Pichani wa pili mkono wa kushoto ambaye anatabasamu ni Waziri wa elimu Sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako mara baada ya ziara yake wilayani Korogwe mara baada ya kufungua na kuweka jiwe la msingi miradi ya shule.,
Pichani wa pili mkono wa kushoto ambaye anaongea ni Waziri wa
elimu Sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako mara baada ya ziara yake wilayani Korogwe,akizungumzia mpango uliopo kwa serikali kwamba hadi
kufikia mwaka 2020 hakutakuwa na shule yenye vyumba vya madarasa vya nyasi,kushoto mwanaume ni mkuu wa wilaya hiyo,Mhandisi Robart Gabriel,wa tatu ni mbunge wa jimbo la Korogwe mji,Mery Chatanda akifuatiwa na mkurugenzi wa halmashauri ya Korogwe mji,Jumanne Shauri kulia..
NA SOPHIA
WAKATI,KOROGWE
WAZIRI wa
elimu Sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema kwamba hadi
kufikia mwaka 2020 hakutakuwa na shule yenye vyumba vya madarasa vya nyasi.
Profesa
Ndalichako ameyasema hayo juzi katika ziara yake ya siku moja wilayani Korogwe
alikotembelea kufungua na kuweka jiwe la msingi baadhi miradi ya shule za
halmashauri ya Korogwe Mjini.
Alisema, kwa
kasi ambayo inaendelea kwenye uboreshaji miundombinu ya sekta ya elimu ili
kuwawezesha watoto kupata elimu itakayokuwa na ubora unaokubalika.
Profesa
Ndalichako alitumia fursa hiyo kupongeza jitihada za ujenzi zilizoonyeshwa
wilayani Korogwe akitaka mshikamano huo kuendelea kuwepo kati ya Viongozi na
wananchi.
"Kumekuwa
na propaganda za kuwakatisha wananchi tamaa, ila niwaombe endeleeni kumuunga
mkono rais Dk.John Pombe Magufuli na kushirikiana nae na lazima muelewe
wananchi mnayo nafasi kuchangia maendeleo yenu "alisema.
Aidha
Profesa Ndalichako aliongeza kwa kubainisha kuwa rais Dk. John Magufuli
anapenda watu wanaojituma na kwa aliyoyaona Korogwe hatosita kumfikishia
salaam.
Aidha,
aliwataka walimu kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi na kuwajengea uzalendo
watoto hatua itakayowawezesha kupenda nchi yao.
Pia,ametumia
nafasi hiyo kuwaasa wanafunzi kutokubali kutoa fursa kwa watu ambao kila uchao
wamekuwa wanawaza kupoteza amani ya nchi ambayo imekuwa gumzo kwa miaka
mingi.
Katika ziara
hiyo ya Profesa Ndalichako, mkuu wa wilaya ya Korogwe Mhandisi Robert Gabriel
alimweleza Waziri huyo kuwa, Korogwe imejidhatiti kufanya kazi badala ya
kuruhusu migogoro.
"Kiukweli
Korogwe tunataka kazi ndio ziongee, hatutaki maneno na nikuahidi mheshimiwa
Waziri sisi tutaendelea kuchapa kazi "alisema mkuu huyo wa wilaya ya
Korogwe.
Vilevile
mkuu huyo wa wilaya alimweleza Waziri kuwa jitihada za ziada zimekuwa
zikifanyika kufanikisha ujenzi wa mabweni ili kuwaondoshea changamoto watoto wa
kike.
"Ukimlinda
mtoto wa kike utakuwa umelinda Taifa, tumeamua kumpa mtoto wa kike elimu na
tunajenga mabweni ili kuwawezesha kutimiza hatma yao ambayo pia ni hatma ya
Taifa "alisema DC Mhandisi Gabriel.
Wakati
akizindua bweni kwa shule ya Sekondari Semkiwa Profesa Ndalichako aliahidi
kufanya kila liwezekanalo kupata magodoro ili kuwawezesha watoto kuyatumia
mabweni hayo haraka iwezwkanavyo akiahidi sh 10 mil.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment