Saturday, 18 January 2025


 UWT KOROGWE KOROGWE VIJIJINI WATAKIWA  KUACHANA NA WATU WANAOJIPITISHA KUANZA KAMPENI,,,,


Pichani ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Korogwe vijijini,Hadija Mshahara akiwataka wajumbe wa baraza hilo kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo na kumuombea rais Dk.Samia Suluhu Hassani ili aweze kufanya kazi vema.


NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) Korogwe Vijijini,Hadija Mshahara, amewataka Wajumbe wake kumuombea kwa Mungu, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan apate afya njema ili kuweza kuendelea kuwahudumia vyema Watanzania.

Mshahara ametoa nasaha hizo Juzi kwenye kikao hicho cha UWT Korogwe vijijini kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Korogwe Mkoani Tanga.

Katika Mkutano huo, Mwenyekiti huyo wa UWT Korogwe Vijijini alimuelezea Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwamba ni mchapakazi aliyefanikisha upatikanaji wa miradi mingi ya maendeleo nchini Tanzania na hata wikayani Korogwe.

Kutokana na hali hiyo aliwaomba Wajumbe wa UWT kuendelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu Rais Dk. Samia ili aendelee kuwa mwenye afya njema na hivyo kumudu kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia Wananchi.

Mbali na hayo,Mwenyekiti huyo wa UWT,Mshahara amewasihi Wajumbe wake kuendelea kumuunga mkono Mbunge wao aliopo madarakani hatua ambayo itamwezesha kufanikisha kazi mbalimbali kupitia miradi iliyopewa Korogwe Vijijini.

"Mbunge Mnzava amefanya mambo makubwa katika wabunge wote waliopita kila mmoja alifanya kwa nafasi yake ila Timothy Mnzava amefanya makubwa tuendelee kumpatia ushirikiano "alisema Hadija Mshahara Mwenyekiti wa UWT Korogwe Vijijini.

Aidha pia amewapongeza Wajumbe wake kwa kazi kubwa waliyoifanya kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa akisema wamechangia upatikanaji ushindi mkubwa hatua ambayo pia imewezesha Wanawake wengi kushika nyadhifa kwenye vitongoji na Vijiji..

Pamoja na hayo amepongeza utendaji kazi wa madiwani wa Viti maalum licha ya changamoto wanazokumbana nazo aliongeza kuwasisitiza Wanawake kuwa vinara wa hamasa kuanzia ngazi ya familia hatua ambayo itasaidia kuujenga CCM.
Mwisho.

Pichani ni wajumbe wa UWT Korogwe Vijijini mkoani Tanga,juzi wakifuatilia taarifa kwenye kikao cha kawaida cha baraza la UWT kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM wilayani hapo.



Katika picha ni miongoni mwa wajumbe wa UWT Korogwe Vijijini wakifuatilia taarifa za kikao hicho

No comments:

Post a Comment