Tuesday, 17 March 2026

WADAU WA MASHINDANO YA DUVII RAMADHANI CUP 2026 KASERA YATUMIKA KUINUA UCHUMI KWA WAJASIRIA MALI,,,


Picha ni Mratibu wa mashindano hayo,Gidion Zumba amesema kuwa mashindano ya Duvii Ramadhani Cup 2026 kusaka washindi mbalimbali huku kufanyika usiku wilayani hapo,lengo kusaka washindi watatu ambao watapata medani na pesa tasilimu.

Na Sophia Wakati,Mkinga

TIMU za soka 48 zimejitokeza wilayani Mkinga mkoani Tanga kushiriki mashindano ya Duvii Ramadhani CUP 2026 kuwania zawadi mbalimbali ikiwemo pesa tasilimu.

Mratibu wa mashindano hayo,Gidion Zumba amesema kuwa mashindano hayo ambayo niya kwanza kufanyika usiku wilayani hapo,lengo kusaka washindi watatu ambo watapata medani na pesa tasilimu.

Alisema kwamba mshindi wa kwanza katika mashindano hayo atakabiziwa pesa tasilimushilingi million 2,000,000,mshindi wa pili million 1,000,000 na watatu 500,000 .

Aidha alibainisha kueleza kwamba zawadi nyingine   ni mchezaji bora shilingi 200.000,mfungaji bora shilingi 200,000 na kipa bora 100,000 sambamba na kupatiwa medani.

Mratibu Zumba alisema kuwa mashindano hayo yanafanyika usiku katika uwanja wa soka Kasera  wilayani hapo kwa mtindo wa mtoano.

'' Mashindano haya yalipangwa kufanyika mwaka jana kwa kuweka maandalizi ya uwanja,lakini kutokana na kujitokeza sababu mbalimbali ilishindikina na kupelekea kufanyika mwaka huu 2026''alisema Mratibu huyo Zumba.

Mratibu Zumba alisema mashindano mbalimbali yamewahi kufanyika katika tarafa mbalimbali yakifahamika kwa jina la Samia Mkinga Cup 2025 ambayo yalishirikisha timu 126 washindi walipata mnyama ng'ombe, mbuzi,jezi na pesa tasilimu.

Katika mashindano hayo yakiendelea kufanyika timu shiriki katika mashindano hayo, zimekuwa zikinufaika na jezi,mipira na pesa tasilimu 100,000 ikiwa ni sehemu ya maandalizi.

Alisema michuano hiyo ya Samia Cup ambayo yalisaidia kupata timu nane bora kila tarafa ambapo walipatikana mshindi alipata shilingi 1,000,000 na ng'ombe,wa pili mbuzi na 500,000 huku wa tatu akizawadiwa 300,000 na mshindi wanne 100,000.

Hata hivyo,Mratibu Zumba alisema michezo ni muhimu sana kwani husaidia vijana kuweza kujiajiri,kupata kipato na kuweza kuondokana na kujiingiza kwenye makundi hatarishi kupoteza ndoto zao.

''Mashindano ya Duvii Ramadhani Cup hayana kiingilio hivyo amewataka vijana kutumia fursa hiyo kuonyesha vipaji vyao ili kuweza kuonekana''alisema Mratibu huyo Zumba.
Mwisho.


Na Sophia Wakati,Mkinga
WADAU wa michezo Kasera wilayani Mkinga wamempongeza mdhamini wa mashindano ya Duvii Ramadhani Cup ambayo yanasaidia kuleta faraja kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Timu ya Soft Toch yenye masikani yake Kasera wilayani Mkinga,Said Kassim amesema michuano hiyo imekuwa mkombozi kuamsha ari kwa jamii.

Amesema kwamba timu hiyo imeshirikisha vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Mkinga lengo kuonyesha vipaji na kuwania zawadi zilizopo.

Said amesema mashindano hayo ambayo yanafanyika usiku niya kwanza yametokea kukubalika kwa wadau ikiwemo vilabu.

''Mashindano ya Duvii Ramadhani Cuo 2026 yameweza kusaidia kuonyesha vipaji mbambali vya michezo vilivyopo wilayani Mkinga kwani tumekuwa tukishuhudia mashindano ya usiku maeneo mengine.

''Kwa mashindano haya tunampongeza mdhamini wa mashindano haya Duvii na muandaaji wake Zumba kuleta burudani hizi kwa vijana kutoka wilaya ya Mkinga''alisema Mwenyekiti wa timu ya Soft Said.

Hata hivyo,amesema tayari vijana wamepata uzoefu na mechi za usiku pia amewataka wadau wa michezo kuendelea kumuunga mkono mdhamini na mwandaaji ili kuweza kuwa endelevu kufanyika wilayani hapo.
Mwisho.





Timu ya soka Mtundani imepata nafasi ya kusonga mbele mashindano ya Duvii Ramadhani Cup baada ya kuifunga wapinzani wao Veterani kwa kwa goli 1-0.

Mchezo huo wa mwendelezo wa vuta nikuvute kwa pazo zote kuonyesha vipaji vya mchezo wa soka,umefanyika saa 10 jioni katika uwanja wa soka Kasera uliopo wilayani Mkinga,

Mtundani imefanikiwa kuandika goli lake mnamo dakika ya 21 kupitia kinara wa timu hiyo,Athumani Mwarasi ambalo limeweza kudumu mpaka dakika 90 mwisho wa mchezo huo.
Mwisho.


Mwenyekiti wa kitongoji Kasera,Rajabu Juma amesema mashindano ya Duvii Ramadhani Cup yamekuwa chachu kwa kina kuyatumia kufanya biashara mbalimbali.

Amesema Wakinamama wananufaika kufanya biashara ndogondogo kwa kiwango kikubwa na hufanyika muda mzuri usiku ambapo niyakwanza kufanyika na kuwavutia wadau wengi.


Pia ametumia nafasi hiyo kumuomba mdhamini wa mashindano hayo Rashid Duvii kuwa endelevu kufanyika kila mwaka ili wananchi waweze kufanya biashara na vijana kuweza kuibua vipaji vyao.

Mwenyekiti huyo wa kitongoji,Rajabu ameomba kufanyika maboresho ya kiwanja hicho ili kuwezesha kuzishu 

No comments:

Post a Comment