Sunday, 26 January 2025








AFISA UHAMIAJI KOROGWE,HAMIS AFUNGUKA MAFANIKIO KAMPENI YA MJUE JIRANINI YAKO,,,

Pichani ni Mrakibu Mwandamizi Idara ya Uhamiaji wilayani Korogwe,Hamisi Juma akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kampeni Mjue jirani tako.  

NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
KUPITIA 'Kampeni ya mjue jirani yako', Idara ya Uhamiaji wilayani Korogwe imefanikiwa kueneza elimu kwa wananchi juu ya shughuli wanazozifanya na hivyo kufanikiwa kudhibiti ukiukwaji wa taratibu na sheria za uhamiaji.

Mrakibu mwandamizi Idara ya Uhamiaji wilayani Korogwe,Hamisi Juma akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  jana alisema kuwa kampeni hiyo ni endelevu ikiwaunganisha watu wote katika suala zima la uelewa wahamiaji haramu na mambo yote yanayohusiana na uhamiaji.

Amesema kuwa, lengo la kampeni hiyo ni kuiwezesha Idara ya Uhamiaji kufanikiwa kuwahudimia Watanzania na kuwapa haki raia wa kigeni kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

"Hii ni kampeni bora na itaendelea kuwepo kwani inawatenganisha wahamiaji na wasiokuwa wahamiaji alisema Afisa uhamiaji huyo wa wilaya ya Korogwe''Hamisi Juma.

Akizungumzia zaidi alisema kwamba, wamekuwa wakitumia Mikutano ya kata WADC kufikisha elimu kwa wananchi anbapo wamekuwa na mahusiano mazuri na watendaji kata.

"Tunashirikiana vyema na watendaji kata wanapokuwa na vikao wanatualika na tunatumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa wananchi"alisema''Alisema Afisa huyo wa Idara ya Uhamiaji Hamisi.

Kuhusu kampeni ya 'mjue jirani yako' alisema,pia wamekuwa wakitumia vyombo vya habari katika kufikisha elimu kwa wananchi huku akiwasihi wanaopata elimu hiyo kufikisha kwa wengine.

Aidha,alisema kuwa, awali Wananchi walio wengi walishindwa kufahamu kwa kina juu ya shughuli za idara ya uhamiaji walijua kuhusu hati za kusafiria ila kupitia kampeni hivi sasa wengi wamefahamu na wanashirikiana nao vyena.

Alisema, kampeni ya 'mjue jirani yako' imesaidia kuwatambua wanaoishi Tanzania kinyume na taratibu za uhamiaji huku faida nyingine ikiwa kuwawezesha Wananchi kuelewa kazi za uhamiaji.

Katika suala la utoaji elimu kwa umma,idara ya uhamiaji wilayani Korogwe imeweza kuyafikia maeneo kadhaa ikiwemo tarafa ya Mombo, Bungu,Magoma na tarafa ya Korogwe Mjini.
Mwisho 


 

No comments:

Post a Comment