Pichani ni Mkuu wa dawati la elimu kwa Umma kutoka ofisi ya TAKUKURU mkoani Tanga,Frank Mapunda akitoa taarifa kwa waandishi wa habari akimwakilisha, Victor Swela ambaye ni Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
TAASISI ya Kuzuia na kupabana na Rushwa TAKUKURU mkoani Tanga imebaini kuwepo Kwa mapungufu kwenye miradi 28 ya maendeleo na hivyo kuokoa fedha za Serikali ya Tanzania kiasi cha billion 5,072,000,000.00.
Mkuu wa dawati la elimu kwa Umma kutoka ofisi ya TAKUKURU mkoani Tanga,Frank Mapunda aKItoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari akimwakilisha, Victor Swela ambaye ni Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga.
Alisema kwamba fedha hizo zimeokolewa baada ya kufanya uchunguzi na ufuatiliaji kwa upande wa uzuiaji rushwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo 60 yenye thamani ya billion 10,621,271,204.00.
Mapunda alisema julai mpaka Septemba mwaka 2023 katika ufuatiliaji wao wamebaini miradi 28 yenye thamani ya shilingi za kitanzani billion 5,072,000,000.00 ilibainika kuwa na mapungufu ambapo Takukuru ilishauri namna ya kurekebisha.
Aidha.alisema Mapungufu hayo yalibainika huko wilayani Handeni kwenye mradi ujenzi wa madarasa 15 kupitia mradi wa BOOST,madarasa 02 ya mfano, matundu 6 ya vyoo, bembea na kihisi moshi huko shule ya msingi Kwamatuku wenye thamani ya Shilingi 2,779,300,000.
Mkuu huyo wa dawati la elimu kwa umma Takukuru,alisema kwamba moja ya mapungufu katika mradi huo ni mabati yenye thamani ya Shilingi 318,454,779.99 yalinunuliwa bila kuwa na vigezo kwa mujibu wa TBS ambapo mabati hayo yamerudishwa kwa mzabuni na uchunguzi umeanzishwa.
Pia mapungufu mengine yaliobainika ni rangi iliyopigwa kwenye kuta za majengo juu ya chuping imeanza kupauka kabla ya jengo kutumika na ushauri ulitolewa kwamba rangi ya jengo irudiwe.
Mapunda alisema katika wilaya ya Muheza kuna mapungufu kwenye ujenzi madarasa katika shule nane kupitia mradi wa BOOST Shilingi 855,400,000 pia mabati yenye thamani ya Shilingi 76,394,000 yalinunuliwa bila kuwa na vigezo kwa mujibu wa TBS na uchunguzi umeanzishwa.
Hata hivyo,Mradi mwingine uliogundulika kuwa na mapungufu ni huko Wilayani Kilindi kulikuwa na ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu sita ya vyoo shule ya.msingi Negero.
Pia imo shule ya Kibirashi wilayani Kilindi,Tanga Jiji ujenzi wa shule moja ya.msingi Jaje ,ujenzi madarasa mawili shule ya msingi Bombo ujenzi wa.madarasa ya awali ya mfano shule ya msingi Mapojoni.
Pamoja na hayo, Takukuru awali ilifanya vikao na wadau wa utekelezaji miradi ya BOOST kabla ya kuanza na baada ya miradi kukamilika ambapo mrejesho ulitolewa juu ya ufuatiliaji wa miradi hiyo.
'' Lengo la Takukuru kufanya vikao kabla ya miradi kuanza ilikuwa ni kuziba mianya ya rushwa katika utekelezaji miradi ya BOOST,na vikao vya mrejesho ufuatiliaji vililenga kuziba mianya ya rushwa katika miradi mingine inayoendelea kutekelezwa kwenye Halmashauri zote zilizopo mkoani Tanga''Alisema Afisa huyo wa Takukuru Mapunda.
Aidha Mapunda alisema kwamba kwenye uchambuzi wa mifumo umefanyika ikiwa ni utekelezaji jukumu la kuzuia rushwa kwa wigo mpana jambo ambalo ni sehemu ya maboresho ya utendaji kazi za Umma.
Akizungumzia zaidi suala la uchamhuzi wa mifumo,Mapunda alisema kuwa, umefanyika uchambuzi wa mifumo tisa 9 lengo likiwa kupata tija ya mifumo imara isiyokwamisha utoaji huduma bora kwa wananchi na utendaji kazi za Serikali kwa ujumla wake.
Ameongeza kuwa mifumo hiyo ni usimamizi na ugawaji mbolea za ruzuku 2022-2023, uchambuzi wa mfumo wa uendeshaji wa bodi za maji za vijiji na uchambuzi mfumo wa mashine za POS kubaini mapungufu ya mfumo na kupata majibu ili kuboresha Mapato.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment