Monday, 25 December 2023

TANESCO TANGA NA ZECO ZANZIBAR ZATOKA SARE YA 2-2,PAMBANO LA KIRAFIKI ZIARA YAO MKOANI TANGA 2023.



Pichani mkono wa kushoto ambaye amesimama ni Meneja wa Tanesco Mkoani Tanga Mathias Solongo akizungumza na wachezaji wa Tanesco Tanga na Zeco ya Zanzibar akieleza kuridhishwa kwake na mchezo huo wa kirafiki kuimarisha mahusiano kazini na kujenga urafiki.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
TIMU za Soka Tanesco Tanga na ile ya Shirika la kuzalisha Nishati ya Umeme ZECO Zanzibar zimeshindwa kutambia  baada ya kutoka Sare ya magoli 2 - 2.

Katika mchezo huo wa vuta nikuvute uliopigwa Jana viwanja vya Popatlal Jijini Tanga, timu ya Zeco ..ndio ilikuwa ya kwanza kuliona lango la wapinzani wao.

Zeco Zanzibar ilianza kuandika goli lake dakika 21 kipindi Cha kwanza kupitiaNabil Hamoor juma Jaja ambalo liliongeza nguvu ya mashambulizi katik mchezo huoAlly Salim.

Baada ya kuongia Kwa goli Hilo,Tanesco Tanga ilijipanga na kusawadhisha kupitia Jackson Chilu dakika 31 na Faidin Kombo dakika ya 47 ambayo yalikuwa muhimu katika mchezo huo.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya aina yake kila timu kuongezea mashambulizi ambap Kwa Zeco yalileta mafanikio baada ya mchezaji Seleman Rashid dakika ya 65 kuifungia goli la pili ambalo liliwapa nguvu kuondoka uwanjani hapo huku goli la pili likifungwa na  Ally Salim ambalo lilikuwa muhimu katika mchezo huo.

Kocha wa timu ya Zeco  Zanzibar,Seifu Mzee Aweso alisema,mchezo huo ulikuwa mzuri ingawa awali wapinzani wao walionekana kumudu kuutawa mchezo huo,lengo ni kufanya ziara na kubadilisha mawazo na kujenga uzoefu sehemu ya kazi.

Katibu msaidizi wa timu Zeco,Mgaza Mhaya Ramadhan amesema amekuja na timu ya watu 53 wakiwemo wachezaji na viongozi kufanya ziara ya siku nne ikiwemo kucheza mechi za kirafiki na wenyeji wao Tanesco ya mkoa wa Tanga.

Alisema,hali ilitokana na wao ZECO kukosa muda wa kufanya mazoezi ya maandalizi tangu walipoingia Jijini Tanga ingawa mapungufu yaliyoonekana mchezoni walimu waliyafanyia kazi.

Meneja wa Tanesco Mkoani Tanga Mathias Solongo alielezea kuridhishwa kwake na mchezo huo wa kuimarisha mahusiano akisema umechezwa kwa nidhamu ya hali ya juu kwa vipindi vyote.

"Nitaendelea kuimarisha kikosi changu,kuwapa muda wachezaji kufanya mazoezi kujiandaa na mashindano yoyote ambayo yayajitokeza"Alisema Meneja huyo Solongo.
Mwisho.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MBUNGE wa Chama Cha Mapinduzi CCM Jimbo la Amani Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, Abdul Yusuph Maalim ameshauri kuwekwa Ligi fupi ya Soka itakayohusiana na mambo ya Muungano. 

Ushauri huo umetolewa jana Viwanja vya Popatlal Jiiini Tanga, katika ziata ya siku MBUNGE huyo Maalim alisema kwamba uwepo wa Ligi hiyo utasaidia katika kuimarisha Muungano uliopo nchini. 

Alisema kwamba,ligi hiyo itakayokuwa ya Muungano ni vyema ikazihusisha timu za taasisi za Serikali akitolea mfano wa Tanesco,ZECO ya Zanzibar hatua aliyoieleza kuwezesha undugu kuimarika.

"Iwekwe ligi fupi ya Mashirika  itakayohusiana na mambo ya Muungano Tanesco, Zeco Zanzibar na wengine kuzidi kujenga udugu tuliokuwa nao na Muungano wetu"alisema Maalim. 

Pamoja na hayo Maalim alisema,iko haja kwa Serikali kuyenga bajeti ndogo kwa ajili ya Wafanyakazi kufanya ziara za mafunzo na hata michezo inayowasaidia kujenga mahusiano. 

Alisema,anafamu kiwa Serikali ina mzigo mzito ila ziara hizo za mafunzo kwa wafanyakazi nazo zina umuhimu katika kuongeza tija kazini. 

"Ifike muda kuwe na bajeti maalum kwenye hizi taasisi,tunajua Serikali ina mzigo mzito ila bajeti ndogo italeta tija baada ya mfanyakazi kuwa kazini muda mrefu"alisema Maalim. 

Mbunge Maalim kabla ya kutumbukia kwenye Siasa alipata kuwa mfanyakazi wa ZECO Zanzibar ambapo amesema taasisi nyingi za Serikali zinafanya Safari kwa kuiitegemea.

Katika mchezo huo wa Kirafiki kati ya ZECO Zanzibar na Tanesco Tanga matokeo yalikuwa mabao 2 kwa 2 huku mchezo ukiwa wenye upinzani mkali. 

Akizungumzia mchezo huo Meneja wa Tanesco Mkoani Tanga Mathias Amon Solongo alisema,ulikuwa wenye kuvutia na ulichezwa kimsingi wa ustaarabu.

Aliwashukuru wanamichezo walioshiriki mchezo huo huku akiahidi kukipeleka Zanzibar kikosi cha timu ya Tanesco ya Tanga.

Mwisho







 

No comments:

Post a Comment