Tuesday 8 August 2023

POLISI TANGA YAFUNGUA JALADA LA UCHUNGUZI WA MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO KUJINYONGA KWA KUTUMIA SHUKA,,,


Pichani ni kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake'Hawapo pichani'juu ya ya tukio la mwanafunzi wa darasa tano kujinyonga.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

JESHI la Polisi Mkoani Tanga limefungua milango ya kupokea taarifa kutoka kwa Mtu yeyote mwenye kuhusiana na kifo cha Mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya mchepuo wa Kiingereza Tripple A, Severine Pius KIyagaza anayedaiwa kufa kwa kujinyonga huko eneo la Pongwe nje kidogo ya Jiji la Tanga.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Henry Mwaibambe alisema jana kuwa taarifa za tukio hilo zimetolewa katika kituo cha polisi Pongwe ambapo polisi walifika eneo la tukio na mwili wa Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 11 na kuuchukua kuendelea na taratibu za kufanyiwa uchunguzi na baadaye kukabidhiwa ndugu zake kwa ajili ya shughuli za maziko kufanyika.

Alisema kwamba,tukio la Kifo cha mwanafunzi Severin Pius Kyagaza lilitokea Agosti 2 mwaka huu Saa 10 Jioni ambapo alikutwa akiwa amejinyonga Chumbani kwake kwa kutumia Shuka na kuwa baada ya hapo mwili wa marehemu Daktari aliufanyia uchunguzi kwa kushirikisha ndugu na Polisi.

Kamanda huyo wa Polisi Mkoani Tanga alisema kwamba,baada ya hapo kumejitokeza malalamiko kupitia mitandao ya kijamii kuwa  baadhi ya ndugu wa marehemu walifukuzwa wasiingie Mochwari wakati wa uchunguzi huku pia ikielezwa mwili wa Severine ulikuwa na jeraja mkononi.

Kutokana na malalamiko hayo, Polisi wamefungua Jalada la uchunguzi ambapo Kamanda Mwaibambe alifafanua kuwa mwili wa marehemu hufanyiwa uchunguzwa kisheria na kuna taratibu zinatakiwa kufuatwa, idadi ya watu wanaotakiwa kuwepo chumba cha uchunguzi na daktari ndiye mwenye mamlaka ya kuamua nani anayestahili kuwepo pindi uchunguzi unapokuwa ukifanyika.

Aidha Fomu ya uchunguzi ndiyo inayoonesha idadi ya watu wanaotakiwa kuwepo kwenye uchunguzi wa marehemu ambapo hata Hivyo alisistiza kusema kuwa askari Polisi walikuwepo na hata wazazi wa marehemu na kwamba kwenye chumba kujaa watu wengi siyo utaratibu na ni kinyume cha sheria.

Alisema kuwa malalamiko hayo yanachukuliwa kwa uzito mkubwa na uchunguzi utafanyika na yote ambayo wanafamilia wana mashaka nayo yatafanyiwa kazi huku akibainisha kuwa taarifa za awali ilizopata Jeshi la Polisi kupitia wanafunzi wenzake kilichosababisha tukio ni kauli za Kaimu makamu mkuu wa shule hiyo kutokuwa sahihi ambapo baada ya wanafunzi kukusanyika Uwanja wa kukutania.

Alisema, Kaimu mkuu huyo wa shule alizungumza ambayo huenda  yaliwafanya wanafunzi kujisikia vibaya baada ya Kiongozi huyo kusema kuna watoto wazazi wao hawajachanga kwenda matembezi mkomazi ni kana kwamba hawapendwi na wazazi wao jambo ambalo huenda lilileta vikwazo.

Pamoja na hayo Kamanda huyo wa Polisi Mkoani Tanga alisema kwamba watayafanyia kazi yote ambayo wamekuwa wakiyapata na kwamba Endapo kuna mtu ana taarifa za ziada awasiliane na Jeshi la Polisi ili kuweza kufanyiwa kazi na kujua chanzo cha kifo hicho, amewaomba wahusika kufanyia subira.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment