Sunday, 19 November 2017

ZOEZI LA BALOZI WA KUWAIT NCHI TANZANIA,JAASIM KUKABIDHI KISIMA NA VIFAA KWA AJILI YA MAMA NA MTOTO ILIKUWA HIVI,,

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
SERIKALI ya Kuwait imesema itaendelea kumuunga mkono Rais wa Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli kwa adhima yake ya elimu bure kwa kusaidia sekta ya elimu na afya hapa nchini.

Thursday, 16 November 2017

MSEMAJI WA TIMU YA MPIRA WA MIGUU WANAWAKE MKOANI TANGA FAIR PLAY QUEENS AMESEMA HANA SHAKA NA KIKOSI CHAKE,,

 Pichani ni msemaji wa timu ya mpira wa miguu mkoa wa Tanga FAIR PLAY QUEENS ,Sophia Wakati juzi akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) juu ya maandalizi ya kujiwinda na ligi ya taifa ya wanawake kwenye uwanja wa soka Disuza inapo endelea na mazoezi ya kila siku.

Ambapo amesema kocha wa timu hiyo,Kuha Idd amezifanyia kazi safu zote muhimu ikiwemo za ufungaji na ushambuliaji lengo kufanya vizuri na kwenye mashindano hayo.
Pichani ni kikosi cha  FAIR PLAY QUEENSkikiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya mazoezi uwanja wa Disuza jijini Tanga..

 Pichani ni kipa namba moja wa timu ya FAIR PLAY QUEENS
Pichani ni kapteni wa timu hiyo,Asha Shabani maarufu Kadosho

Tuesday, 14 November 2017

IFAHAMU RUSHA ROHO RESTAURANT YENYE MAPISHI ASILI YA KISWAHILI ILIYOPO JIJINI TANGA,, Pichani mkono wa kushoto mwanamke ni meneja wa RUSHA ROHO Restaurant,Hythum Yusuph mgahawa uliopo jijini Tanga jinsi unavyo ongoza kwa vyakula mchanganyiko mapishi ya kiswahili asilia,akiwa na kiongozi msaidizi wakitumia kutoa risiti kwa kutumia mashine.,
 Pichani ni meneja wa RUSHA ROHO Restaurant,Hythum Yusuph akionyesha vyakula mbalimbali,
Pichani ni wahudumu wakiwa ndani ya RUSHA ROHO Restaurant wakiwa kwenye maeneo mbalimbali.

Vyakula vilivyopo ni Chai ya rangi,chai ya maziwa,kahawa,kahawa nyeusi,maziwa fresh, Juis pashen,juis ovakado,juis ukwaju,soda coca,soda pepsi,heltho,maji, Chapati,vitumbua,maandazi,donart,calmati,mayai,bajia za kunde,kachori,mihogo,viazi vitamu,magimbi,eggechop,kababu,caltess,spaceng roll,sambusa.

Wali maini,wali nyama,wali kuku,wali samaki,wali mbogamboga,,pilau nyama,pilau maini,pilau kuku,pilau samaki,ndizi kuku,ndizi maini,ndizi samaki,

Supu kuku,supu mbuzi,kuku rosti,mbuzi rosti,samaki rosti,rosti ngombe,samaki wa kukaanga,samaki wa kuchoma,kuku wa kukaanga,kuku sekelo,mishikaki,rosti maini,chips kuku,chips samaki,chips plons,.

Sunday, 12 November 2017

UZINDUZI WA KAMPENI UCHAGUZI MDOGO KITI CHA UDIWANI KATA YA MAJENGO WILAYANI KOROGWE CHAMA CHA MAPINDUZI ILIKUWA HIVI,,,

 Pichani ni mapokezi ya mbunge wa jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde juzi katika uzinduzi kampeni za Udiwani za chama cha mapinduzi CCM katika uchaguzi mdogo utakaofanyika hapo Novemba 26 mwaka huu.
 Pichani katikati ambaye ameshika kofoa ni wanachama wa chama cha mapinduzi wakimpokea mgombea udiwani wa kata hiyo ya Majengo Mustapher Sadick Shengwatu.
 M
NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
CHAMA cha mapinduzi CCM kimezindua kampeni zake za Udiwani katika uchaguzi mdogo utakaofanyika hapo Novemba 26 mwaka huu ambapo mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde aliwataka wananchi wa kata ya Majengo Korogwe mjini kumchagua mgombea wa CCM  ili kuweza kuharakisha maendeleo yao.

Lusinde maarufu kwa jina la ‘Kibajaji’ aliyasema hayo juzi katika viwanja vya Sabasaba kwenye ufunguzi wa kampeni za CCM ambapo aliwaeleza wananchi kuwa amekuja Korogwe kwa ajili ya kuwasihi kumchagua mwanaCCM ambaye anaamini ndiye mgombea sahihi atakayeshirikiana na Serikali iliyopo madarakani.

Katika hotuba yake mbunge huyo wa jimbo la Mtera,alisema maendeleo ya kata ya Majengo yataletwa na wananchi wenyewe kwa kushirikiana na serikali iliyopo madarakani na kamwe jamii haipaswi kudanganyika kuchagua mgombea kutoka vyama vingine vyenye tabia ya kugomea kazi  za maendeleo.

“Ndugu zangu mimi nimekuja kuwaasa,mchagueni mgombea anayetoka CCM Mustapher Shengwatu ambapo mtaharakisha maendeleo kwa vile anapo mahali kwa kuwasilisha kero zenu ila hawa ambao wamekuwa na tabia ya kusema kuwa mkinichagua hamtashiriki kazi fulani achaneni nao”alisema mbunge Lusinde.

Mbunge huyo aliendelea kusema kuwa kuchaguliwa kwa mgombea udiwani huyo Shengwatu kutatoa fursa kwake na chama cha mapinduzi kuisimamia serikali kikamilifu hatua ambayo itawezesha utekelezwaji wa miradi mingi ya maendeleo na hivyo kata ya Majengo kusonga mbele kwa haraka.

Awali akizungumza kabla ya Lusinde aliyekuwa mgeni rasmi ufunguzi huo wa kampeni,mbunge wa jimbo la Korogwe mjini Mary Pius Chatanda alisema,wananchi hawapaswi kudanganyika na kauli za wapizani kwamba CCM haijafanya chochote huku wakitumia mitandao ya jamii kueneza propaganda hizo.

Chatanda alisema kwamba uongozi wake kwa kushirikiana na chama cha mapinduzi kupitia serikali iliyopo madarakani umefanikiwa kufanya mambo kadhaa ambayo yataleta ukombozi mkubwa kwa wananchi mjini Korogwe ambapo alisema kunajengwa mradi mkubwa wa maji kuondosha kero iliopo.

Chatanda alisema kwamba mradi huo unatekelezwa katika eneo la Mtonga na unatarajiwa kukamilika kipindi kifupi kijacho na pindi utakapokamilika unatarajiwa kuondoa kero ya maji huku idadi kubwa ya wananchi wa Korogwe wakitarajiwa kunufaika na uwepo wa mradi huo utakaokuwa wa kihistoria.

Mbali na kutaja mradi wa maji alisema kuwa jitihada zinaendelea kuboresha miundombinu ya barabara sanjari na vituo vya afya lengo likiwa kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma bora ambapo aliwasisistiza wananchi wa kata ya Majengo kumchagua mgombea wa CCM ili kuharakisha maendeleo.

Naye mgombea udiwani wa kata hiyo ya Majengo Mustapher Sadick Shengwatu alisema kwamba iwapo atapata fursa ya kuchaguliwa kuwaongoza wananchi wa Majengo atahakikisha kwamba miradi yote iliyoanza kutekelezw3a inamalizika na mipya inaibuliwa kwa lengo la kutatua kero zinazoikabili jamii.

Shengwatu alisema kwamba,akichaguliwa atashirikiana vyema na wananchi bila kujali itikadi za namna yeyote ile huku akitanabaisha kuwa ataimarisha mshikamano na viongozi waliopo,wananchi katika kuisogeza mbele kata ya Mjengo huku akiahidi wanawake na vijana kuangaliwa kwa namna yake.
Mwisho.
Pichani ni mgombea kiti cha udiwani wa kata hiyo ya Majengo Mustapher Sadick Shengwatu juzi mara ya baada ya mkutano akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani lengo la kuwania nafasi hiyo.

Thursday, 2 November 2017

KAMANDA TANGA,WAKULYAMBA AKIZUNGUMZIA JINSI WALIVYOFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA WAFANYABIASHARA WAWILI NYUMBA YA KULALA WAGENI JIJINI HAPO,,

Pichani ni kamanda wa polisi mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba akiwaeleza waandishi wa habari (hawako pichani) jinsi walivyofanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya wafanyabiashara wawili walikutwa wamekufa nyumba ya kulala wageni Bomai Inn jijini Tanga.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
JESHI la Polisi Mkoani Tanga.linamshikilia mfanyabiashara, Ismail Yahaya Muhaji (41) mkazi wa Bulwa Amani wilayani Muheza,Dar e salaam na Tunduma mkoani Songwe akituhumiwa kuhusika kwa Mauaji ya watu wawili.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakuyamba amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo akisema, kuwa mtuhumiwa tayari yuko mikononi mwa Polisi kwa mahojiano ili kujua kiini cha mauaji hayo. 

Alisema, mtuhumiwa ambaye ana makazi yake huko Bulwa Amani Muheza, Dar es Salaam na Tunduma Mkoani Songwe anahusishwa na mauaji ya Septemba 25 mwaka huu wa 2017 jijini hapo.

Kamanda,Wakulymba alisema kwamba katika kipindi hicho kulitokea mauaji ya kutatanisha kwenye nyumba ya kulala wageni ya Bomai Inn iliyopo Jijini Tanga. 

Kutokana na tukio hilo jeshi la Polisi liliendelea na uchunguzi hadi kufanikiwa kumnasa mtuhumiwa huyo mkoani Mwanza ambaye anaendelea kushikiliwa kwa uchunguzi. 

Aidha Kamanda Wakulyamba alitanabaisha kwamba katika mahojiano mtuhumiwa amekiri kutenda tukio hilo la kusikitisha kwa Jamaa zake hao waliofariki dunia. 

Alisema mtuhumiwa (Muhaji) amekiri kuwapa kilevi kikali (Valium)  marehemu hao wawili kwa kutumiwa mwanya wa ukaribu nao katika biashara walizofanya. 

Hata hivyo alisema, mtuhumiwa huyo tayari ameshafikishwa Mahakamani huku upelelezi ikiendelea kujua kisa na chanzo cha mauaji hayo ya kikatili. 

Kamanda huyo wa jeshi la Polisi Mkoani Tanga alisema jeshi la Polisi litaendelea kuwakamata wahalifu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili haki kuweza kutendeka na amani kuimarika.
Mwisho.

Sunday, 22 October 2017

TAASISI YA WICOF YA MKOANI MOROGORO IKIWA KATIKA ZOEZI LA KUGAWA MISAADA MKOANI TANGA,,,,

Pichani mkono wa kushoto mwanamke ambaye amevaa baibui jeusi ni mwanachama wa  taasisi ya WICOF,Zainab Bendera akifuatiwa na Mohamedi Dhahabu wakikakabidhidhi misaada kwa watumishi wa hospital ya rufaa Bombo mkoani Tanga,
 Pichani wa pili mkono wa kushoto ni mwenyekiti wa taasisi ya WICOF, Mwajabu Dhahabu mwanachama wake Zainab Bendera juzi katika ziara ya kugawa misaada husika ilisambazwa hospitali yarufaa Bombo Jijini Tanga na Zahanati ya Potwe iliyopo wilayani Muheza katika mkoani hapo.
Pichani ambaye amevaa baibui ni mwanachama wa WICOF,Zainab Bendera juzi katika zoezi la kugawa misaada husika ilisambazwa hospitali yarufaa Bombo Jijini Tanga na Zahanati ya Potwe iliyopo wilayani Muheza katika mkoani hapo.
Ugawaji wa madawa Zahanati ya Potwe iliyopo wilayani Muheza katika mkoani Tanga ilikuwa hivi.
Picha ni wananchi mara baada kukabidhiwa msaada wa madawa kwa ajili ya Zahanati ya Potwe iliyopo wilayani Muheza katika mkoani Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja.


 Picha ni vifaa mbalimbali vya msaada vilivyotolewa na taasisi ya WICOF yenye maskani yake mkoani Morogoro,kwa ajili ya kuhifadhia maziwa kwa ajili ya watoto.


NA SOPHIA WAKATI, TANGA
TAASISI ya Wanawake Women Infants and Community Outreach Foundation (WICOF) imetoa msaada wenye thamani ya zaidi sh 3.1 million kusaidia Wagonjwa kwenye baadhi ya hospitali na Zahanati katika mkoa wa Tanga. 

Mwenyekiti wa taasisi hiyo Mwajabu Dhahabu amesema juzi kuwa misaada husika ilisambazwa hospitali yarufaa Bombo Jijini Tanga na Zahanati ya Potwe iliyopo wilayani Muheza katika mkoani hapo. 

Dhahabu ametaja misaada hiyo kuwa ni shuka 36 kwenye Wodi ya watoto Bombo hospitali, deep freezer la kuhifadhia maziwa ya watoto pamoja na dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba. 

Alifafanua kuwa maeneo yote hayo misaada waliyoitoa imegharimu zaidi ya sh 3.1 milioni ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kusaidia huduma za afya kwa jamii. 

Naye mwanachama wa asasi hiyo ya WICOF yenye makao yake makuu mjini Morogoro, Zainab Bendera alisema wamejipanga kusaidia huduma za jamii hasa sekta ya afya ili kuokoa nguvu kazi. 

Alisema, tayari wamechukua michoro inayoihusu Zahanati ya Potwe ili kuangalia namna watakavyoweza kushiriki kuifanyia ukarabati na hivyo kutoa huduma zenye ubora na viwango stahiki. 

"Tukiwa sehemu ya watanzania tumeguswa kuisaidia jamii yetu, tunaunga mkono jitihada za Serikali yetu kupitia kauli mbiu ya hapa kazi tu "alisema Bendera. 

Aidha Bendera ametoa wito kwa asasi nyingine wakiwemo mtu mmoja mmoja wenye uwezo kujitokeza kusaidia sekta ya afya ili kuweza kuimarika na kuleta tija kwa watanzania walio wengi.
Mwisho. 

CCM MKOANI TANGA YASISITIZA VIONGOZI NA WANACHAMA KULETA MABADILIKO NDANI YA CHAMA,,,

Pichani ni katibu wa CCM mkoa wa Tanga,Allan Kingazi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake akisisitiza viongozi na wananchama kuleta mabadiliko ndani ya CCM.

NA SOPHIA WAKATI, TANGA
KATIBU wa chama cha mapinduzi CCM mkoani Tanga,Allan Kingazi amesema uchaguzi kujaza nafasi mbalimbali za uongozi umekwisha akiwataka wanachama kushirikiana na viongozi wao kuiletea mabadiliko CCM. 

Kingazi ameyasema hayo juzi akisema baada ya uchaguzi ndani ya chama chao kumalizika kinachohitajika ni mabadiliko huku akiwasihi viongozi kushirikiana na wanachama kuimarisha ngome za chama cha mapinduzi CCM. 

"Tunashukuru uchaguzi umemalizika vizuri kilichobaki ni kujenga Chama, baada ya wanachama kuwaweka viongozi madarakani washirikiane nao kuimarisha ngome ili kukiletea chama mabadiliko makubwa"alisema Kingazi. 

Wakati,Kingazi akiyasema hayo,mwenyekiti wa CCM wilayani Tanga,Meja mstaafu Hamisi Mkoba amewataka viongozi wenzake kuanzia ngazi ya matawi na mashina kuhakikisha kipaumbele chao kuwa kurejesha hadhi ya CCM jijini hapo. 

Alisema, viongozi waliochaguliwa wanapaswa kutambua kuwa chama chao kimejijengea heshima kubwa miongoni mwa jamii hivyo wana kila sababu kukitukikia kwa uadilifu ili kuendelea kudumisha heshima iliyokuwa nayo CCM. 

Pia,amewataka wana CCM kuwa na uchungu na chama chao katika kukitetea huku akiwataka kuunganisha nguvu zao kurejesha kata 13 zilizokwenda upinzani. 

"Kiukweli nitoe shukrani kwa kuchaguliwa sasa naomba ushirikiano twendeni kwenye maeneo yetu kupigania maslahi ya CCM, kila mmoja wetu awe na uchungu na CCM "alisema Meja mstaafu Mkoba. 

Mwenyekiti huyo wa CCM wilayani Tanga,alisema kwamba kulingana na heshima kubwa ya chama hivyo miongoni mwa jamii kuna uwezekano mkubwa kurejesha kata zilizopotea akisisitiza uwepo mshikamano madhubuti. 

Mkoba amesema, kupitia mshikamano wao ana matumaini makubwa kwamba CCM itaendelea kuheshimika miongoni mwa jamii huku chama hicho kikiendelea kupata ridhaa ya kuwatumikia watanzania.
Mwisho.