shigela na mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Lushoto Dk. Charles Mkombacheka alimweleza RC kuwa hali ya upatikanaji wa dawa kwa sasa ni asilimia 85 huku ukiwepo mpango wa kuwezesha dawa kupatikana.

Katika taarifa hiyo,Dk. Mkombacheka alisema,ili chumba hicho ‘Bufferstock’ kuanzishwa zinahitajika sh 113 milioni zilizopatikana kutoka KFW ili kuandikisha familia za akina mama wajawazito ambapo ‘Buferstock’ hiyo itakuwa tayari ndani ya wiki tatu kutoka sasa kukabiliana na upungufu wa dawa.

Kuhusu suala la msongamano wa wajawazito wodini,mganga huyo alisema kuwa kuboreka kwa huduma ya afya ya uzazi na mtoto katika hospitali ya wilaya imepeleka akinamama wengi kujifungulia hospitali na kuwa na msongamano ndani ya wodi na kusababisha wazazi kulala wawili ndani ya kitanda kimoja.

Aidha alisema,wastani wa idadi ya akina mama wajawazito wanaojifungua imeongezeka toka wajawazito 3 hadi wanne  mwaka 2013-2014 na kuwa nane hadi 12 kwa mwaka 2017 kwa siku wakati mpango wa muda mfupi wa utatuzi changamoto ukiwa ni ukarabati wa wodi moja iliyokuwa mbovu.

Pia,upo mpango wa kubadilisha matumizi ya ukumbi wa maktaba kuwa wodi ili kuongeza idadi ya wodi kutoka moja hadi tatu hali ambayo imesababisha idadi ya vitanda vya kulaza wazazi kuongezeka kutoka 27 hadi 50 na vitanda vya kujifungulia kutoka vitatu hadi sita ofisi ya DED ikiwezesha hili.

Aidha alitanabaisha kwamba ofisi hiyo ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Lushoto imefanikiwa kutekeleza hilo ikitumia kiasi cha sh 15,494,500 kwa kutumia mhandisi wa halmashauri na ‘loco fundi’ ili kupunguza gharama ambapo fedha zote hizo zimetokana na mapato ya hospitali.

Akizungumzia mpango wa muda mrefu katika kutatua changamoto ya msongamano wa wajawazito,mganga huyo alisema kwamba wanakusudia kujenga jingo kubwa ‘Maternity home comlex’ kwa ajili ya akina mama wajawazito kukiwa na wodi zote za akina mama wajawazito na watoto.

Alisema,kwa kuanzia halmashauri imetenga kiasi cha Tsh 50 milioni (2017/18) huku akisisitiza kusema kuwa ili kuweza kukamilisha jingo hilo kiasi cha Tsh 400 milioni zinahitajika ambapo kwa upande wake mkuu wa mkoa Martine Shigela alipongeza jitihada za halmashauri kufikia hatua hiyo ya maboresho.

Shigela aliahidi kutoa mifuko 150 ya saruji ili kutumika kujenga majengo mengine lengo likiwa kufanya upanuzi wa hospitali hiyo akisema hatua hiyo imeonyesha kuwa halmashauri imeguswa na utatuzi wa changamoto hiyo inayopaswa kuungwa mkono katika kuipatia upanuzi na kuondosha changamoto.

Alisema,Rais katika kuomba kura aliahidi kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo huduma kwenye sekta ya afya ambapo aliomba majengo hayo kutumika kama mpango wa serikali ambapo mkoa umejipanga hospitali ya Bombo kuwa ya rufaa ili kuwepo kwa uwezekano wa kupatikana madaktari bingwa wengi.

RC Shigela alisema kuwa,hatua hiyo itasaidia kuongeza ufanizi katika utendaji kazi  huku akibainsiaha kuwa duniani kote kupitia sekta ya afya inapoboreshwa inakuwa rahisi kwenye mpango wa kuharakisha maendeleo huku akisistiza kusema kuwa utamaduni maboresho sekta ya afya utakuwa endelevu.
Mwisho.
 Mkono wa kushoto ambaye amevaa suti ni mkuu wa mkoa wa Tanga,Shigela wa tatu mkono wake kushoto ni mkurugezi wa halmashauri hiyo,Makwega wakicheza ngoma ya asili siku ya ufunguzi huo wa wodi..

 Mganga mkuu wa hospital ya lushoto,Mkombacheka akitoa ufafanuzi kwa mkuu wa mkoa wa Tanga.

 Pichani katikakati ambaye amevaa sare ya CCM ni katibu wa chama cha mapinduzi wilayani Lushoto,Ramadhani Mahanyu akizungumzia miongoni mwa ahadi za rais Dk.John Magufuli ni kuboresha sekta ya afya.
 Pichani ni RC Tanga,Shigela akifungua majengo ya wodi za wazazi Lushoto,,
 RC Tanga,mara baada ya kufungua..
 Baadhi ya kina mama wajawazito wakiwa wamelazwa wodi hiyo mpya na muuguzi wa zamu..

 Picha ni baadhi ya wodi iliyofunguliwa,,
 Pichani ni mkuu wa mkoa huo akiwa na viongozi akitembelea akionyeshwa baadhi ya vitanda vikiwa nje kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati.
 Pichani katikati ambaye amekaka ni mkuu wa mkoa huo akizindua mpango wa magonjwa yasioambukiza wilayani Lushoto katika ziara yake ya siku mbili.

 RC Tanga akiwa kwenye moja ya vipimo katika uzinduzi wa mpango huo,,
 Pichani katikati ni mkuu wa wilaya ya Lushoto,January Rugangika akipima katika ziara hiyo,,
 Mkuu wa wa Tanga akiangalia baadhi ya majibu yake ya uzito.
Pichani ni mwenyekiti wa halmashauri ya Lushoto,Lucas Shemndolwa akipima presha siku ya uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment