Sunday, 8 September 2024
TANGA CITY MARATHON 2024 IMESEMA MAANDALIZI YAMEKAMILIKA KWA UPANDE WA ZAWADI NA KUWATAKA WASHIRIKI WENYE SIFA KUJITOKEZA,,,,,
Thursday, 29 August 2024
HOME GUARD FC, SMALL PRISON ZAAGA MASHINDANO ULINZI CUP TANGA
Mratibu wa Mashindano ya Ulinzi Cup Sophia Wakati akikagua timu za soka Small Prison na Home Guard kabla ya kuanza mchezo wao katika uwanja wa soka Ziwani Pongwe Jijini Tanga |
Na Sophia Wakati, TANGA.
TIMU za soka Small Prison na Home Guard zimeaga Mashindano ya Ulinzi Cup baada ya kila mmoja kufungwa katika mchezo wa hatua ya mtoano inayoendelea kwenye viwanja vya Ziwani Pongwe Jijini Tanga.
Mashindano hayo yanaratibiwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga yakiwa na lengo la kutoa elimu kwa vijana kujiepusha na vitendo vya uhalifu katika jamii wanazoishi ikiwemo kuwa mabalozi wa amani kwenye maeneo yao
Katika mchezo wa awali wa ufunguzi wa mashindano hayo timu ya soka TFC waliigaragaza Home Guard bao 1-0 bao ambalo lilifungwa na Mohamed Saidi dakika ya 5 hya mchezo huo ambao ulikuwa na upinzani.Mratibu wa Mashindano ya Ulinzi Cup Sophia Wakati kushoto akitoa elimu kwa wachezaji wanaoshiriki mashindano hayo kuhusu lengo la mashindano hayo kuunga urafiki baina ya Polisi na Jamii
Huku mchezo wa pili uliochezwa Agosti 21 mwaka huu timu ya Chote FC waliweza kuwapigisha kwata maafande wa Jeshi la Magereza Small Prison bao 1-0 ambalo lilifungwa na Boniface Majere dakika ya 47.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mashindano hayo,Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kuhakikisha Jeshi la Polisi linakuwa karibu na Jamii jambo ambalo ni muhimu katika kuhakikisha kuimarisha ulinzi.
Mbaraka alisema kwamba kufanyika kwa mashindano hayo katika maeneo mbalimbali yanasaidia na kuwawezesha vijana kuweza kuyatumia kama njia muhimu ya ajira,kujenga afya pamoja na kusaidia kuwaondoa vijana kwenye masuala ya uhalifu na dawa za kulevya na wanaamini mashindan hayo yatakuwa chachu kubwa ya kuinua vipaji vya wachezaji.
Naye kwa upande wake Mratibu wa Mashindano hayo Sophia Wakati alivitaka vilabu vinavyoshiriki kwenye mashindano hayo kuhakikisha wanazingatia sheria 17 za mpira wa miguuu zilizowekwa ikiwemo kuacha kuwachukia waamuzi.
“Lengo la Mashindano hayo ni kujenga undugu baina ya Jeshi la Polisi na Jamii lengo kujenga urafiki msijengeane chuki hakikisheni mnacheza kwa kuzingatia nidhamu ambayo itakuwa chachu ya mafanikio kwenye jambo lolote lile lakini msiwachukie waamuzi kutokana na kwamba wakati mwengine kunakuwa na makosa ya kibinadamu”Alisema
Mwisho.
HALMASHAURI ZA MKOA WA TANGA ZATAMBA KUYATUMIA MAONYESHO YA NANE NANE 2024 KUTANGAZA FURSA ZILIZOPO
Pichani ni Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Mkinga Faizu Nyoni akionyesha miongoni mwa mazao yanayolimwa wilayani humo |
NA SOPHIA WAKATI,MOROGORO
WAJASIRIAMALI kutoka wilaya ya
Mkinga Mkoani Tanga, wameyatumia maonesho ya Kilimo nane nane kwa mwaka huu
katika kutanua wigo wa masoko hatua ambayo lengo lake ni kuongeza tija kwa
uzalishaji wa bidhaa.
Afisa Kilimo Mkinga,Faizu Nyoni
ameyasema hayo juzi Mkoani Morogoro kwamba, maonesho ya mwaka huu
yameongeza elimu kwa wajasiriamali na pia kuwawezesha kutanua wigo wa masoko.
Alisema, Halmashauri ya Wilaya ya
Mkinga imewawezesha wananchi kada mbalimbali kushiriki maonesho hayo ili
kuweza kujifunza vitu vingi huku wakibadilishana mbinu za uzalishamali.
"Tumekuja na wakulima ambao
wamediriki kuchukua mbegu za mazao wakatumie kule tulikotoka, pia tumekuja na
wajasiriamali mbalimbali wakiwemo vijana waliokopeshwa mikopo ya asilimia
kumi" alisema.
Kwa upande wa vijana hao
waliofanikiwa kupata mikopo ya asilimia kumi, afisa Kilimo huyo alisema, hao
walinunua mashine kutengeneza masweta na kwamba kuwepo kwao Morogoro
kumewasaidia kuongeza wigo wa soko.
"Hapa wasiliamali tumewapa muda
wanatembea kupata Connection wateja kuwa wengi" alisema afisa Kilimo huyo
huku akitanabaisha kwamba Kilindi wanazalisha mazao ya biashara na chakula.
Amesema kwamba tayari wamefanya
uhamasishaji wa zao la Korosho ambapo kwa kipindi cha mwaka jana wameanza
matarajio yao yakiwa ni kutaka kuanzisha Amcos kwa sababu Korosho haziuzwi kwa
njia za kawaida.
Pia wilaya ya Mkinga imeanzisha
Kilimo cha zao la Pamba na pia wamekuwa wakizalisha lishe jambo ambalo kwa
kiasi kikubwa limesaidia kuiimarisha lishe ya wananchi hususani watoto.
Miongoni mwa wajasiliamali Duga
Sigaya wilayani Mkinga,Elina Mumba amesema amenufaika na maonyesho ya nanenane
kwa kutangaza bidhaa zake zinazotokana na zao la Muhogo na Korosho baada ya
kupatiwa mikopo na halmashauri.
Mwisho
NA SOPHIA WAKATI,MOROGORO
WAKULIMA wa zao la Mkonge wilayani
Mkinga wameiomba Serikali kuwaangalia wakulima wadogo kwa jicho la huruma katika
kuwapatia mikopo ya muda mrefu, hatua ambayo itawawezesha kuendesha kilimo
hicho kwa ufanisi.
Meneja wa Kampuni ya Duvii Farm
inayohusika na Kilimo na uchakataji Mkonge wilayani Mkinga, Robert Rashid Duvii
alitoa Rai hiyo juzi kwenye kilele cha maonesho ya wakulima nanenane Mkoani
Morogoro.
Duvii alisema kwamba maonesho hayo
yamewasaidia wakulima mbalimbali kujifunza mambo mengi sambamba na kuona
jitihada za Serikali katika kuhakikisha wananchi wanaelimika.
Alisema kuwa, katika uzalishaji wa
zao la.Mkonge manufaa makubwa yameanza kupatikana ingawa wakulima wanakabiliwa
na changamoto ya miundombinu sanjari na suala la mikopo kwa wakulima wadogo
wadogo.
Alisema, kwa mkulima mdogo ili
kuweza kuangalia Shamba lake na kupata mazao yenye ubora inamchukua muda mrefu
na mara nyingi wamekuwa wakikwama kwa kukosa mikopo ya muda mrefu.
"Kwa upande wa Mkonge Serikali
iangalie namna ya kutoa mikopo ya muda mrefu,mkulima akishindwa kuangalia
shamba vizuri atashindwa kupata product nzuri "alisema Duvii.
Akizungumzia changamoto ya
miundombinu, Meneja huyo wa Duvii Farm alisema,pamoja na zao la Mkonge kwa
sasa kuonekana kuwa na manufaa makubwa.Ukosefu
mashine za uchakataji ni changamoto kwa wakulima.
Aidha Meneja huyo alisema, Duvii
Farm wanazo mashine mbili ikiwemo ile ya kuhamahama 'mobile' huku wakiwa katika
mchakato wa kununua mashine kubwa ya Korona itakayokuwa mkombozi kwa wakulima
wadogo.
"Sisi tunazo mashine mbili moja
ni Moverable na nyingine ni Stored pale pale. Viwanda vikubwa vipo vichache na
wakulima ni wengi nadhani bodi ya Mkonge walishaelezwa watafute mashine zao ili
kusaidia wakulima" alisema Robert Duvii.
Pamoja na kuyasema hayo, Duvii
alitumia nafasi hiyo kusema kuwa wanakusudia kuleta mashine kubwa itakayokuwa
na uwezo wa kuchakata tani nne kwa muda wa saa moja na kwamba itakapokuja
itakuwa mkombozi wa wakulima wa Mkinga.
Mwisho.
NA SOPHIA WAKATI,MOROGORO
RIADHA TANGA KUMPA USHIRIKIANO MUANDAAJI WA MASHINDANO YA TANGA CITY MARATHON
CHAMA cha Riadhaa Mkoa wa Tanga (RT) kimesema kwamba kitampa ushirikiano wa kutosha muandaaji wa Mashindano ya Riadhaa ya Tanga City Marathon ili kuweza kuondoa changamoto zilizojitokeza msimu uliopita na yaweze kuwa na tija na mafanikio makubwa.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Chama cha Riadha (RT) Mkoani Tanga,Sophia Wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu namna walivyojipanga kuhakikisha wanampa ushirikiano wa kutosha muadaaji huyo ili mashindano hayo yaweze kufanyika kwa ufanisi.
Alisema pia kuweza kufanyika vizuri kwa kufuata taratibu zote za Mashindano hayo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga kupitia Afisa Michezo Mkoa
“Mbio hizi za Tanga City Marathon ni mashindano muhimu kwa mchezo wa Riadha mkoani hapa na kwa sasa tumeyaingiza kwenye kalenda ya Mkoa na sasa yatakuwa yakifanyika kila mwaka na sisi RT kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga tutatoa ushirikiano wa kutosha kwa waandaaji”Alisema Sophia Wakati.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Septemba 22 mwaka huu ambapo yataanzia kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort na kuzunguka maeneo mbalimbali Jijini Tanga na kuishia hapo huku yakishirikisha wakimbiaji katika makundi matatu ya Kilomita 21,10 na 5 za kujifurahisha.
USAJILI WA TANGA CITY MARATHON 2024 KUFANYIKA KWA MTANDAO "ONLINE"
Tuesday, 6 August 2024
MAONYESHO YA NANENANE 2024,YAIBUA WAKULIMA KUTOA CHANGAMOTO ZAO KWENYE SEKTA YA KILIMO,,
Pichani ni mkulima wilayani Muheza akiwa kwenye maonyesho ya nanenane 2024.
NA SOPHIA WAKATI,MOROGORO