Thursday, 27 February 2025

RUWASA -KUNUFAISHA WANANCHI ZAIDI YA ELFU 28 KUPATA MAJI SAFI KOROGWE,,, 
Picha ni Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Korogwe, Injinia Muharami Mohamedi ameyasema hayo juzi wakati akiwasilisha taarifa yake kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Korogwe vijijini.

NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
KATIKA kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Wilayani Korogwe umefanikiwa kukamilisha miradi Sita ya maji iliyogharimu Shilingi 2,045,399,927 inayohudumia watu 26,388 kwenye vijiji vipatavyo 15.

Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya Korogwe, Injinia Muharami Mohamedi ameyasema hayo juzi wakati akiwasilisha taarifa yake kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Korogwe vijijini.

Katika taarifa yake hiyo ameitaja miradi hiyo kuwa ni ule wa Lwengera uliyotekelezwa kwa gharama ya Shilingi 761,475,594 na mradi wa maji ya mtiririko Mlembule uliyotumia Sh. 987,384,000.

Pia kuna mradi wa kuchimba visima virefu sita katika vijiji vya Kwetonge, Mswaha,Mafuleta,Changalikwa,Kulasi na Magamba Kwalukonge uliyogharimu Shilingi 203,995,500.

Ukarabati wa mradi wa maji Mkwakwani shilingi 30,000,000,ujenzi wa tenki la maji lita 50,000 katika kijiji cha Mgambo shilingi 22,544,833 na ujenzi wa tenki la maji lita 75,0000 kwenye kijiji cha Kijango shilingi 40,000,000.

Kwa upande wa miradi iliyokamilishwa na RUWASA katika mwaka wa fedha 2024/2025 wilayani Korogwe imekamilisha miradi yenye thamani ya Shilingi 1,374,567,035.

Miradi hiyo inahudumia Wananchi 16,267 waliopo katika vijiji nane (8) na miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa maji Magila Gereza uliyogharimu Shilingi 775,743,809 na ukarabati na upanuzi mradi wa maji Sisi kwa sisi uliyogharimu kiasi cha shilingi 327,166,478.

Kwa mujibu wa Injinia Muharami pia umo mradi wa maji Kwedege uliyogharimu shilingi 80,000,000, ukarabati na upanuzi mradi wa maji Makole, ukarabati na upanuzi mradi wa maji Kijungumoto na ukarabati mradi wa maji Kwagunda na hivyo kufanya jumla ya Shilingi 1,374,567,035.
Mwisho.





Pichani ni miongoni mwa madiwani wa braza la madiwani halmashauri ya korogwe vijijini wakishauri mara baada ya  kuwasilishwa taarifa ya miradi ya RUWASA.

Picha ambaye amesimama ni mwenyekiti wa halmashauri ya Korogwe vijijini,Sadick Kalaghe akipongeza RUWASA.

No comments:

Post a Comment