Monday 4 December 2023

POLISI TANGA YASHIKILIA BOTI KWA KUTUMIKA KWA UVUVI HARAMU WA KUTUMIA BARUTI,,,



Pichani ni Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Almachius Mchunguzi akieleza jinsi polisi walivyofanikiwa kukamata boti iliyokuwa inatumika kwa uvuvi haramu.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
JESHI la polisi mkoani Tanga linashikilia Boti aina ya Fible ambayo inadaiwa kutumiwa na Wavuvi kwa kuvua Samaki kinyume na taratibu za kisheria kwa kutumia 'Baruti',.

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Tanga,Almachius Mchunguzi akithibitisha kutokea kwa tukio hilo alisema polisi wakiwa doria za majini na kuitilia shaka boti hiyo na kuifuatilia wavuvi walikimbia kusiko julikana.

Alisema kwamba tukio hilo lilitokea Novemba 21/11/2023 huko bahari ya Hindi katika Kisiwa cha Jambe kilichopo Wilayani Tanga huku ikiwa na kilogram 30 za samaki.

"Polisi tunashikilia boti ya uvuvi na samaki kilogram 30,baada ya kuikama tunafuatili kuwasaka wahusika,taratibu nyingine ziweze kuchukuliwa dhidi yao''Alisema kamanda Mchunguzi.

Alisema kuwa, katika Operesheni zake, Polisi wamefanikiwa kukamata boti moja aina ya Fible ambayo ilikuwa na Wavuvi wanaotumia baruti pindi wanapovua Samaki.

Aidha alisema kwamba, wavuvi hao walifanikiwa kukimbia huku boti iliyokuwa na Kilogramu 30 za Samaki wa aina mbalimbali waliitelekeza ikishikiliwa na Jeshi la Polisi.

"Polisi tumejipanga kuimarisha doria kufanya nchi kavu na Baharini, ambapo sasa hivi zimeanza kuzaa matunda tarehe 21 Novemba katika Kisiwa cha Jambe Wilayani Tanga Polisi tumefanikiwa kukamata boti aina ya 'Fible' ikiwa na wavuvi wanaotumia baruti"alisema Mchunguzi. 

Hata hivyo,Kamanda Mchunguzi alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili hatua kuchukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika na suala hilo ambalo ni kinyume na taratibu za sheria.

Katika tukio jingine, Kamanda Mchunguzi alisema, watu 21 wamekamatwa na bangi Kg 43, Mirungi Kg 124.5 na Heroine gram 242 huku watuhumiwa wanne wakikamatwa kwa kusafirisha wahamiaji haramu.

Vilevile watuhumiwa saba (7) ambao ni raia wa Ethiopia wamekamatwa kwa kuingia nchini pasipokuwa na vibali.

Pamoja na hayo tukio jingine linamuusisha mtu mmoja aliyekamatwa kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia Silaha aliyoitaja kuwa ni Panga.

Kamanda Mchunguzi alisema kuwa ni moja sehemu ya mafanikio ya Jeshi la Polisi ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja yaani Oktoba 22 mpaka Nov 27,2023 ambapo pia Polisi walikamata watu 107 katika misako mbalimbali Mkoani Tanga. 
Mwisho.

No comments:

Post a Comment