NA SOPHIA WAKATI,TANGA
Bingwa mtetezi wa bonanza la kumuenzi Baba wa taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere 2022 amekiri kwamba mshindi Suka Veteran ya jijini Dar
e salaam aliyeshinda kwa kufunga magoli 7-6 kwa mikwaju
ya penati amepatikana kihalali.
Kocha wa timu ya Kijichi veteran yenye masikani yake Mtoni
kijichi wilayani Temeke jijini Dar es alaam,Lenus Mwegobwe ameyasema hayo mara
baada ya kuisha pambano hilo la fainali.
Alisema kwamba wao ni washiriki na walijiandaa vizuri katika
kundi lao la timu nne na kufanikiwa kushinda hatua ya awali na kufanikiwa
kuingia hatua kucheza fainali kuhakikisha wanatetea ubingwa wao wa mwaka jana
lakini bahati haikuwa yao.
Mashindano yaliandaliwa vizuri,wapinzani wetu Suka veteran walifanikiwa
kuibuka bingwa kwa mikwaju ya penati 7-6 na kuibuka kuwa mabingwa Nyerere Day mwaka 2023
jijini Tanga.
‘’Tunakubali matokeo ya mchezo wa fainal,tunaipongeza timu ya
Mandingo veteran ya jijini Tanga waandaaji wa bonanza hilo,baada ya kukosa
ushindi tunakwenda kujiandaa na mabonanza mengine.
Pia ametumia nafasi hiyo kuwashauri wachezaji wa vilabu vya veterani
mbalimbali kujitokeza kwenye vilabu vyao ili kuweza kufanya mazoezi kujiweka
vizuri kiafya na kushiriki mabonznza.
‘’Maviterani tunatakiwa kujiweka vizuri kiafya,pia kukutana
kwenye mabonanza yanayofanyika mikoa mbalimbali kuweza kukutana na
kubadilishana mawazo’’Alisema kocha wa Kijichi veteran Lenus.
Mwisho.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
WADAU wa bonanza la kumuenzi Baba wa Taifa Mwalim Julias
Kambarage Nyerere wametumia fursa hiyo kuwashauri wachezaji wa zamani kujiunga
na vilabu vya veteran ili waweze kutunza vipaji vyao na kujenga mtandao ndani
na nje ya nchi.
Hata hivyo,amewashauri wawekezaji wa viwanda na makampuni mbalimbali
kujitokeza kuweza kudhamini vilabu vya veteran ili kuweza kutumia sekita ya
michezo kuweza kutangaza shughuli zao ndani na nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa timu ya soka Kitambi
Noma veteran yenye maskani yake jijini Arusha, Jemes Rugangila amesema mpira wa veteran umebeba kundi kubwa
wakiwemo watumishi na wafanyabiashara na wakubwa.
Alisema kwamba kwa kupitia klabu ya Kitambi Noma veteran
wamefanikiwa kujenga mtandao na klabu mbalimbali na ikiwemo Pars chini ya Muti veteran,Umoja
zinazoundwa na wafakazi na wafanyabiashara wa nchini Kenya.
‘’Sisi Klabu ya kitambi Noma veteran ni washiriki wa kudumu kwenye
mabonanza tuko chini ya Tanskim na mdhamini mkubwa TBL wamekuwa wakisapoti
safari zetu kutembea Tanzania na nje ya nchi’’alisema Mwenyekiti huyo wa
Kitambi Noma Jemes.
Alisema kwamba umoja huo wa vilabu vya veteran umebeba kundi
kubwa watumishi wa serikali na wanyabiashara wakubwa na wadogo lengo kubwa
kujenga urafiki wa kudumu kwa kutembeleana kupitia sekta hiyo ya michezo.
Akizungumzia zaidi ushiriki wao katika mabonanza ikiwemo la kumbukumbu
kumuenzi baba wa taifa Mwalim Julias Kambarage Nyerere lililoandaliwa na timu
ya Mandingo veteran ya jijini Tanga,lilikuwa zuri sana hatukuweza kuwa mabingwa
lakini tunajiandaa na mashindano mengine.
‘’Kushiriki mabonanza ni utaratibu wetu wa kawaida,katika
kundi letu bonanza la Nyerere Day tumecheza vizuri sana lakini hatukubahatika
kuwa washindi,tunakwenda kujiandaa na bonanza jingine la Madesho Day linalo tarajiwa
kufanyika mkoani Moshi.
‘’Mpira wa veteran umebeba kundi kubwa wengine wakiwa
wafanyakazi,wafanyabiashara,wenye kufanya maamuzi kwenye makampuni,wenye zaidi
ya miaka 35 ,hivyo wadhamini wanaweza kunufaika kutangaza biashara zao’’alisema
Jemes.
Klabu ya Kitambi Noma veteran ya jijini Arusha ina mpango
mkakati wa kuandaa mbio ya Marathon mwaka 2024 kwa kushirikisha vilabu
mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Amesema mbio hiyo itakayofahamika kwa kwa Kitambi Noma
Marathon 2024 itashikisha vilabu vyote vya veteran ndani na nje ya nchi lengo
kuweza kufurahi,kuendeleza urafiki iliojengeka kupitia sekta ya michezo.
Mwisho.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
Msemaji wa Timu ya Suka Veterani ya Jijini Dar es salaam, Ramadhani Athumani Mganga ametamba kwamba, ubingwa walioupata umetokana na maandalinzi ya kujiandaa na bonanza hilo kutimiza ndoto yao
Hata hivyo,amesema ni kutokana na mkakati uliopo baina ya wachezaji na viongozi kushirikiana kuibuka kuwa bingwa msimu huu wa 2023 na kufungua milango kujiandaa na mabonanza mengine yatakayojitokeza ndani na nje ya nchi.
Msemaji huyo,Ramadhani maarufu Bufon alieleza kuwa tulifanya maadalinzi ya muda mrefu chini ya kocha Boban na ilikuwa ni dhamira yao ya dhati kuibuka kuwa washindi.
Aidha,amewapongeza waandaji Mandingo veterani ya jijini Tanga kuandaa bonanza hilo ambalo limesaidia kuwakutanisha kukumbushana na kubadilishana mawazo na kuweza kujenga mtandao.
''Suka veterani ni klabu ambayo inaongoza kujikusanyia makombe mengi kupitia mabonanza na niwashiriki wa kudumu na tutaendelea kujipanga''Alisema msemaji huyo wa Suka veterani Ramadhan huku akiwasihi wachezaji wenye vipaji vya soka kujitokeza kujiunga klabu za veterani.
Aidha,alisema kwamba, kitu pekee wanachoweza kujivunia
ni uwepo wa wachezaji mahiri wakiwemo wale walioweza kuwika vipindi
vilivyopita.
“Sisi klabu ya Suka veteran tumekuwa na maandalizi toka mwaka jana, timu yetu
inayoongoza kwa makombe mengi.Tunawapongeza walioamdaa Bonanza wenzetu wa
mandingo veteran”
Alibaishani kuwa mara baada ushindi huo Kikosi kitaendelea kunolewa na Kocha wa Haruna Moshi maarufu ‘Bobani’kiukweli tumepata kombe tunawashukuru sana Mandingo veteran kwa kuandaa bonanza.
Hata hivyo,Msemaji huyo wa klabu ya Suka Veteran Ramadhan amesema Baada ya ushindi huo Suka Veteran wanakwenda kujiandaa mazoezi kuelekea Moshi kwa Bonanza
na baadaye Arusha kwa mchezo kama huo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment