Friday, 29 September 2023

TRA TANGA YAZINDUA KAMPENI YA TUWAJIBIKE KUTOA ELIMU KWA WAFANYABIASHARA NA WANUNUZI,,,,



Pichani mkono wa kushoto ni Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga,Thomas Masese akiwa katiika Uzinduzi wa Kampeni ya Tuwajibike yenye lengo la kuelimisha wafanyabiashara na wanunuzi umuhimu wakutoa na kudai risiti wanaponunua na kutoa huduma akiwatembelea baadhi ya wafanyabiashara jijini hapo.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

MAMLAKA ya Mapato TRA Mkoa wa Tanga imezindua Kampeni ya Tuwajibike kwa lengo la kuwaelimisha Wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kutoa risiti huku Wanunuzi nao wakitakiwa kutimiza wajibu wao wa kudai stakabadhi hizo kutokana na bidhaa ama huduma wanazonunua.

Katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo, uliofanyika leo barabara ya kumi na mbili jijini hapo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Tanga,James Kaji aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba, ambapo Kaji aliwataka Viongozi wa Wafanyabiashara kuwahimiza wanachama wao kuona umuhimu wa kutoa risiti.

Alisema , kwa mfanyabiashara kutumia Mashine za EFD  itasaidia Serikali kukusanya mapato yake kwa ukamilifu hatua ambayo pia itatoa fursa ya utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi na kupunguza changamoto.

Kaji amehimiza umuhimu wa Wafanyabiashara kushirikiana na Mamlaka ya Mapato TRA ili kuhakikisha Kodi zinalipwa ambapo alisisitiza matumizi ya mashine za Kielektroni sambamba na suala la wafanyabiashara kutoa risiti huku wanunuzi nao wakihamasishwa kudai risiti.

"Suala la kulipa kodi ni haki na hata vitabu vya dini vinaeleza  wajibu wa kila mtu,wafanyabiashara tulipe kodi kwa wakati kumsaidie rais Samia Suluhu Hassan kurahisisha ujenzi utekelezaji miradi ya maendeleo hapa nchi. 

Mkuu huyo wa wilaya ya Tanga,Kaji alitumia nafasi hiyo kwa kuwataka Waandishi wa habari kutumia taaluma zao katika kuielimisha Jamii kuona umuhimu wa kutoa na kudai risiti ambapo pia alitumia jukwaa hilo kuwasihi Mamlaka ya Mapato TRA kuona namna ya kuwatumia Wadau hao wa habari kuwa kiunganishi na Umma.

Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga,Thomas Masese alisema kazi inayofanyika kupitia Kampeni hii ya Tuwajibike ni kuelimisha, kufuatilia yale TRA inayofundisha na kuona kama yanatekelezeka kubwa likiwa suala la watu kutoa na kudai risiti wanaponunua na kutoa huduma.

Aidha Meneja huyo wa Mamlaka ya TRA Mkoa wa Tanga alisema kwamba,kudai na kutoa risiti inasaidia kupata mauzo sahihi ikiwa ni pamoja na kutoza kodi sahihi bila kuwepo kwa uonevu wa aina yeyote kwa Wafanyabiashara hatua ambayo pia itapunguza manung’uniko kwa wananchi.

“Kutotoa na kutodai risiti yote ni makosa yanayostahili adhabu, ni muhimu kwa mtu kutoa na kudai risiti yake ili kuondokana na changamoto zxiisizokuwa za lazima p[indi akibainika kutotekeleza wajibu wake”alisema Meneja huyo wa Mamlaka ya Mapato TRA Mkoani Tanga Masese.

Kwa mujibu wa Meneja huyop wa TRA Mkoa wa Tanga,alibainisha Kampeni hiyo ya Tuwajibike uzinduzi wake unafanyika nchi nzima na Tanga imeungana na maeneo mengine huku akitanabaisha kuwa utaratibu huo utoaji elimu  utakuwa endelevu na wilaya zote zitahusishwa.

Mwisho.












 

No comments:

Post a Comment