Sunday, 2 April 2017

UZINDUZI WA WIKI YA UPANDAJI MITI WILAYA YA KOROGWE ILIKUWA HIVI,,

 Pichani mkono wa kulia ni mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robart akiwasikiliza viongozi mbalimbali wakiwasilisha taarifa zao katika hafla ya uzinduzi wa upandaji miti.
 Pichani anayeongea ni diwani wa kata ya Makuyuni,Richard Mndolwa akizungumzia mkakati uliopo na kamati yake ni kuhakikisha kila mwanafunzi anapanda mti kuweka alama na kuwajenga na kulinda mazingira.
 Pichani ni mkuu wa shule ya sekondari Madago,Mzamilo Misanya akisoma taarifa yake ambapo aliiomba serikali kuwezesha kujenga uzio ili kuondoa changamoto ya uharibifu unaojitokeza kwa baadhi ya watu kufungulia  mifugo wakati wa usiku na kuharibu mazingira shuleni hapo.
 Pichani mkono wa kulia mwanamke ni Bi.miti wa halmashauri ya Korogwe vijijini,Hadija Kihamia akisoma taarifa ya halmashauri hiyo ambapo ina mpango wa kupanda miti 12 million.
 Pichani ni mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robart akizindua kampeni ya kupanda miti shule ya sekondari Madago wilayani hapo.
 Pichani ni mwenyekiti wa halmashauri ya Korogwe vijijini,Charles akipanda mti.


Pichani mkono wa kushoto ambaye amesimama ni mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robart akisoma taarifa yake katika hafla ya uzinduzi wa wiki ya upandaji miti halmashauri ya hiyo.

NA SOPHIA NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
MKUU wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel amesema kwamba kuna haja kwa kila kaya kupanda miti 10 ya aina mbalimbali ikiwemo ile ya matunda hatua ambayo italiwezesha Taifa kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi yanayochangia changamoto mbalimbali kujitokeza miongoni mwa jamii.
Mbali na kutoa maagizo kwa kila kaya kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti lakini pia kiongozi huyo wa wilaya aliwataka viongozi wa vijiji kudhibiti mifugo inayozurura ovyo hatua ambayo itasaidia kupunguza vitendo vya uharibifu wa mazingira ambao umekuwa ukisababishwa na mifugo hiyo.
Mhandisi Gabriel alitoa maagizo hayo wakati juzi alipokuwa kwenye Uzinduzi wa wiki ya upandaji miti ambayo ilifanyika huko Sekondari ya Madago iliyopo kata ya Makuyunji ambapo alitanabaisha kuwa uharibifu wa mazingira umechangia mabadilikop ya tabia ya nchi wilayani Korogwe.
Alisema,ushahidi ambao unadhihirisha athari za mabadiliko ya tabia ya nchi wilayani Korogwe ni kukosekana kwa mvua za uhakika ambapo hapo awali hali ilikuwa shwari kwa mvua za vuli kunyesha kuanzia mwezi wa tisa huku masika ikiwa mwezi wa februari tofauti na hali inavyoendelea sasa.
Ili kukabiliana na hali hiyo,Mhandisi Robart  alisema kwamba jamii inatakiwa kubadilika kwa kuhakikisha inapanda miti huku ikiepuka vitendo ambavyo vinachangia uharibifu wa mazingira ambapo aliwataka viongozi wa vijiji,kata na tarafa kushirikiana na wataalam wa misitu kusimamia upandaji miti.
Mhandisi Robart pia alitumia fursa hiyo kuagiza ukusanywaji takwimu sahihi za miti iliyopandwa na wananchi na viongozi wa vijiji kuheshimu sheria zilizopo sanjari na kuimarisha usimamizi wa sheria iliyopo,kufuata utaratibu wa uvunaji miti asilia huku maeneo ya hifadhi ya misitu yakiendelea kutengwa.
Pia mkuu huyo wa wilaya ya Korogwe alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi kuhusu suala la upungufu wa chakula akiwataka kupanda mazao yanayostahimili ukame akitolea mfano zao la mihogo hatua aliyoieleza kuwa itawawezesha kukabiliana na changamoto ya upungufu wa chakula.
“Tuzitumie mvua hizi kikamilifu kupanda mazao yanayohimili ukame na hata yalke ya muda mfupi,ni vyema kwa watu kutenga angalau ekari moja kulima mihogo inasaidia sana pindi kunapojitokeza suala la upungufu wa chakula”alisema mkuu huyo wa wilaya ya Korogwe Mhandisi Robert .
Mkuu huyo wa wilaya aliwashukuru wananchi wa tarafa ya Mombo,kata ya Makuyuni,walimu na wanafunzi wa sekondari Madago kwa mapokezi na ushirikiano katika kufanikisha shughuli hiyo ya utunzaji mazingira ambapo kila mwaka siku ya upandaji miti na uzinmduzi wake hufanyika Aprili mosi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa kwa mkuu huyo wa wilaya jumla ya miti 1,500,000 inatarajiwa kupandwa, miti 500 imepandwa eneo la uzinduzi hapo Maqdago sekondari huku miti ipatayo 1,499,500 inatarajiwa kupandwa kwenye kata mbalimbali zilizopo kwenye halmashauri  ya wilaya Korogwe.
Awali akizungumza katika uzinduzi huo diwani wa kata ya Makuyuni,Richard Mndolwa alisema kwamba kamati yake na kuweka mkakati endelevu juu ya utunzaji mazingira kuanzia wanafunzi kupanda miti.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment