MADIWANI KOROGWE VIJIJINI WAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA BILLION 42 -2025-26
NA SOPHIA WAKATI, KOROGWE
Pichani ni baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Korogwe vijijini wakifuatilia kuwasilishwa kwa bajeti ya 2025-2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe limeadhimia kutumia kiasi cha Shilingi 42,185,006,702.00 katika bajeti yake ya Mwaka wa fedha 2025/2026.
Pichani ni Mchumi wa halmashauri ya Korogwe vijijini,Pantaleo Nkangara akipokea maoni ya madiwani mara baada kuwasilisha bajeti kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Wakili Goodluck Mwangomango kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano jengo jipya la utawala lililopo kata ya Makuyuni wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Bajeti hiyo imepitishwa katika kikao cha Baraza la madiwani kwenye taarifa ambayo iliwasilishwa na Mchumi wa halmashauri ya Korogwe vijijini,Pantaleo Nkangara ambaye kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Wakili Goodluck Mwangomango.
Katika makisio hayo ya bajeti ya 2025/2026 ruzuku ya matumizi mingineyo ni shilingi 1,410,823,000 na ruzuku ya Mishahara ni shilingi 29,174,460,000 huku jumla ndogo ikitajwa kuwa kiasi cha Shilingi 30,585,283,000.
Kwenye miradi ya Serikali kuu ,ufuatiliaji na tathimini miradi ya maendeleo Shilingi 70,000,000.00, mfupi wa jimbo Shilingi 81,302,000.00 huku ujenzi na ukarabati hospitali ya wilaya ukiwa Shilingi 276,000,000.00.
Aidha ununuzi wa Vifaa kwa ajili ya hospitali ya wilaya ni Shilingi 300,000,000.00, ununuzi Vifaa vya zahanati Shilingi 100,000,000.00 na ukamilishaji maboma ya Mabweni Sekondari kiasi cha Shilingi 40,000,000.00.
Pia kwenye ukamilishaji miradi viporo mabwalo shule za Sekondari zipo Shilingi 173,000,000.00, ununuzi wa vifaa kwa ajili ya zahanati Shilingi 100,000,000.00, mtihani wa upimaji darasa la nne Shilingi 491,577,000.00 na mtihani wa taifa wa kuhitimu darasa la Saba Shilingi 541,220,000.00.
Vile vile kwenye mtihani wa taifa kuhitimu kidato cha Sita kuna shilingi 54,629,000.00,mtihani wa taifa wa kuhitimu kidato cha nne shilingi 381,011,000.00, mtihani wa upimaji kidato cha pili shilingi 237,859,000.00, elimu bila ada msingi shilingi 815,193,718.00 na elimu bila ada Sekondari shilingi 930,462,984.00 hivyo kufanya jumla ndogo kuwa Shilingi 4,402,355,702.
Kwa upande wa miradi ya wafadhili sustainable rural water supply and sanitation (SRWSS) education - world bank ni shilingi 217,902,000.00 na sustainable rural water supply and sanitation (SRWSS) MoF shilingi 544,753,000.000.
Fedha nyingine ni shilingi 555,388,000.00 za mfuko wa pamoja wa afya (HSBF), Quality education - BHC UK Shilingi 30,000,000.00, kufua kikuu/ukoma 7,727,000.00 na malaria - global fund MSQI shilingi 1,414,000.00.
Shilingi 174,000,000.00 ni health system strengthening of immunization service GAVI, boost primary student learning shilingi 1,020,758,000.00, Secondary education quality improvement project (SEQUIP) shilingi 624,287,000.00 na Tassaf PSSN II shilingi 1,277,500,000.00.
Kwa mujibu wa Mchumi huyo Nkangara alisema jumla ndogo ya fedha hizo ni shilingi 4,453,729,000.00 na kwenye jumla kuu ya miradi shilingi 8,856,084,702.00 huku jumla kuu ya bajeti hiyo ikiwa kiasi cha shilingi 42,185,006,702.00.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Korogwe Kallaghe Sadick Yusuph amewataka watumishi kusimamia vizuri bajeti hiyo ili iweze kuleta tija..
Mwisho.
Pichani ni Mchumi wa halmashauri ya Korogwe vijijini,Pantaleo Nkangara akipokea maoni ya madiwani mara baada kuwasilisha bajeti kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Wakili Goodluck Mwangomango kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano jengo jipya la utawala lililopo kata ya Makuyuni wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Pichani ni baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Korogwe vijijini wakifuatilia kuwasilishwa kwa bajeti ya 2025-2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Pichani ni wadau mbalimbali wa halmashauri ya Korogwe vijijini wakiwa kwenyekikao cha kuwasilisha bajeti ya 2025-26.
No comments:
Post a Comment