Wednesday 18 October 2023

BONANZA LA TIMU ZA SOKA VETERANI KUMUENZI BABA WA TAIFA MWALIM JULIAS NYERERE LILIKUWA HIVI JIJINI TANGA 2023,,,

Pichani wa pili mkono wa kushoto ni Mjumbe kamati ya utendaji TFF Taifa,Hald Abdallah akimkabizi kikombe kapteni wa timu ya Suka Veteran ya jijini Dar es alaam mara baada ya kuibuka washindi bonanza la kumbukumbu kumuenzi baba wa taifa Mwalim Julias Nyerere uwanja wa Popatlaly uliopo jijini Tanga.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

BONANZA la Soka la kumbukumbu ya Kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere limetimua Vumbi katika Viwanja vya Popatlal Jijini Tanga.

Bonanza hilo limeshirikisha timu 16 kutoka mikoa mbalimbali ndani na nchi jirani ya Kenya,ikiwa ni ishara ya kuonesha mshikamano baina ya nchi mbili.

Kwa mwaka huu mshindi wa Bonaza hilo ni timu ya Soka ya Suka Veterani ya Jijini Dar es salaam ambao walifanikiwa kuwafunga Kijichi Veteran kwa Penalti 7 - 6.

Kwa matokeo hayo Suka Veterani ni baada ya kutoka sare ya ya bila kufungana na kuandaliwa mikwaju ya penati,wametwaa Kombe ambalo walikabidhiwa na Mjumbe wa Kamati ya utendaji TFF, Hald Abdallah.

Awali akizungumza wakati wa ufunguzi mashindano hayo ya Bonanza Mjumbe huyo wa TFF Halid Abdallah alisema kuwa , michezo inajenga mahusiano na udugu.

Aidha,aliwapongeza waandaji wa mashindano hayo ya Bonaza, Mandingo Veterani akiwasihi kuwa na ari hiyo hiyo ya kuandaa michezo inayosaidia kutanua wigo kufahamiana.

Mwisho.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

RAIS wa Timu ya Suka Veterani ya Jijini Dar es salaam, Ramadhani Athumani Mganga ametamba kwamba, ubingwa walioupata ni matokeo ya kuwa na kikosi kipana.

Mganga aliyasema hayo Jana katika Viwanja vya Popatlal Jijini Tanga eneo ambalo Bonanza la Soka kwa ajili ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere lilifanyika.

Alisema, kabla ya kufanyika kwa mashindano hayo wamefanya mazoezi ya muda mrefu wakijiandaa kushiriki michezo inayokwenda kwa mtindo wa Mabonanza.

Aidha Mganga alisema kwamba, kitu pekee wanachoweza kujivunia ni uwepo wa wachezaji mahiri wakiwemo wale walioweza kuwika vipindi vilivyopita.

“Sisi tunamekuwa na maandalizi toka mwaka jana, timu yetu inayoongoza kwa makombe mengi.Tunawapongeza walioamdaa Bonanza wenzetu wa mandingo veteran”

Mgangaalitanabaisha kuwa Kikosi chao kwa sasa kinanolewa na Kocha wa Haruna Moshi ‘Bobani’wamepata kombe amewashukuru mandingo kwa kuandaa bonanza. Mchezaji aliyeng’ara miaka iliyopita.

Baada ya ushindi huo Suka Veteran wataelekea Moshi kwa Bonanza na baadaye Arusha kwa mchezo kama huo.

No comments:

Post a Comment