Thursday 17 August 2023

POLISI TANGA,YAWASHIKILIA WATU WATANO KWA TUHUMA ZA MAUAJI KUMNYONGA MWENDESHA BODABODA,KUMTOA MACHO NA KUPORA PIKIPIKI ,,


Pichani mkono wa kushoto ni Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Tanga,ACP Almachius Mchunguzi leo akitoa taarifa  kwa waandishi wa habari Ofisini kwake juu ya Operesheni iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Tanga.

 NA SOPHIA WAKATI,TANGA

JESHI la polisi Mkoa wa Tanga linawashikilia watu watano kwa tuhuma za Kumnyonga na kumtoboa Macho mwendesha bodaboda Kimbo Mandia Kirita (52) mkazi wa Kwamaraho Kata ya Malezi iliyopo wilayani Handeni mkoani Tanga.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga,ACP Almachius Mchunguzi alitoa taarifa hiyo leo Ofisini kwake wakati akizungumza na Waandishi  wa Habari ambapo alisema kwamba tukio hilo lilitokea Usiku wa kuamkia Agosti sita (6) mwaka huu.

Aliwataja waliokamatwa katika tukio hilo ni watu watano (5) ambao wameweza kutambuliwa kwa majina yao kuwa ni Ezekiel Thomas Lazaro, Miraji Haji, Seif Haji Baraka, Omari Salehe na Amina Athumani huku mmoja alikutwa na pikipiki ya marehemu.

Alisema kuwa, taarifa za tukio hilo zilitolewana ndugu wa marehemu saa 3;00 asubuhi katika kituo cha polisi wilayani Handeni na ndugu wa marehemu na kuanza msako maeneo mbalimbali  wilani hapo iliyofanikisha kuwabaini watuhumiwa.

ACP Mchunguzi alisema kwamba baada ya kupokea taarifa za tukio hilo polisi walifika eneo la tukio katika kijiji cha Kwamaraho kata ya Malezi ambapo na kumkuta marehemu Likimbo akiwa amenyongwa kwa kutumia kamba ya katani kisha kukatwa kichwani kipande cha macho na pikipiki yake kuibiwa.

‘’Polisi baada ya kupata taarifa tukaanza kufanyia operesheni maeneo mbalimbali ya wilaya ya Handeni na kufanikiwa kuwatia nguvuni watu watano kuhusishwa na mauaji hayo’’Alisema Kamanda Mchunguzi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapo,Mchunguzi alibainisha kueleza kwamba watuhumiwa wanaendelea na mahojiano baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa Mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Mwisho. 


No comments:

Post a Comment