Saturday 12 August 2023

MASHINDANO NGAO YA HISANI WAMILIKI WA MAHOTELI JIJINI TANGA WAJIVUNIA MAPISHI YA KIPWANI,,,




NA SOPHIA WAKATI,TANGA

WAMILIKI wa Mahoteli na Nyumba za kulala wageni Jijini Tanga wamesema, wamejipanga vizuri katika kuwahudumia Wageni wanaofika kwa ajili ya shughuli mbalimbali ambapo wameahidi kuwapatia huduma za kimsingi kama vile chakula aslia na hata malazi bila kuwepo kwa usumbufu wa aina yeyote.

Meneja mapokezi wa Hoteli ya Mtendele Hoteli iliyopo eneo la Chuda Jijini Tanga, Zaina Mohamediamesema kwamba, katika utekelezaji wa majukumu yao,wamejipanga katika utoaji wa huduma bora kwa wateja wao hatua ambayo lengo lake ni kuvutia wageni zaidi kutembelea Tanga.

“Kiukweli tumejipnga kuwahudumia vyema wateja wetu katika utoaji huduma zenye viwango vya ubora na hata gharama zetu kuwa nafuu mkwa upande wa malazi na hata chakula tunachoawapatia”alisema Mwakilishi huyo wa Hoteli ya Mtendele iliyopo maeneo ya Chuda katika Halmashauri ya Jiji la Tanga.

Zaina alisema kwamba, katika kutoa huduma hizo wamekuwa wakihakikisha wanapika chakula chenye ubora huku malazi yakiwa katika kiwango kinachostahiki jambo ambalo wageni wanaofika kupata huduma wamekuwa wakilifurahia wakati wote na hivyo kuwafanya kuwa na wateja wa uhakika.

Alisema kuwa, kwa mgeni anayefika Tanga, ataweza kufurahia chakula asilia kilichotengenezwa katika mahadhi ya Pwani sanjari na meneo ya malazi kuwa tulivu, safi  na usalama ukiwa wa hali ya juu ambapo amewato wasiwasi wateja wanaotembelea Jiji la Tanga kwamba watakapofika watahudumiwa vyema.

“Kwa kweli kwa upande wetu si watoa huduma za Hoteli Tanga tumejipanga vyema…Tanga ni Jiji la aina yake.Mgeni atakapofikia kwenye Hoteli na Nyumba zetu za kulala wageni atapata huduma ambazo hataweza kusahau, ubora wa vyakula na malazi ni wa hali ya juu, tunapika chakula asilia”alisema Zaina.

Akizungumzia mashindano ya ngao ya Hisani yanayoendelea kufanyika Jijini Tanga,Zaina alisema,licha ya kuwepo kwa wageni wengi lakini wote wanahudumiwa katika viwango vinavyostahiki na hivyo hakuna malalamiko kutoka kwa wateja wao huku akisisitiza kusema Tanga ni shwari nwakati wote.

Mwisho.


Pichani mkono wa kushoto ni Meneja mapokezi wa Hoteli ya Mtendele Hoteli iliyopo eneo la Chuda Jijini Tanga, Zaina Mohamedi akiwa katika utekelezaji wa majukumu ambapo amesema amejipanga kutoa huduma bora kwa wageni.
























Picha mbalimbali za hotel ya Mtendele jijini Tanga.

 

No comments:

Post a Comment