Saturday, 18 January 2025

NDEGE ZISIZO NA RUBANI ZAFANYA MASHAMBULIZI SUDAN,,


 Shambulizi la ndege zisizo na rubani nchini Sudan limepiga kituo cha umeme na kuacha majimbo mawili ya mashariki bila umeme.

Mamlaka inalaumu vikosi vya wapiganaji wa RSF, ambavyo chini ya wiki moja iliyopita vililenga bwawa la umeme wa maji kaskazini.

Watu milioni 12 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano hayo tangu vita vilipoanza Aprili 2023.

Walioshuhudia walisema takribani ndege sita zisizo na rubani zilipiga kituo cha umeme katika mji wa Showak.

Kuna ripoti kwamba uwanja wa ndege wa Atbara katika jimbo la River Nile pia ulilengwa pamoja na kituo kikuu cha umeme katika mji wa Sinja ulioko kusini-mashariki.

Vikosi vya wapiganaji wa RSF vimekuwa vikilenga miundombinu muhimu katika maeneo ya Sudan ambayo yanadhibitiwa na jeshi.

Pande zote mbili zimetekeleza unyanyasaji mkubwa dhidi ya raia.

Serikali ya Marekani imeweka vikwazo dhidi ya mkuu wa jeshi na kiongozi wa RSF. UN inaonya kuwa inazidi kuwa hatari kwa raia na mashambulizi ya kikabila dhidi ya wachache.

No comments:

Post a Comment