Tuesday 8 August 2023

TFF YAFUNGUKA LENGO LA KUFANYIKA MASHINDANO YA NGAO YA HISANI TANGA ,,,,,



Pichani ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano,Khalid Abdallah akiwa katika uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga akizungumza na waandishi wa habari akiwata mashabiki na wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano ya Ngao ya Hisani. 

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
WAKATI mashindano ya ngao ya Hisani yakitarajiwa kuanza kutimua nyasi kesho katika Uwanja wa CCM Mkwakwani,Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia ligi hiyo huku lengo likiwa kuongeza hamasa.

''TFF haijakosea kuleta mashindano ya Ngao ya Hisani Tanga,nampongeza Rais Wallace Karia na kamati yake ya utendaji kuleta michuano hii Tanga,wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi''alisema Khalid.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Khalid Abdallah leo amesema kuwa, mashindano ya Ngao ya Hisani kuletwa Tanga siyo 'Fever' ila ni kutokana na Mkoa huo kuwa kitovu cha  Mchezo wa Mpira wa miguu nchini Tanzania.

"Mashindano kuletwa Tanga ni faraja kubwa,Tumshukuru President Karia na Kamati yake ya utendaji.Watu wajaze Uwanja baada ya TFF kuichagua Tanga na siyo fever ni Kwa sababu ni kitovu cha mpira nchini"alisema Khalid Abdallah.

Mwenyekiti huyo wa Mashindano wa TFF alisema kwamba,watu wanapaswa kununua Ticket zao kwa utaratibu wa NCARD mapema ili kuingia uwanjani na kwamba hakutauzwa ticket za mkononi.

Alisema, Kwa jukwaa kuu ukiachilia wageni waalikwa VIP Kwa upande wa kulia na kushoto Ticket zitauzwa kwa bei ya Shilingi 30,000/- na maeneo mengine yote yaliyobaki ticket zitauzwa kwa bei ya Shilingi 10,000/-.

Aidha ametoa Rai kwa wale ambao watakosa uwezo wa kifedha kuingia uwanjani kusalia majumbani na kuangalia mchezo huo kupitia Azam TV huku akisisitiza kusema kuwa Watoto wadogo wanapaswa kuachwa majumbani Kwa ajili ya Usalama.

Alisema kuwa milango ya Uwanja wa CCM Mkwakwani itakuwa wazi kuanzia majira ya Saa nne (4) asubuhi kwa wapenzi kuweza kuingia kupata fursa ya kushuhudia mchezo wa kwanza wa ngao ya Hisani kati ya timu za Azam FC ya Dar es Salaam na Singida Fountain Gate.
Mwisho.


 

No comments:

Post a Comment