HAKIMU MWALUSAMBA AFUNGUKA..TUMEJIPANGA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA WADAU,,,WIKI YA SHERIA,,,
Pichani ni Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya Korogwe,Sikitu Mwalusamba akizungumzia wiki ya sheria 2025 kwa kushirikiana na wadau wilayani hapo jwalivyojipanga kutoa elimu na Mada mbalimbali zitakazotolewa kwa wananchi.
NA SOPHIA WAKATI, KOROGWE.
HAKIMU mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya Korogwe,Sikitu Mwalusamba watatumia vema wiki ya sheria 2025 kwa kushirikiana na wadau wilayani hapo imejipanga kutoa elimu na Mada mbalimbali kwa wananchi zitakazotolekupitia juma hilo na kutajwa baadhi ni kuhusu utaratibu wa kupata dhamana na kukata rufaa,
Hakimu huyo Mkazi Mfawidhi,Sikitu aliyasema katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi,ambapo alieleza wiki ya Sheria kwa Mwaka huu 2025,ambayo imezinduliwa tarehe 25 Januari mwaka huu.
Alisema, wiki hiyo iliyozinduliwa kwenye ofisi za Mkuu wa wilaya ya Korogwe kwa maandamano na kupita barabara ya Muembeni hadi kufika Viwanja vya chuo cha ualimu TTC.
Aidha,alisema Mgeni rasmi wa shughuli hiyo alikuwa Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Dk.William Mwakilema ambapo kwenye chuo hicho cha TTC pia kulifanyika Bonanza la michezo mbalimbali.
Kauli mbiu ya wiki ya Sheria 2025 ni "Tanzania ya 2050 nafasi ya taasisi zinazohudumia haki maadili katika kufikia malengo makuu yenye kufikia dira ya Taifa ya maendeleo".
Kwa mujibu wa Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Korogwe,Sikitu alisema kwamba hapo januari 26 Mwaka huu Kamati ya wiki ya Sheria imefanya kazi ya kutoa elimu kwenye Gereza la Manundu na baadaye Kwamngumi.
Aidha,alibainisha kueleza kwamba siku zinazofuata elimu itatolewa Chuo cha ualimu TTC Korogwe, chuo cha afya Hisani, Magunga hospitali na kwenye shule za msingi.
Hakimu mkazi mfawidhi huyo aliongeza mada mahsusi ikiwemo ile ya ukatili wa kijinsia,jinsi ya kupata dhamana,namba ya kukata rufaa na mengine yataelimishwa kupitia wiki hiyo.
Hata hivyo,aliwataja miongoni mwa Wadau watakaohusika na kutoa elimu mbali na Mahakama pia watakuwepo Takukuru, Polisi, ofisi ya mwendesha mashtaka na wengine.
Hata hivyo,ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha Wananchi kujitokeza lengo kuweza kusikiliza elimu itakayotolewa,kuuliza maswali ili kuweza kupata uelewa zaidi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment