Thursday 14 September 2023

HAFLA YA KUMUAGA KATIB U MSTAAFU WA CCM MKOANI TANGA, SULEIMAN ILIKUWA HIVI AKIWASIHI VIONGOZI NA WANACHAMA KUILINDA NGOME YA CCM ,,,


Pichani ni katibu mstaafu wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Tanga,Suleiman Mzee Suleiman katika hafla ya kumuaga mara baada ya kutoa shukurani zake akitoa nasaha kwa viongozi na wanachama wa chama hicho akisisitiza kufanyakazi kwa kuzingatia kanuni na taratibu.


NA SOPHIA WAKATI,TANGA
VIONGOZI  na wanachama wa Chana Cha Mapinduzi CCM, Mkoani Tanga wameaswa kufanya kazi Kwa uadilifu huku wakiimarisha ushirikiano kuepuka kukigawa chama hicho kunachotawala.

Ushauri huo umetolewa na Katibu mstaafu wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Tanga,Suleimani Mzee Sukeimani wakati alipokuwa AK hutubia Wanachama kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Legal Naivera Jijini Tanga.

Katika mazungumzo yake,Suleimani alisema,Chama Cha Mapinduzi kinaongozwa Kwa mujibu wa Katiba na kwamba Viongozi na wanachama wake wanapaswa kukitumikia kwa Uadilifu.

Alisema kwamba,kufanya kazi ndani ya chama hicho tawala ni utumishi wenye misingi ya kujitokea na kwamba isije ikatokea mtu kuingia CCM kwa na lengo ya kwamba ataweza kupata utajiri.

Suleimani aliwasilisha shukrani zake Kwa wanaCCM Mkoani Tanga Kwa kumpatia ushirikiano mkuhwa katika kipindi choye alichopata kuhudumu.

Aliwasihi kuendeleza msgikamano na viongozi waliopo hatua ambayo itasaudia kukijenga chama huku alibainisha kuwa ni jukumu la kila mwanachama popoye alipo kuhakikisha CCM inashinda ngazi zote na kuendelea kutawala.

Amempongeza Mwenyekiti wa CCM Mkoani Tanga Rajabu Abdurahaman Kwa kuiwezesha CCM kurejesha Kata ambazo zikioata kutwaliwa na upinzani akisema hivi Sasa maeneo hayo yamebakia historia Kwa kurejeshwa chama Cha Mapinduzi CCM.

Amemwelezea kiongozi huyo wa CCM Mkoani Tanga kuwa ni mpenda watu na mwenye mahusiano mazuri ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM na hata Serikalini akihimiza kuungwa mkono.

Mbali na hayo alimuimba Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoani Tanga kumfikishia Salaam zake Kwa Mwenyekiti wa CCM Taiga Rais Dk Samia Suluhu Hassan Kwa hatua yake ya kuonesha kujali maslahi ya watumishi ndani ya CCM kwa maelezo kuwa Kwa jinsi kiongozi huyo anavyopambana siyo muda mrefu maslahi yao yataenda kuimarika.

Sherehe ya kuagwa Kwa Katibu huyo wa CCM Mkoa wa Tanga ilihidhuriwa na wanaCCM wakiwemo wanachama wa kawaida,wabunge, viongozi wa Serikali na hata wakuu wa idara huku wakipata fursa kuonesha upendo wao Suleiman kwa kumpatia Zawadi mbalimbali.

Kutokana na Suleimani Mzee Suleimani kunga'atuka kwenye nafasi hiyo ya ukatibu wa CCM Mkoani Tanga anayeshikilia wadhifa huo kwa Sasa ni Selemani Sankwa aliyetokea Mtwara.
Mwisho.


 

Pichani mkono wa kushoto ni ni Mwenyekiti wa CCM mkoani Tanga,Rajabu Abdurahaman akimkabizi katibu mstaafu zawadi Suleimani Mzee Suleiman mkono wa kulia akiwa na familia yake.

Pichani mkono wa kulia mwanamke ni katibu tawala wa mkoa wa Tanga,Pili Mnyema akimkabidhi zawadi Katibu mstaafu wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Tanga,Suleiman Mzee Suleiman kushoto ya utendaji kazi bora.
 
Pichani mkono wa kushoto ni katibu mstaafu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Tanga,Suleiman Mzee Suleiman akiteta kitu na katibu wa CCM mkoa wa Tanga anayeshikilia nafasi hiyo kwa sasa,Suleiman Sankwa kulia siku ya hafla ya kumuaga

Pichani mkono wa kulia ni katibu Tawala wa mkoa wa Tanga,Pili Mnyema akimkabidhia katibu mstaafu wa chama cha mapinduzi mkoani Tanga,Suleiman Mzee Suleiman kushoto kwa utendaji bora.




 Pichani ambaye amevaa gauni la kijani ni  Meneja wa  RUWASA mkoa wa Tanga,Mhandisi Pendo Lugongo  akimkabidhi zawadi Katibu Suleiman Mzee Suleiman kwa kuguswa na utendaji wake.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)imetoa Zawadi ya Kifaa maalum cha kupozea na kuchemshia Maji ‘Water Dispensar’ ikiwa ni shukurani na pongeza kwa utendaji kazi wa Katibu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Tanga kwa ushirikiano aliouonesha kwa wafanyakazi wa .

Hayo yamejiri katika hafla ya kumpongeza Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Suleimani Mzee Suleimani aliyemaliza muda wake ambapo Wadau mbalimbali walijitokeza kumpongeza na kimpatia Zawadi;

Meneja wa RUWASA Mkoani Tanga, Mhandisi Pendo Lugongo alisema,Uongozi wa CCM Mkoa wa Tanga umeweza kushirikiana vyema na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira hatua ambayo imerahisisha utendaji kazi.

 “Sisi kama RUWASA tunakiri kupata ushirikiano kutoka kwa CCM Mkoa kupitia Katibu wake Suleimani Mzee Suleimani, tumefarijika nasi kuwasilisha Zawadi yetu ikiwa sehemu ya kuungana naye”alisema Lugongo.

Mbali na Mhandisi huyo wa RUWASA kuwalisha zawadi hiyo kwa Katibu huyo wa Chama Caha Mapinduzi Mkoa wa Tanga, Wadau wengine wakiwemo Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliwasilisha zawadi zao ikiwa sehemu ya kuonesha shukrani zao.

Wabunge hao wakiongozwa na Husna Shekiboko walikabidhi fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni tano huku WanaCCM wengine waliohudhuria nao wakitoa zawadi zao na hivyo kufanya Sherehe hiyo kufana.

Kutokana na Katibu huyo wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga kumaliza muda wake wa utumishi wake, nafasi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga kwa sasa inashikiliwa na Suleimani Sankwa aliyetokea Mtwara.

Mwisho.




Pichani mkono wa kushoto ni Meneja wa RUWASA kushoto mara baada ya kukabidhi zawadi wakiwa kwenye picha ya pamoja na katibu mstaafu katikati na Mhandisi wa miradi TANGA UWASA,Rashid Shabani mkono wa kushoto.





No comments:

Post a Comment