Saturday, 18 January 2025

 

WASSIRA MAKAMU MWENYEKITI MPYA BARA CCM,,,

Mkutano Mkuu wa chama tawala nchini Tanzania, CCM, umemuidhinisha Stephen Wassira kuwa Makamu mwenyekiti mpya wa chama hicho upande wa Tanzania bara.

Stephen Wassira, anachukua nafasi ya AbdulRahman Kinana ambaye alijiuzulu wadhifa wa Makamu mwenyekiti wa CCM, hatua iliyoridhiwa na mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Rais wa Tanzania.

Kinana alihudumu katika nafasi hiyo kwa takribani miaka miwili na miezi mitatu, tangu kuchaguliwa kwake mwezi Aprili 2022. Makamu mwenyekiti mpya wa CCM Tanzania Bara, Wassira, ni mzee wa umri wa miaka 80.

Ana uzoefu wa kufanya kazi serikalini katika nafasi mbalimbali za Naibu Waziri na Waziri katika Wizara tofauti tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere hadi awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete.

Wassira anatarajiwa kuwa nguzo muhimu ya ushauri kwa mwenyekiti Samia hususan kusimamia nidhamu ndani ya CCM wakati Tanzania ikielekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu, huku Samia akiwania kuchaguliwa ili kushika kipindi cha pili na cha mwisho cha urais.

Kwa mujibu wa Katiba ta CCM Makamu mwenyekiti Tanzania Bara ndiye mwenyekiti wa kamati ya maadili na nidhamu ya chama hicho.

No comments:

Post a Comment