Pichani ni katibu wa CCM halmashauri ya Korogwe mjini akitoa maelekezo kabla ya uchaguzi kwa wajumbe halali wenye sifa ya kupiga kura.
Pichani ni baadhi ya wajumbe wa halmashauri ya Korogwe mjini mara baada ya kukamilisha zoezi la kupiga kura wakisikiliza matokeo ukumbi wa halmashauri hiyo.
MKUTANO mkuu wa uchaguzi kwa Chama cha map[induzi CCM
Korogwe Mjini umefanyika jana kwenye ukumbi wa halmashauri ya Mji ambapo Kada Mwenyekiti
Emmanuel Chale amefanikiwa kutetea vyema wadhifa wake baada ya kuwabwaga
wanachama wengine wawili waliokuwa wakiwania kiti hicho.
Katika kinyang’anyiro hicho cha nafasi ya mwenyekiti Chale aliyepata
kura 205 alikuwa akichuana na Iddi Sad Mdoe na Athuman Magogo ambapo kwa nafasi ya mkutano mkuu wa Taifa
wagombea walikuwa tisa (9) huku Dk Frank Mhilu,Mjata Daffa na Asia Kingongo
wakipata wasaa wa kuwa wawakilishi.
Uchaguzi huo pia ulihusisha upatikanaji wa nafasi za wajumbe
kutoka vijana kwenda halmashauri kuu ambao walipita bila kupingwa ni Ally
Chamzimu,Mujibu Salim,Muntalla Mkesa na Pascal Itemo wakati Anna
Kanyika,Mariamu Lyagoda na Rose Magembe walifaniweza kuwa wajumbe kwenda UWT.
Mbali na nafasi hizo pia uchaguzi huo ulimchagua
mwanaharakati wa masuala ya mazingira Revocatus Njau kuwa katibu mwenezi wa
chama cha mapinduzi CCM Korogwe Mjini akifanikiwa kuwabwaga wenzake watatu huku
Elizabeth Haule na Allen Kingama wakitwaa nafasi ya mkutano mkuu mkoa.
Walioshinda nafasi ya halmashauri kuu kwenda wazazi ni
Thobias Nungu na Raphael Mbughuni ambapo mara baada ya matokeo hayo yote
kutangazwa mwenyekiti wa CCM wilaya aliyechaguliwa Emmanuel Chale alitumia
fursa hiyo kuwasihi wanachama kuimarisha mshikamano ili kuweza kujenga chama chao.
Chale alisema kuwa ili kuweza kuimarisha chama chao kwa
kuondosha makundi huku akisistiza kusema kuwa uchaguzi ulishamalizika na sasa
kila mwanachama anapaswa kutumia mafasi aliyonayo kukitumikia chama kwa maslahi
ya umma akisema kwa pamoja wanapaswa kumuunga mkono Rais kuchapa kazi.
Wakati Korogwe Mjini wakihitimisha uchaguzi huo nako Korogwe
vijijini kwenye ukumbhi wa chuo cha Ualimu TTC kulifanyika uchaguzi wa aina
hiyo uliomwezesha Hemed Nassoro ‘Malingumu’ kunyakua nafasi ya mwenyekiti akifanikiwa
kumbwaga kwa mbali kada wa chama hicho tawala Rajabu Kaniki.
Katika kinyang’anyiro hicho cha wadhifa wa Mwenyekiti Malingumu
alitetea nafasi yake hiyo kwa kupata kura 745 wakati Kaniki akipata 141 na kwa
nafasi ya katibu mwenezi aliyefanikiwa kushika wadhifa huo ni Ally Waziri kwa
kura 98 akiwa miongoni mwa wanachama waliofanikiwa kutetea nafasi zao za awali.
Wazi alikuwa akichuana na Bakari Rashidi aliyepata kura 10,Peter
Mfumya kura 10 na Salimu Mhando kura moja uchaguzi ambao ulilazimika kurejewa
mara ya pili baada ya kujitokeza mkanganyiko kwa kura kudaiwa kuongezeka katika
hatua za awali kwa mafasi hiyo ya kumpata mwenezi wa chama hicho.
Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo kumalizka mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi CCM Korogwe Vijijini Hemed Nassoro ‘Malingumu’ alisema
CCM ya mazoea imepitwa na wakati na hata ile iliyokuwa ikionekana kuwa legelege
ama ya makundi haipaswi kuendelea kuwepo zaidi ya kuchapa kazi.
Aliwataka wanachama wa chama hicho tawala kuelekeza nguvu
zao katika uchaguzi wa serikali za mitaa hapo mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa
madiwani,ubunge na Rais kwa mwaka wa 2020 akisisitiza kusema kuwa kuna kila
sababu kwa CCM kuendelea kushika dola kwa maslahi ya watanzania wote.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment