Pichani ni kamanda wa polisi mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba akisoma taarifa baada ya operesheni iliyofanyika katika bandari bubu ya kigombe wilayani Muheza.
NA SOPHIA WAKATI.TANGA
SHEHENA za bidhaa za magendo zikiwemo Sukari,mafuta ya kula
na mchele zimekamatwa na jeshi la Polisi mkoani Tanga zikiwa zikekamatwa zikiwa
zinateremshwa kwenye Bandari Bubu ya Kigombe iliyopo huko wilayani Muheza huku
wamiliki wake wakiwa wanaendelea kusakwa ili hatua stahiki kuchukuliwa.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga Benedict Wakulyamba alitoa
taarifa hiyo jana wakati alipokuwa akizunbgumza na Gazeti hili huku akibainisha
kuwa miongoni mwa bidhaa hizo za magendo zilizokamatwa kuna Sukari mifuko
64,mafuta ya kula aina ya OKI madumu 364 na mchele mifuko 10.
Kamanda wa Kulyamba alisema sukari hiyo ni ile ya kutoka
nchini Brazili wakati mchele ukiwa umetoka Pakistani na mafuta ya kula yametoka
Indonesia ambapo bidhaa hizo zote zilikuwa zimepakiwa kwenye Jahazi lenye
nambari Z 1221 MV linalotambulika kwa jina la YARAZAKI huku mmiliki akikosa
kujulinaka.
Alisema kuwa polisi kwa kushirikiana na maafisa wa TRA,Uvuvi
doria waliweza kukikamata chombo hicho kilichokuwa na bidhaa hizo za magendo
huko bandari Bubu ya Kigombe kata ya Kigombe wilayani Muheza ambapo bado mpaka
sasa thamani halisi ya vitu vinavyoshikiliwa haijaweza kufahamika.
Aidha kamanda Wakulyamba alisema kuwa jeshi la polisi
linaendelea kumsaka Nahonda wa Jahazi hilo mmiliki wa chombo na mwenye bidhaa
ambazo zilikuwa zikisafirishwa huku akifafanua kuwa mifuko 10 ya mchele uzito
wake kila mmoja ilikuwa kilogramu 50,sukari kila mmoja kilogramu 50 na hayo
mafuta.
“Tunaendelea kuwasaka wale wote wanaohusika na kusafirisha
mzigo huo wa magendo ambapo mpaka sasa hatujafanikiwa kuwanasa,tunamtafuta
Nahodha,mmiliki wa chombo na hata mwenye mzigo ambao ulikuwa ukisafirishwa ili
hatua za kisheria kuweza kuchukuluiwa”alisema kamanda Wakulyamba.
Ametoa wito kwa wafanyabiashara kufuata mfumo rasmi ili kulipa
kodi kwa ustawi wan chi yetu huku akiasa tabia za baadhi ya wafanyabiashara
kujihusisha na magendo jambo ambalo kisheria halikubaliki ambapo linaweza
kumsababishia mshiriki wa shughuli hiyo kupatwa na matatizo yasiyo na msingi.
Mwisho.
NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
JESHI la polisi wilayani Korogwe mkoani Tanga,liko kwenye
opresheni kumsaka mkazi mmoja wa Magunga wilayani hapo,Ibrahim Kichele (40)kwa
tuhuma za kumnyonga kichanga cha miezi minne Ramadhan Ibrahim na kumtupa porini
kwa kile kilichodaiwa ugomvi wa kifamilia na wivu wa kimapenzi.
Hata hivyo,habari ambazo sio rasmi zilieleza kwamba chanzo
cha ugomvi huo ni Ibrahim Kichele alipata taarifa kutoka nje kwa majirani kwamba
kichanga hicho sio mtoto wake chake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba akidhibitisha
alisema tukio hilo limetokea juzi saa 8.00 usiku huko katika kijiji cha
Kwasamangube kilichopo wilayani Korogwe.
Alisema kuwa siku ya tukio mtuhumiwa Ibrahim Kichele
alikwenda nyumbani kwa mama mkwe wake alikokuwa akiishi mtaraka wake
aliyefahamika kwa jina la Hadija Kitigo (26) ambaye walitengana mwaka mmoja
uliopita.
Kamanda Wakulyamba alisema baada ya kufika kwa
mkwewe huyo kugonga na kuingia ndani kwenye chumba alichokuwa akiishi mtaraka
wake ambaye alizaa nae watoto wawili.
“Baada ya kuingia ndani ya chumba alichokuwa akiishi
mtaraka wake Hadija mara kulizuka ugomvi uliopelekea kumchoma kisu sehemu ya shavu na mkono wa kulia na kuondoka
na kichanga kutokomea nacho kusiko julikana”alisema.
Kamanda Wakulyamba alisema maiti kichanga hicho ilipatatika
March mosi,mwaka huu mchana katika kichaka huku kikiwa kimeuwawa kwa kunyongwa
na kubamizwa kwenye fuvu lake la kichwa.
Aidha alisema taarifa za tukio hilo ziliwasilishwa
kituo cha polisi wilayani Korogwe na uongozi wa kijiji hicho cha Kwasamangube Magunga
wilayani hapo.
Alibainisha kwamba polisi walifika eneo la tukio na
kumkuta mwanamke huyo akiwa amelala chini huku akijiuguza ambapo walimchukua na
kumkimbiza hospital ya Magunga kwa matibabu na kufanya msako katika maeneo
mbalimbali.
Akizungumza na Uhuru,Aziza Ramadhani ambaye ni mama
mkwe wa Hadija alisema mkwe wake alifika nyumbani kwake mapema kama ilivyo
desturi yake ya kwenda kumbembeleza mkewe kwa lengo la kurudiana na kuwajulia
hali watoto wake ndipo kuzuka kwa vurugu hizo.
Mwisho.
Pichani
ni kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba jana
akizungumzia sakata la mkazi wa Kwasamangube Kichele aliyemcharanga
mtaraka wake mapanga na kutokomea na kichanga cha miezi 4 kutimiza lengo
lake la kukinyonga kwa wivu wa kimapenzi.
No comments:
Post a Comment