Pichani ni miongoni mwa wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba Pongwe mkoani Tanga Kuelekea
Simba Day:wakifanya usafi wa mazingira kituo cha afya Pongwe na kugawa zawadi kwa wagonjwa wodi mbalimbali.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
KATIKA
kuelekea Simba Day Wapenzi na Wanachama wa Klabu ya Simba kutoka tawi la Pongwe
Best lililopo nje kidogo ya Jiji la Tanga, wametoa misaada ya Kijamii kwa kutoa zawadi mbalimbali ikiwa seemu ya
kufariji wagonjwa waliolazwa kwenye Kituo cha afya Pongwe.
Misaada hiyo
ni pamoja na Sabuni za unga na vipande huku wakitumia fursa hiyo kufanya usafi
kwenye mazingira ya kituo hicho cha afya ambapo wana Simba hao wametumia siku
ya jana kushirikiana na jamii.
Mbali na
kufanya shughuli hiyo katika kituo cha afya Pongwe lkini pia wapenzi hao wa
timu ya Simba wwaliwatembelea wazee wanaoishi kwenye Kambi ya watu wanaougua ugonjwa
wa ukoma ya Umba.
Akizungumza
kwa niaba ya Mwenyekiti wa Simba tawi la Pongwe Best, Patrice Mgendi alisema
kwamba; “Tumeamua kutumia siku hii kuelekea Simba Day kuwafariji wagonjwa na
wenye mahitaji maalum”alisema.
Asha Salmada
ambaye ni mganga mfawidhi wa kituo cha afya Pongwe alisema kwamba, wamefarijika
kuona wana Simba hao wamechukua hatua kuona umuhimu wa kuisaidia jamii jambo
ambalo husaidia kuwapatia faraja.
“Kwa niaba
ya Kituo, tumejisikia vizuri wana Simba kufanya usafi na kuwapa zawadi wagonjwa,
tunaomba timu nyingine zingeiga mfano huu”alisema Salmada.
Wana Simba
wengine walioshiriki zoezi hilo la kutoa zawadi kwa wagonjwa walisema kwamba,
wamedhamiria utaratibu huo wa kuchangamana na jamii kuwa endelevu kwa kuwa wana
wajibu kufanya hivyo kama watanzania.
Pamoja na
hayo Salmada alitoa rai kwa wana Simba na wanamichezo wengine kuwa tayari
kushiriki mazoezi mengine akitolea mfano lile la kuchangia damu sanjari na
kutembelea kituo cha afya Pongwe kupima afya zao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment