KAMPUNI YA RENATA NI SULUHISHO LA MAGONJWA SUGU TANZANIA,,
Pichani ni Dk.Twaha Hassan kutoka kampuni ya RENATA , akielezea umuhimu wa tiba lishe zinazozalishwa kwa mimea asilia na matunda pamoja na Kahawa iliyo msaada mkubwa katika kutibu magonjwa sugu.
NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
WANANCHI wametakiwa kuzitumia bidhaa zitokanazo na tiba lishe hatua ambayo itawasaidia katika kulinda afya za binadamu dhidi ya magonjwa sugu ukiwa ni pamoja na kupata fursa ya kujikwamua kiuchumi.
Rai hiyo imetolewa na mtaalam wa tiba lishe wa Kampuni ya RENATA Health World Tanzania, Dk. Joanness Petro almaarufu JJ, alipokuwa akizungumza na baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya wilayani Korogwe.
Katika semina hiyo ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa White House uliopo Korogwe Mjini, shughuli ambayo iliwahusisha Wananchi wa kada mbalimbali wakiwemo Viongozi wa kidini.
Dk. JJ kutoka kampuni ya RENATA Health World Tanzania alisema, wanahusika na uuzaji bidhaa za tiba lishe kwa lengo la kuwasaidia Wananchi kuimarisha afya zao huku wakiongeza pato.
Aidha,wamechukua jukumu la kutoa elimu kwa wananchi hao ili kuwawezesha kunufaika na uwepo wa kampuni ya RENATA inayohusika na bidhaa za tiba lishe ili kuwawezesha kulinda afya na pia tiba kuongeza kipato chao.
Aidha,aliongeza kusema kuwa RENATA imekuwa ikihusika na bidhaa za tiba lishe zenye uwezo mkubwa katika kuimarisha afya kwa kuimarisha na kurutubisha seli za mwili zilizochakaa.
Miongoni mwa bidhaa walizonazo ni zile zinazotibu magonjwa mbalimbali yaliyo Sugu na pia tiba lishe hiyo inasaidia kufanya ngozi ya mwili kuwa nyororo na kuongeza uimara wa mwili kumfanya mtu mwenye umri mkubwa kuonekana kama kijana.
Baadhi ya magonjwa yanayoweza kutibiwa kupitia tiba lishe kutoka kampuni ya RENATA ni sukari,mifupa,meno,macho,vidonda vya tumbo,saratani aina zote na hata changamoto zinazowakumba wakina mama kimaumbile.
"Tunazo tiba lishe zinazoshughulika na seli za mwili na zimekuwa na matokeo mazuri zinatibu magonjwa sugu, ni virutubisho vinavyokwenda kuhuisha seli zilizokufa jambo ambapo huwa chanzo cha maradhi mbalimbali"alisema Dk. JJ.
Kwa upande wake mtaalam mwingine wa RENATA Dk.Twaha Hassan, alisema kuwa tiba lishe wanazohusika nazo zimezalishwa kwa mimea asilia na matunda huku alitanabaisha kuwa pia wanayo Kahawa iliyo msaada mkubwa katika kutibu tatizo la moyo, nguvu za kiume, kike na kusafisha mishipa ya damu.
Kuhusu namna ambavyo anayetumia tiba lishe kutoka kampuni ya RENATA anaweza kunufaika kwa kuongeza kipato chake,Dk. Hassan alisema huku akiwataka wananchi wanaosumbuliwa na magonjwa sugu kuondoa tatizo hilo.
"Mtu akijisajili kwenye mfumo wetu tutampatia utaratibu ambao na yeye anaweza kuwaelimisha watu wengine, watakapojiunga wengine kupitia yeye hapo huanza kunufaika kwa kupata fedha"alisema Dk. Hassan.
Kwa mujibu wa Dk.Hassan yapo madaraja tofauti ambayo mteja anaweza kujiunga kwenye mfumo wao ambao hutoa viwango tofauti vya fedha za papo kwa hapo lengo likiwa kuwakwamua Wananchi katika hali duni kimaisha.
Mmoja wa washiriki wa Semina hiyo, Ahmad Mwinyimsanga alielezea kuridhishwa kwake juu ya elimu waliyoipata huku akiahidi kuwa Balozi mzuri wa tiba lishe kupitia kampuni ya RENATA.
"Leo nimejifunza mengi mazuri, RENATA wamekuja kuboresha afya zetu, Mimi nawaona ni wakombozi ingawa unaweza kuona wanauza dawa ila lengo lao kuu ni kutukinga dhidi ya maradhi na hata kutibu, hapo hapo ukijiunga nao unapata 'commission' na kuongeza kipato"alisema Ahmad Mwinyimsanga Mkazi wa Kwamsisi wilayani Korogwe.
Kampuni ya RENATA Health World Tanzania imeweka Ofisi zake Jijini Dar es Salaam, Kibaha na Zanzibar, hivi sasa imekusudia kufungua matawi mengine Mkoani Tanga kwa kuanzia na wilaya ya Korogwe.
Mwisho.

Picha ni Dk. Joanness Petro almaarufu JJ, kutoka kampuni ya RENATA Health World Tanzania, akionyesha bidhaa zinazotolewa na kampuni hiyo,kwenye semina iliyofanyika wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.
Picha ni miongoni mwa wananchi walioshiriki semina iliyoandaliwa na kampuni ya RENATA.
No comments:
Post a Comment