MAPENZI

NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
MAITI ya mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha kidereko wilayani Handeni,Zubeda Mbamila (35) imekutwa imenyongwa shingini kwa kutumia kanga kwenye nyumba ya kulala wageni inayofahamika kwa jina la Betha
Gest house iliopo wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,Liberatus Sabas alisema kuwa mwili huo wa marehemu Zubeda umegunduliwa juni 7,mwaka huu saa 4.30 asubuhi na mhudumu wa gest hiyo baada ya kukuta chumba hicho kimefungwa kwa nje.

Sabas alisema kuwa baada ya kuona mlango wa chumba hicho kimebanwa kwa nje ndipo kutilia mashaka na kufungua ambapo alikuta mwili huo umetelekezwa huku ukining"inia pembeni ya kitanda ukiwa na barua yenye
ujumbe pembeni.

"Baada ya kukuta hali hiyo aliondoka na kutoa taarifa polisi ambapo alifika na kuuchukua mwili wa marehe pamoja na ujumbe huo ulioandikwa na mume wake kwamba amemuua kwa wivu wa kimapenzi na kwamba hata watakutana kwa mungu hata yeye anakwenda kujiua mto msangazi uliopo wilayani hapo"alisema Sabas.

Kamanda huyo alisema katika mahojiano mhudumu na jeshi la polisi alisema awali maremu waliwasili nyumba hiyo ya kulala wageni juni 6,mwaka huu saa 7.00 mchana akiwa na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Musa Masaija (59) mkazi wa Ushirika chanika wote wakitokea wilayani Handeni kwa lengo la kupumzika.

Alisema wapenzi hao wanatabia ya kuja kwenye nyumba hiyo mara kwa mara na kwamba baada ya kupatiwa chumba hicho waliingia ambapo hawakuonekana tena kutoka kama kawaida yao.

Alibainisha KUWA tukio hilo lilitokea saa 9.00 usiku na ndugu
wamepatikana ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya magunga wilayani Korogwe kusubiri ndugu wa marehemu kuuchukua na kuendelea na taratibu za mazishi.

Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha mauaji hayo sanjari na kumpata mume aliyesababisha mauaji hayo kwa lengo la kumfikisha mahakamani kukabiliana na tuhuma hiyo ya mauaji.
mwisho.


NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MWANAMKE mmoja Vumilia Michael (30) mkazi wa Amboni nje kidogo na Jiji la Tanga amekutwa amekufa chumbani kwake kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa kimapenzi.

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga,Juma Ndaki akithibisha kutokea kwa tukio hilo amesema limetoa saa mbili usiku huko katika kijiji cha Mabokweni Amboni wilayani Tanga.   

Alisema taarifa zilitolewa na viongozi wa mtaa katika kituo kidogo cha polisi Amboni kuwa mwanamke huyo Vumilia amefariki ndani ya chumba chake alichokuwa akiishi.

Ndaki alisema baada ya kupokea taarifa hizo polisi walifika na kuukuta mwili wa mwanamke huyo ukiwa ndani ya chumba chake huku ukiwa na majeraha ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu za shingo.

 Alisema chanzo ni wivu wa kimapenzi ambapo awali kabla ya kifo chake marehemu alikuwa akiishi na mtu anayedhaniwae kuwa na mahusiano ya kimapenzi katika nyumba hiyo ambapo walikuwa na mgogoro.

Alisema kuwa mara kwa mara majirani wamekuwa wakiwasikia wapenzi hao wakizozana juu suala la uaminifu ambapo mwanaume alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa ana mahusiano na mpenzi mwingine.

“Baada ya polisi kufika eneo la tukio nakufanya uchunguzi,marehemu alikuwa na mpenzi wake kukaibuka ugomvi,mara mwanaume huyo alitoka na kuuacha mlango wazi kutokomea kusiko julikana”alisema kaimu huyo wa polisi Ndaki.

Alisema baada ya majirani kutilia shaka ndipo walipolazimika kuingia ndani na kuukuta mwili wa marehemu Vumilia ukiwa unamajeraha na kupelekea kuwafahamisha viongozi wa mtaa huo na kutoa taarifa polisi.

Hata hivyo hakuna aliyekama kuhusishwa na tukio hilo huku jeshi la polisi likiendelea na msako mkali kumsaka mtuhumiwa aliyefanya mauaji hayo ya kinyama ili kufikishwa mahakamani jibu tuhuma hiyo.
Mwisho.

NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE

JESHI la polisi mkoani Tanga,linaendelea na msako mkali maeneo mbalimbali ya mkoa huo kwa lengo la kumnasa Mussa Masaiji (59) aliyemuua mpenzi wake katika nyumba ya kulala wageni Betha Gest house
iliyopo wilayani Korogwe.

Marehemu aliyefahamika kwa jina la Zubeda Mbanila (35) mkazi wa kijiji cha kidereko wilayani Handeni mkoani hapo,amekutwa amekufa kwa kunyongwa kwa kutumia kanga kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni inayofahamika kwa jina la Betha Gest house iliopo wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,amanda wa Polisi mkoa wa Tanga,Jaffar Mohamed akizungumza na waandishi wa habari juzi
alisema kuwa mwili wa marehemu Zubeda umegunduliwa juzi  saa 4.30 asubuhi na mhudumu wa nyumba hiyo ya wageni baada ya kukuta chumba hicho
kimefungwa kwa nje.

Jaffar alisema kuwa baada ya kuona mlango wa chumba hicho umefungwa  kwa nje mhudumu alitilia shaka akaamua kuufungua kwa funguo ndipo akakuta mwili wa mwanamke huyo ukining"inia na pembeni ya kitanda kukiwa na
barua yenye
ujumbe mrefu.

Alisema ujumbe huo ambao unaonekana kuandikwa na mtu aliyejiita ni mumewe unaeleza kuwa ameamua kumnyonga kwa sababu ya kumhisi kwamba marehemu Zubeda alikuwa akitembea na wanaume wengine jambo ambalo
lilisababisha ashindwe kujizuia kwa sababu alikuwa akimpenda mkewe hivyo kaamua kumuua ili naye ajiue kwa kujitosa katika mto Msangasi uliopo Wilayani Korogwe

" Ujumbe huo uliendelea kwa kwa kusema umeandikwa na mume wake kwamba amemuua kwa wivu wa kimapenzi na kwamba watakutana kwa Mungu kwani hata yeye anakwenda kujiua mto msangazi uliopo wilayani hapo
Korogwe"alisema Jaffar.

Alisema  kwa mujibu wa maelezo ya  mhudumu  wa nyumba hiyo ya kulala wageni ni kuwa marehemu aliwasili hapo  juzi saa 7.00 mchana akiwa na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Musa Masaija (59) mkazi wa Ushirika chanika wote wakitokea wilayani Handeni kwa lengo la
kupumzika.

Alisema wapenzi hao wanatabia ya kwenda kwenye nyumba hiyo mara kwa mara na kwamba baada ya kupatiwa chumba hicho waliingia ambapo hawakuonekana tena kutoka kama kawaida yao.

Alibainisha kuwa tukio la kumnyonga mwanamke huyo inaonekana lilifanyika  saa 9.00 usiku na kwamba mwili wa marehemu Zubeda tayari ndugu wamejitkeza na kuchukua ulikuwa umehifaadhiwa katika hospitali
ya Magunga.
Mwisho.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MKAZI mmoja wa Makorora jijini Tanga, Idi Mohamed miaka ( 20) anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani Tanga kwa  tuhuma za kumbaka mtoto wa kike  mwenye umri wa miaka 9.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Jaffar Mohamed alieleza kuwa lilitokea June 15 mwaka huu saa 2.30 usiku katika  mtaa wa msaka ngoto Makorora jijini mjini hapo..

Jaffar alisema mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa la ubakaji  wakati mtoto huyo alipokosa pesa ya kuingia katika kibanda cha video ambapo alimpa shilingi Elfu moja ili mtoto huyo aweze kuingia na kuangalia picha kwenye banda la Video.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa  huyo alikaa hadi mwisho wa kuangalia picha na kuondoka na mtoto huyo hadi katika banda bovu lililopo jirani na eneo hilo kisha kutekeleza tendo hilo la kinyama dhidi ya mtoto .

Hata baada ya kufanya kitendo hicho mtuhumiwa  huyo aliondoka na kumuacha mtoto huyo akielekea nyumbani kwao, na ndipo mtoto huyo alipokwenda kumueleza mzazi wake kuhusia na tukio hilo.

Kwa Mujibu wa Polisi mzazi wa mtoto huyo alimpeleka katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kwa uchunguzi baada ya mtoto huyo kulia kwa uchungu kutokana na maumivu makali aliyoyapata.

Hata hivyo Mtuhumiwa huyo anaendelea kushikiliwa na Polisi hadi hapo uchunguzi utakapokamilika ili aweze kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma hiyo.
Mwisho.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MAHAKAMA kuu kanda ya Tanga, imemtaka Majaliwa Abdallah(30) mkazi wa Mwakijembe wilayani Mkinga kwenda kutumikia kifungo cha miezi 12 nje baada yakupatikana na hatia ya kumuua mjomba wake Thomas Nzoka bila kukusudia ambapo ni kinyume na kifungu namba 195 kidogo cha kwanza kinachohusu mauaji.
Hukumu hiyo imetolewa  na Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Tanga,Iman Aboud mbele ya wakili wa serikali,Shose Naiman na wakili mtete wa kujitegemea Erick Akaro.
Mwanasheria wa serikal,Shose Naiman alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo tarehe 25/11/2014 huko eneo la Mwakijembe katika kilabu ya Pombe ya kienyeji wilayani Mkinga mkoani Tanga.
Alieleza mahakamani hapo kwamba siku ya tukio  mshitakiwa akiwa katika kilabu hiyo na mjomba wake palizuka ugomvi kuzozana na kumpelekea mshitakiwa kuondoka eneo hilo.
Shose alisema kuwa marehemu Thomas alimfuata na kuanza kumpiga ndipo mshitakiwa katika kujihami alimsukuma na kupelekea kuanguka na  kuvunjika mguu wa kulia ambapo alishirikiana na wananchi wengine kumpeleka katika Zahanati yaMwakijembe kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
 “Baada ya kufikishwa katika Zahanati hiyo Novemba 28,mwaka 2014 alifariki na uchunguzi wa madaktari ulionyesha marehemu Thomas alimwagikiwa na damu kwenye mapafu na kusababisha kifo chake”alisema mwanasheria huyo wa serikali Shose.
Aliendelea kueleza kwamba baada ya tukio hilo polisi walifika kwenye eneo la tukio na mshitakiwa kukamatwa kupelekwa katika kituo cha polisi Maramba na baadae alipelekwa kwa mlinzi wa amani ambako amekiri kutenda kosa hilo na kupandishwa mahakamani kwa kosa hilo la mauaji.
Kwa upande wake wakili mtetezi wa mshitakiwa,Erick Akaro aliiomba mahakama hiyo kuangalia katika upande wa kutoa adhabu kwani mshitakiwa ni kosa lake la kwanza na hana rikodi mbaya na tayari ameshakaa miaka mitatu mahabusu na pia kuangalia mahusiano yake na marehemu.
Wakili mtetezi aliendelea kueleza mahakamani hapo kwamba pia ni kijana nguvukazi na mazingira ya kosa yanaonyesha kwamba marehemu ni chanzo cha kifo chake nani tegemezi katika familia yake hivyo  ameiomba mahakama hiyo kuzingatia katika kutoa adhabu ndogo kwa mshitakiwa.
Baada ya Jaji mfawidhi,Iman kujiridhisha na maelezo hayo ndipo alipomtaka mshitakiwa Majaliwa kwenda kutumikia kifungo cha miezi 12 nje kuwa mwana jamii wa kawaida na endapo atajihusisha na kosa lolote ndani ya muda huo basi atarudishwa kuwajibika na kosa lake linalomkabili.


Mwisho. 
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
Ofisa wa Jeshi la wananchi (JWTZ)  MT.69500 S/SGT,John Komba(50) na wenzake watatu akiwamo Sophia John  (17) ambaye ni binti yake wamepandishwa katka mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya Tanga kwa shtaka moja la kumuua kondakta wa daladala jijini hapo.

Wakiliwa serikali Denata Kazungu akiwasomea washtakiwakosa lao jana wakiwamo askari mgambo wawili Warioba Nchama (28) na Benard Semchaa (25) mara baada ya kufikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi.

Kazungu alieleza mahakamani hapo kuwa lidaiwa mahakamani hapo mbele ya hakimu mafawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi  Tanga,Hilda Lyatuu.

Alieleza kwamba Ofisa MT.S/SGT.John na wenzake walitenda kosa hilo januari 27 mwaka huu huko katika kambi ya jeshi Nguvumali iliopo  Jijini Tanga,washtakiwa hao wote kwa pamoja walimuu a Salimu Kassim maarufu (Rambo) ambaye ni dereva wa daladala.

Aliendelea kudai kuwa washtakiwa hao walimchukua kondakta huyo kutoka kwenye daladala na kumpeleka eneo hilo la kambini ambako walishambulia ambapo ni kosa kinyume na kifungu 196 na 97 cha kisheria ya kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.  .

Baada ya kusikiliza shitaka hilo ndipo,Hakimu Lyatuu aliwaambia washtakiwa hao kuwa hawapaswi kujibu chochote kutokana na uzito wa shauri lao na kwamba shitaka lao linastahili kufikishwa mahakama kusikilizwa na jaji.

Hata hivyo,Hakimu huyo aliahirisha keshi hiyo hadi itakapotajwa tena Februari 12 mwaka huu na kesi hiyo haina dhamana ambapo alisema watakwenda mahabusu.
Mwisho.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tanga,imemhukumu mkazi mmoja wa wilayani Pangani,Elinema Kibo (23) kunyongwa mpaka kufa baada ya kupatiakana na hatia katikakesi ya mauaji mke wa kaka yake huku mwingine akiachiwa huru.

Hukumu hiyo ambayo imetolewa juzi katika Mahakama hiyo kuu na Jaji Protas Rugazia mbele ya mawakili wa serikali,Mselei Mfinanga ambae alikuwa akisaidiana na Mwansiti Athuman.

Kesi hiyo ambayo ilianza kunguruma mwaka 2011 katika mahakama ya wilaya yaPangani na baadae kuhamishwa mahakama kuu Kanda ya Tanga,ilishirikisha washitakiwa wawili na mkazi wa kijiji cha Bweni wilayani hapo,Said Zuberi maarufu Chidi ambaye aliachiwa huru baada ya kukosekana na hatia.

Akiwakumbusha washitakiwa shitaka lao,wakili Mfinanga alieleza mahakamani hapo kuwa Kibo na Chidi walitenda tuhuma hiyo Februaly 2,mwaka 2008 huko Pangani katika kijiji cha Amboni.

Mfinanga aliendelea kueleza kwamba washitakiwa wote kwa pamoja Februal 2,mwaka 2008,siku na muda usiofahamika katika kijiji cha Amboni wilayani Pangani walimuua Magdalena Elias kwa kile kilichodaiwa hakuwa muaminifu kwenye ndoa yake.

“Baada ya kumuua Magdalena mshitakiwa Kibo ulitiliwa shaka na polisi ambapo ulikubali na kuongoza kuwaonyesha mwili ulipo na pia ulikutwa na simu pamoja na viatu vya marehemu aina ya malapa ukiwa unavitumia”alisema wakili huyo wa serikali Mfinanga.

Aliendelea kueleza kuwa mshitakiwa Kibo baada ya kukamatwa uliwalalamikia  polisi kwamba marehemu Magdalena ambaye alikuwa ni shemeji yake mke wa kaka yake,hakuwa muaminifu kwenye ndoa yake na hivyo alikuwa akiitia aibu familia yao.

Washitakiwa hao wote wawili waliokuwa wakikabiliwa na kesi hiyo ya mauaji walikuwa wakitetewa mahakamani hapo na wakili wa kujitegemea,Alfred Akaro.

Jaji,Rugazia baada ya kujitosheleza na maelezo ya pande zote yaliyotolewa katika kesihiyo ndipo alitoa hukumu hiyo ya kumtaka mshtakiwa namba moja,Kibo kunyongwa mpaka kufa huku Chidi akimwachia huru kwa kukosekana na hatia kwenye kesi hiyo.

Alisema kwamba ametoa hukumu hiyo kama fundisho ili kwa watu wengine ambao wanatabia kama hiyo ya kujichukulia sheria mkononi ni kosa kinyume na sheria ya nchi yetu.
Mwisho.    


No comments:

Post a Comment