DC KOROGWE DK.MWAKILEMA,,WANANCHI TUMIENI MADAWATI WIKI YA SHERIA YALIYOANDALIWA NA MAHAKAMA KUTATUA KERO ZAO,,,,,
Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe,Dk.William Mwakilema akiwahutubia wananchi wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi Wiki ya sheria iliyoandaliwa na Mahakama wilayani hapo.
NA SOPHIA WAKATI,KORODWE
WANANCHI wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, wametakiwa kutumia vizuri madawati yaliyowekwa kwenye Halmashauri katika kuwasilisha kero zao ili kupatiwa msaada wa kisheria hivyo kuweza kudai na kupata haki zao.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe,Dk.William Mwakilema wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi Wiki ya sheria iliyoandaliwa na Mahakama wilayani hapo.
Kauli hiyo aliitoa kwenye Uzinduzi uliofanyika Viwanja vya Chuo cha ualimu TTC Korogwe akiwataka Wananchi kutumia madawati mahsusi yaliyoandaliwa kuelimisha Wananchi namna ya kuweza kudai haki zao.
Alisema ,Serikali imeandaa mazingira mazuri yanayolenga kuwaondolea changamoto wananchi huku akibainisha kuwa kwenye madawati yaliyowekwa wapo wataalam kwa ajili ya kusaidia watanzania.
Pamoja na hayo Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi wa Korogwe kuhakikisha kuwa katika wiki hii ya sheria wanakuwa tayari katika kuwapokea na kuwapatia ushirikiano wadau watakaofika maeneo yao kuwaelimisha.
Alisema kwamba, katika wiki hii ya sheria idara ya Mahakama na maafisa wengine wanaoshughulika na masuala ya kisheria watatembelea maeneo mbalimbali kutoa elimu kwa wananchi wote bila kuyasahau makundi maalum wakiwemo wanafunzi.
Vile vile alisema kuwa, elimu inayotolewa ina umuhimu mkubwa na kwamba katika nyakati hizi za utandawazi watoto wanakabiliwa na changamoto nyingi kulingana na mazingira ya utandawazi huku watu wakikwama kupata haki zao kutokana na kutojua eneo la kukimbilia baada ya kufanyiwa dhuluma.
"Makundi mbalimbali yatatembelewa tujitokeze kwa wingi kuwasikiliza maafisa wetu wanaokuja kutupatia elimu, mara nyingi watoto wanaopata shida wanashindwa kujua mahali kwa kujitetea"
Kauli mbiu ya wiki ya Mahakama kwa Mwaka huu inasema "Tanzania ya 2050 kutoa nafasi kwa taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia maendeleo".
Pia amewataka Watoto kutumia fursa hiyo kama maono yao juu ya Tanzania ya miaka ijayo akisema kuwa wao ni kundi ambalo linatarajiwa kuwa ndio viongozi wa miaka ijayo.
Ametumia fursa hiyo kuishukuru idara ya Mahakama na taasisi nyingine kwa kuonesha ushirikiano lengo likiwa kuwezesha wiki hiyo ya Mahakama inayoadhimishwa maeneo mbalimbali hapa nchini.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Hakimu mwandamizi wa Mahakama ya Mombo,Alfayo Laizer alitumia nafasi hiyo kwa kuwataka Wanafunzi kutumia muda wao vizuri kusoma kwa vile wazazi, walezi na serikali hutumia fedha nyingi na hata muda kuwawezesha kusoma.
Mwisho.
VIONGOZI wakiwa kwenye matembezi uzinduzi wiki ya sheria wilayani Korogwe.
Pichani mwakilishi kutoka ofisi ya mwanasheria wa serikak akiwasilisha salamu za ofisi hiyo.
Pichani katikati mwanaume ambaye amevaa fulana nyekundu ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Dk.William Mwakilema akiongoza matembezi Uzinduzi wiki ya sheria,mkono wa kushoto ni mwanamke ambaye amevaa kofia na suluali nyeusi ni Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya Korogwe,Sikitu Mwalusamba na kulia ni afisa kutoka jeshi la polisi wilayani hapo.
No comments:
Post a Comment