Monday, 25 September 2023

KAMANDA TANGA,MCHUNGUZI AELEZA OPERESHENI YA KUSALIKISHA SILAHA KWA WATAKAO KAIDI,,

Pichani ni kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Tanga,Almachius Mchunguzi ametoa akizungumza na waandish wa Habari ofisini kwake mpango kabamde umewekwa wa kufanya operesheni. 

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

POLISI Mkoani Tanga limewataka Watu wote wanaomiliki Silaha kinyume na taratibu kuanza kuzisalimisha kwa hiari na kwamba hatua kali za kisheria hazitasita kuchukuliwa kwa watakaokaidi kufanya hivyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi ametoa kauli wakati akizungumza na waandish wa Habari ofisini kwake ambapo amesema mpango kabamde umewekwa wa kufanya operesheni.

Mchunguzi alisema kwamba, zoezi la kusalimisha Silaha kwa hiari lilianza Septemba Mosi mwaka huu na litamalizika Oktoba 31 ambapo aliwasisitiza wanaomiliki kinyume na taratibu kutumia mwanya huo kuzirejesha.

Alisema kwamba,watakaodiriki kusalimisha Silaha kwa hiari wakati huu hawatachukuliwa hatua ila kwa wale watakaokaidi hadi kipindi Operesheni ya kuwasaka itakapoanza, wakibainika watachukuliwa hatua kali.

“Watakaosalimisha sasa hivi hawatachukuliwa hatua ila watakaokaidi hadi Operesheni ya kuwasaka itakapoanza watambue kuwa hatua kali za kisheria hazitasita kuchukuliwa dhidi yao”alisema Kamanda huyo wa Polisi.

Kamanda huyo wa Polisi Mkoa wa Tanga alisema kwamba, wale waliyo tayari kusalimisha Silaha wanapaswa kuzifikisha kwenye vituo vya Polisi vilivyopo karibu yao na ofisi za Serikali za mitaa na vijiji.

Aidha pia ametumia nafasi hiyo kwa kuwaasa Watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya kuacha tabia hiyo akisema kuwa operesheni maalum ya kuwasaka itaendeshwa.

“Polisi tutaendesha Operesheni kali kwa wauzaji wa dawa za kulevya, ni vyema wanaojihusiaha na vitendo hivyo kuacha na kutafuta kazi nyingine”alisema alisema Kamanda huyo wa jeshi la polisi Mchunguzi.

Pia ametoa wito kwa Raia wema kuendelea kushirikiana na Polisi katika kubadilishana taarifa zitakazosaidia kudhibiti vitendo vya uhalifu na kuifanya Tanga kuendelea kuwa salama wakati wote akishauri uwepo ulinzi shirikishi.

Amewaasa Wananchi kutojihusiaha na ununuzi wa vitu vya Wizi kwa maelezo kuwa pindi watakapofanya hivyo na ikatokea kukamatwa watahusishwa katika uhalifu.

Mwisho. 

 

No comments:

Post a Comment