Thursday 17 August 2023

POLISI TANGA JINSI ILIVYOFANIKIWA KUMNASA FUNDI UJENZI KWA MAUAJI YA MKE WAKE NA SHEMEJI YAKE,,,

Pichani mkono wa kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tanga ,Almachius Mchunguzi akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, akitoa taarifa kwa waandisho wa habari wa mkoa wa Tanga.

NA SOPHIA WAKATI,MUHEZA

POLISI Mkoani Tanga inamshikilia fundi ujenzi Swalehe Miraji Ally miaka 38 mkazi wa Mkanyageni kwa tuhuma za kuwaua watu wawili akiwemo mke wake Mwanahawa Hassan Mohamed miaka 24 na shemeji yake Sauda Sufian Mbogo miaka 20 kwa kutumia panga kwa kile kinachodaiwa kuwa imeetokana na vivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tanga ,Almachius Mchunguzi akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, amemtaja mtuhumiwa wa Kosa hilo kuwa ni Swalehe Miraji Ally (38) ambaye ni Fundi Ujenzi wilayani Muheza.

Alisema taarifa za mauaji hayo zilitolewa  katika kituo kidogo Mkanyageni na ndugu wa marehemu ambapo polisi walijipanga kwenda eneo la tukio na kuikuta miili ya Mke wake huyo Hawa Hassan na Shemeji yake Sauda Sufiani.

 Kamanda huyo wa Polisi alisema kwamba, umahiri wa askari wake uliwezesha kumtia nguvuni Mtuhumiwa Swalehe aliyekuwa amekimbilia  huko Mkoani Tabora alikokuwa amekwenda kwa ajili ya kujificha.

‘’Polisi ilifanya msako wa kumsaka mtuhumiwa Swalehe kwa kuvitumia vyanzo vyetu,tukapata taarifa yuko mafichoni mkoani Tabora,tumefatilia tumemtia nguvuni ‘’Alisema Kamanda Mchunguzi.

 Kamanda huyo wa jeshi la polisi mkoani Tanga,Mchunguzi aliesema kuwa katika mahojiano na polisi Swalehe amekiri kutenda kosa kutokana na ugomvi wa kifamilia na upelelezi ukikamilika atafikishwa Mahakamani kukabiliana na tuhuma inayomkabili.

Wakati huo huo huko eneo la Kwamungwe Wilayani Handeni Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Heleni Sila Dahel (28) aliyeuawa kwa kukatwa kichwa  na mtuhumiwa wa tukio hilo amefahamika kwa jina la Rajabu Athumani (32) tayari amekamatwa na amekiri kutenda kosa hilo na upelelezi ukikamilika atapandishwa Mahakani.

Mwisho.

 


 

No comments:

Post a Comment