Tuesday 8 August 2023

BENK YA NMB MADARAKA TANGA YAGAWA JEZI KWA AJILI YA WASHINDI MASHINDANO YA ULINZI CUP 2023,,,


Pchani wa pili mkono wa kushoto ni Meneja wa benk ya NMB Elizabeth Chawingaakimkabizi jezi Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe ofisini kwake akiwa ameambatana na maafisa mbalimbali wa benk hiyo.

    NA SOPHIA WAKATI,TANGA

Mara baada ya kukabidhi hizo,Elizabeth amesema benk imegushwa na utendaji kazi wa jeshi la polisi kupambana na uhalifu kwa kutumia mashindano ya Ulinzi Cup kutoa elimu kwa vijana kujiepusha na kuwafichua wanaojihusisha na vitendo viovu. 

Polisi Jamii yaibuka Kidedea Ulinzi Cup.

TIMU ya Soka Polisi Jamii FC yenye maskani yake FFU Majani mapana Jijini Tanga imefanikiwa kutoka kifua mbele baada ya kuifunga Tanesco kwa mabao 4 – 1 katika mchezo wa Ligi ya kuwania Kombo la Ulinzi uliofanyika Uwanja wa shule ya msingi Kombezi.

Polisi jamii ilikuwa ya kwanza kufunga magoli yake kupitia vinara wa timu hiyo, Khalifa Hussein aliyeifungia mabao mawili dakika ya 11 na 47,huku Shauri Juma goli moja dakika ya 48, Salimu Mazimu goli moja dakika 78 mpambano ambao ulikuwa na burudani ya kuvutia.

Goli la kufutia machozi la Tanesco Tanga lilipachikwa kimiani na Mwedi aliyewahadaa walizni wa Police Jamii na kuachia mkwaju mkali uliokwenda moja kwa moja wavuni na kumsinda mlinda mlango Endrew Solnaj.

Kwa matokeo hayo Police Jamii wamefanikiwa kuwa washindi watatu kwenye ligi hiyo iliyokuwa ikishirikisha timu 20 huku ikiendeshwa kwa mtindo wa mtoano.

Lengo la  ligi hiyo ilikuwa ni Jeshi la Polisi kushirikiana na Jamii hususani Vijana kupitia sekta ya michezo kutumia mpira wa miguu kupambana na vitendo vya uhalifu.

Kwa kutumia jukwaa hilo Jeshi la Polisi limekuwa likitoa elimu kwa Jamii kupambana na uhalifu kwa kutoa taarifa za kuwafichua wahalifu ili sharia kuchukua mkondo wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe katika mazungumzo yake na Wanahabari alisema juzi kuwa,fainali za ligi hiyo zitafanyika baada ya kumalizika kwa mashindano ya ngao ya hisani Jijini Tanga.

Mwisho.


Pichani mkono wa kulia ni miongoni mwa maafisa wa benk ya NMB Madaraka mkoani Tanga akimpongeza Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapo kushoto,Henry Mwaibambe kwa kutoa elimu kupitia sekta ya michezo.






















 

No comments:

Post a Comment