Saturday 5 August 2023

SHABIKI WA SIMBA PONGWE ,AFUNGUKA NAIPENDA SIMBA KULIKO MKE WANGU,,



Pichani ni shabiki akiri kuipenda Timu ya Simba kuliko Mke wake wa ndoa.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

MWANACHAMA na mpenzi wa Klabu ya Simba tawi la Pongwe Best, Ally Kileo amesema kwamba, hata kikosi hicho ipoteze michezo hatetereki kuihama timu hiyo.

Kileo mwenye miaka  (41) amesema kwamba anaipenda zaidi Klabu ya Simba kuliko Mke wake kwa vile katika maisha yake alianza kuwapenda zaidi wana Msimbazi kulio ndoa.

“Kabla ya kuwa na Mke nilipenda Zaidi Simba, sikupta kuwa na mpenzi isipokuwa Timu ya Simba hivyo kati ya Simba na Mke naipebda zaisi Simba”alisema Kileo.

Kileo aliasema hayo jana kwenye mahojiano maalum huko Pongwe nje kidogo ya Jiji la Tanga eneo ambalo wana Simba walishiriki shughuli za jamii kufanya usafi kituo cha afya Pongwe na kugawa zawadi kwa wagonjwa.

Katika kituo hicho cha afya Pongwe wanachama na wapenzi wa Simba waligawa Sabuni za Unga na miche kwa wagonjwa waliolazwa ikiwa ni sehemu ya kuwafariji.

Mbali na kujitolea kwenye kituo hicho cha afya lakini pia wana Simba hao walikwenda eneo la Umba kuwafariji wazee waliopo kwenye Kambi maalum ya wakoma.

Mwisho.



Kuelekea Simba Day: Pongwe Best kuwafariji kituo cha Wakoma.

Washiriki Usafi mazingira, kufariji na kugawa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa Kituo cha Afya Pongwe.


KATIKA kuelekea Simba Day Wapenzi na Wanachama wa Klabu ya Simba kutoka tawi la Pongwe Best lililopo nje kidogo ya Jiji la Tanga, wametoa misaada ya Kijamii kwa  kutoa zawadi mbalimbali ikiwa seemu ya kufariji wagonjwa waliolazwa kwenye Kituo cha afya Pongwe.

Misaada hiyo ni pamoja na Sabuni za unga na vipande huku wakitumia fursa hiyo kufanya usafi kwenye mazingira ya kituo hicho cha afya ambapo wana Simba hao wametumia siku ya jana kushirikiana na jamii.

Mbali na kufanya shughuli hiyo katika kituo cha afya Pongwe lkini pia wapenzi hao wa timu ya Simba wwaliwatembelea wazee wanaoishi kwenye Kambi ya watu wanaougua ugonjwa wa ukoma ya Umba.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Simba tawi la Pongwe Best, Patrice Mgendi alisema kwamba; “Tumeamua kutumia siku hii kuelekea Simba Day kuwafariji wagonjwa na wenye mahitaji maalum”alisema.

Asha Salmada ambaye ni mganga mfawidhi wa kituo cha afya Pongwe alisema kwamba, wamefarijika kuona wana Simba hao wamechukua hatua kuona umuhimu wa kuisaidia jamii jambo ambalo husaidia kuwapatia faraja.

“Kwa niaba ya Kituo, tumejisikia vizuri wana Simba kufanya usafi na kuwapa zawadi wagonjwa, tunaomba timu nyingine zingeiga mfano huu”alisema Salmada.

Wana Simba wengine walioshiriki zoezi hilo la kutoa zawadi kwa wagonjwa walisema kwamba, wamedhamiria utaratibu huo wa kuchangamana na jamii kuwa endelevu kwa kuwa wana wajibu kufanya hivyo kama watanzania.

Pamoja na hayo Salmada alitoa rai kwa wana Simba na wanamichezo wengine kuwa tayari kushiriki mazoezi mengine akitolea mfano lile la kuchangia damu sanjari na kutembelea kituo cha afya Pongwe kupima afya zao.

Mwisho.



 

No comments:

Post a Comment