Sunday 8 September 2024

TANGA CITY MARATHON 2024 IMESEMA MAANDALIZI YAMEKAMILIKA KWA UPANDE WA ZAWADI NA KUWATAKA WASHIRIKI WENYE SIFA KUJITOKEZA,,,,,

Pichani katikati Msemaji Kamati ya Mashindano Tanga City Marathon, Fatma Mbinga, akizungumza na Vyombo vya Habari katika Ukumbi wa Amboni kwenye Hoteli ya Tanga Beach Resort iliopo  Jijini Tanga mkono wa kulia ni ni Miongoni mwa Wadhamini Mushi kutoka Bumaco.


Usajili 'Tanga City Marathon' 2024 kufanyika kwa mtandao 'Online'.


NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MUANDAAJI wa mashindano ya Riadha 'Tanga Marathon 2024' amesema mchakato umekamilika na kuwataka washiriki wenye vipaji vya mchezo huo  kujitokeza kukamilisha taratibu na kupata fursa ya kufanya mazoezi na kuendeleza kipaji chake.

 Hata hivyo amesema mashindano hayo yamekuja kivingine huku Usajili kwa washiriki wake unafanyika kwa njia ya mtandao 'Online' kupitia marathon. imartgroup.co.tz.

Msemaji Kamati ya Mashindano hayo, Fatma Mbinga, akizungumza na Vyombo vya Habari huko katika Ukumbi wa Amboni kwenye Hoteli ya Tanga Beach Resort iliyopo  Jijini Tanga alisema, huu ni msimu wa nane (8) kwa mbio hizo kufanyika Jijini hapo. 

Alisema, kwa mwaka huu usajili wa kumwezesha mtu kushiriki Tanga Marathon unafanyika kupitia njia ya mtandao huku akibainisha kuwa wamekuja kivingine na zawadi ni zenye kuvutia kwa washindi mbio hizo.

"Tunataraji Mbio zitakuwa tarehe 22/09/2024 leo ni uzinduzi tunatangaza jezi yetu ambayo ni nzuri, Tshirt yetu hii ina nafasi kubwa ya kufanya udhamini"alisema  Fatma huku akitanabaisha kwamba medali zitatolewa kuanzia washindi wa mbio za Kilomita 5,10 hadi 21.

Aidha amesema kwamba, kwa mwaka huu 'Tanga Marathon' imejipanga kurejesha fadhila kwa jamii kwa kusaidia uimarishaji miundombinu ya elimu hususani madawati. 

Tayari Kampuni ya Bima ya Bumaco, iMart Group Ltd na Tanga Beach Resort zimejitokeza kudhamini mashindano ya Tanga Marathon Mwaka 2024.

Naye Mwenyekiti wa chama cha riadha Mkoa wa Tanga,Sophia Wakati alitumia nafasi hiyo kwa kutoa wito kwa wadau kujitokeza kwa wingi kufadhili mchezo huo na mingine ya aina hiyo inayokuwa ikifanyika katika mkoa huo wa Tanga. 

Alisema kwamba,kwa kufanya udhamini Chama cha riadha itatoa fursa kwao kujifunza mambo mbalimbali huku wakinufaika na fursa za uwekezaji zilizoandaliwa na Serikali yao katika mkoa huo uliopo pembezoni mwa Bahari ya Hindi.
Mwisho.
Pichani mkono wa kushoto mwanamke ni Msemaji Kamati ya Mashindano Tanga City Marathon, Fatma Mbinga, akionyesha sare itakayotumika mwaka huu 2024 kwa Vyombo vya Habari katika Ukumbi wa Amboni kwenye Hoteli ya Tanga Beach Resort iliopo  Jijini Tanga.

Pichani Msemaji Kamati ya Mashindano Tanga City Marathon, Fatma Mbinga, wakionyesha Medali ambazo zitatolewa kwa washiriki kwa Vyombo vya Habari katika Ukumbi wa Amboni kwenye Hoteli ya Tanga Beach Resort iliopo  Jijini Tanga mkono wa kulia ni ni Miongoni mwa Wadhamini Mushi kutoka Bumaco.

No comments:

Post a Comment