Monday 4 December 2023

KAMANDA TANGA,MCHUNGUZI AMEWATAKA WASAFIRISHAJI ABIRIA KWA NJIA YA PIKIPIKI KUFUNGA ''TRUCKING SYSTEM''

Pichani mkono wa kushoto ni Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Tanga, Almachius Mchunguzi  akiwa na msaidizi wake kulia akiwa ofisini kwakwe akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ikiwemo ya wasafirishaji abiria kwa kutumia pikipiki kwa waandishi wa habari mkoani hapo. 

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
KAMANDA wa jeshi la polisi mkoani Tanga ,Almachius Mchunguzi  amewataka wasafirishaji abiria kwa kutumia Pikipiki maarufu Bodaboda, kufunga vifaa maalum 'Trucking System' zitakazowasaidia kuonesha mizunguko yao pindi wanapoyatekeleza majukumu yao.

Ametoa wito huo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Tanga lengo likiwa kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na kuweza kutimiza malengo yao. 

Kamanda Mchunguzi alisema kuwa, watu wanaofanya biashara ya bodaboda wanatakiwa kuwa makini na wakichukua tahadhari kwa vile wamekuwa wahanga wakuu wa vitendo vya uhalifu hususani nyakati za usiku. 

"Waendesha bodaboda nawashauri wafunge Trucking System ambayo inaweza kusaidia kufuata mienendo ya Pikipiki hata ikiibiwa ni rahisi jeshi la polisi kufuatiliwa matukio ya uhalifu" alisema Kamanda Mchunguzi. 

Aidh,Kamanda Mchunguzi aliwataka bodaboda hao kuhakikisha wanajisajili katika Vijiwe vyao hatua ambayo itawawezesha kufahamiana kirahisi na pia kudhibiti watu walio wahalifu.

Pia ametumia nafasi hiyo kwa kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano wao wanaouonesha kwenye ulinzi shirikishi huku wakitoa taarifa za uhalifu kwa Jeshi la Polisi Mkoani Tanga. 

Katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka,Kamanda Mchunguzi pia amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zisizo za msingi zinazoweza kuepukika.

Alisema,Jeshi la Polisi litaendelea kufanya operesheni kali kudhibiti madereva wasiozingatia sheria za Usalama barabarani ambapo amesisitiza suala zima la uzingatiaji sheria za barabarani. 

Mwisho. 



No comments:

Post a Comment