Mwenyekiti mpya wa bodi ya TTCL, Omari
Nundu akiwaomba watanzania kutumia mawasiliano hayo ya TTCL ili kuliwezesha na kulipa
nguvu shirika hilo kufanya kazi kwa tija.
Pia alisema kuwa kujenga uzalendo kutumia huduma za TTCL itawezesha kuifanya nchi kuwa na nguvu kutokana na kuwa na
mashirika yake yanayotoa huduma kwa wananchi.
“Kiukweli tanzania haiwezi kusifika
kama hatuna vyombo vyetu wenyewe kwa maana ya mashirika yanayotoa huduma kwa
kiwango kikubwa,” alisema mwenyekiti huyo mpya wa bodi Nundu.
Mkuu wa mkoa Tanga akizungumza na wafanyakazi,,
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
SERIKALI mkoani Tanga,imewataka wafanyakazi wa Kampuni ya
Simu nchini hapa TTCL, kukubali kwenda na mabadiliko ya
teknolojia ya mawasiliano katika utoaji wa huduma bora.
Hata hivyo,imesema lengo kubwa likiwa kutoa huduma zitakazowavutia watanzania walio wengi kujiunga na mitandao yao ikiwemo ile mpya ya 4G LTE ya simu ya kampuni hiyo .
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela,ametoa kauri hiyo juzi katika uzinduzi wa huduma hiyo mpya ambapo alisema moja ya faida itakayopatikana kwa watanzania ni kujiunga na kutumia mitandao ya TTCL ili kusaidia kuongeza pato la Taifa.
”Wafanyakazi wa TTCL hili ni shirika la Umma lazima tubadilika,faida
itakayopatikana inakwenda kwenye mfuko mkuu wa serikali hazina ambayo itawezesha
kuwahudumia wananchi katika miradi mbalimbali kama elimu, afya, barabara"alisema RC Tanga.
RC
Shigela alisema kwamba upatikanaji wa fedha kupitia huduma hiyo
zitawezesha kusaidia mipango mbalimbali ya maendeleo iliyowekwa na
serikali ya awamu ya tano ya Dk.John Magufuli.
“Wakati umefika watanzania watumie
mtandao wa TTCL hasa watumishi wa serikali na kuhusu hili nikitembelea miradi
katika maeneo ya mkoa nitataka nipate taarifa ya idadi ya watu
ambao wanatumia mtandao wa TTCL"alisema Shigela.
Mwisho.
Wafanyakazi wa TTCL Tanga wakimsikiliza mkuu wa mkoa siku ya uzinduzi.
Pichani mkono wa kushoto ni kaimu Mkurugenzi wa TTCL,Waziri Kindamba, akieleza kwamba lengo la kuzindua huduma hiyo ya 4G ELT Jijini hapo ili
kwenda sambamba na fursa za kiuchuni zilizopo ikiwemo ujenzi wa bomba la mafuta
kutoa Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mjini hapa.
Mkono wa kushoto ni Kaimu mkurugenzi wa TTCL,Waziri mara baada ya uzinduzi wakimkabidhi RC Shigela mabango yenye ujumbe "Twaja leo Twabaki hapahapa Tanga Tumefanuikisha"kulia ni mwenyekiti mpya wa bodi,Nundu.
No comments:
Post a Comment