Pichani mkono wa kulia mwanamke ni katibu tawala wa mkoa wa Tanga,Zena Said ziara yake akitembelea mabanda la halmashauri ya Handeni maonyesho ya tano ya biashara mwahako mkoani hapo,
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
SERIKAL mkoani Tanga imezitaka kada
za vijana na wakina mama kuelewa kwamba mikopo wanayopatiwa siyo zawadi na
wanapaswa kurejesha baada ya kuitumia katika kutekeleza miradi yao ya uzalishaji
mali huku lengo likiwa kuweza kujikwamua kiuchumi.
Kauli hiyo imetolewa juzi na katibu
tawala mkoa wa Tanga,Zena Said wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho ya
biashara huko eneo la Mwahako Jijini Tanga huku akielezea kutoridhishwa kwake
na ushiriki mdogo wa kada ya vijana katika shughuli hiyo ambayo ingekuwa fursa
kwao kujikwamua.
Alisema kuwa serikali yao imekuwa
ikitoa fedha kupitia kila halmashauri ambapo kuna asilimia zilizotengwa maalum kwa
ajili ya makundi hayo ili kuweza kutumika kwa kuendesha shughuli
mbalimbali za uzalishaji mali akiwataka kuitumia vyema fursa hiyo katika
kuanzisha miradi ya kimaendeleo.
Katibu tawala huyo,Zena alisema
kwamba fedha hizo ambazo ni mikopo sio kama zinatolewa kama zawadi na zimelenga
kuwasaidia kuendesha shughuli za kiuchumi huku akisema wale watakaobahatika
kupewa fedha hizo wanapaswa kuzitumia kuendesha miradi na kurejesha hatua
ambayo itasaidia wenzao kukopeshwa.
“Kiu kweli zipo asilimia
mnazopaswa kukopeshwa sio kwamba zinatolewa tu bali ni mkopo unaotolewa kwa
utaratibu ili uwasaidie kuendesha shughuli zenu “serikali imedhamiria
kuwasaidia vijana hivyo ni juu yenu kujitokeza kwa kufuata masharti ya kujiunga
vikundi na kuweza kuzitumia hizo fursa “alisema Zena.
Aidha,alibainisha kwamba lengo kubwa
la serikali ni kuwawezesha vijana kupata mitaji kuendesha biashara zao huku
akiwasihi wakazi wa Jiji la Tanga kujitokeza kwa wingi ili kuweza kujionea
shughuli mbalimbali zinazofanywa na mashirika na taasisi za umma na pia
wajasiriamali kupata kufaidika na fursa zilizopo.
Katibu tawala huyo ametumia nafasi
hiyo kutoa angalizo kwa vijana na wanawake wasio na fedha kujitokeza ili
kukopeshwa na kuondokana na dhana ya kuona kile wanachopatiwa kuwa ni sawa na
zawadi bali imelenga kuwaendeleza mitaji yao akiwataka kufuata taratibu stahiki
za masuala ya mikopo.
Naye,Mtani Manundu ambaye ni
afisa mshauri wa biashara wa Benki ya CRDB jijini Tanga amesema kwamba wamekuwa
wakiyatumia maonyesho hayo katika kuielimisha jamii namna ambavyo wanaweza
kunufaika na mikopo kutoka kwenye asasi za fedha ikiwemo benki yao kwenye
matawi mbalimbali.
Vile vile Augustino Kasale ambaye ni
Afisa uhusiano wa serikali alisema shirika la maendeleo ya Petrol Tanzania TPDC
wanatumia maonyesho hayo kuelimisha jamii kuona fursa ikiwemo ile ya gesi
kupitia mradi mkubwa wa bomba la mafuta akiamini kwamba wananchi walio wengi
watanufaika.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment