Sunday 4 June 2023

TBS JINSI INAVYOTUMIA MAONYESHO YA BIASHARA KUELIMISHA WAJASIRIA MALI KUTENGENEZA BIDHAA ZENYE UBORA KUUZA NDANI NA NJE YA NCHI.

Pichani ni Meneja wa Shirika la Viwango (TBS) Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Joseph Mwaipaja  akizungumza na  waandishi wa habari (hawapo pichani) akiitaka jamii kutengeneza bidhaa zenye ubora ili kuweza kuuza ndani na nje ya nchi,kwenye Maonesho ya biashara yanayoendelea kufanyika katika maeneo ya Mwahako Jiji la Tanga.

 NA SOPHIA WAKATI,TANGA

SHIRIKA la Viwango TBS Kanda ya Kaskazini, limewataka wajasiriamali kuhakikisha wanatengeneza bidhaa zenye nembo ya ubora ya TBS ili kuwawezesha kuuza ndani na nje ya nchi pasipo matakwa mengine ya kiviwango.

Meneja wa Shirika la Viwango (TBS) Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Joseph Mwaipaja   Mwaipaja ameyasema hayo jana kwenye Maonesho ya biashara yaliyoandaliwa na Chama cha wafanyabiashara Tanzania TCCIA yanayoendelea kufanyika katika maeneo ya Mwahako Jiji la Tanga.

Mhandisi Mwaipaja amesema wanatumia maonyesho hayo kutoa wito kwa Wajasiriamali kutumia kutembelea banda la TBS ili kupata elimu namna ambavyo wanaweza kupata nembo ya ubora kwa kwa ajili ya bidhaa wanazozalisha.

Amesema kwamba, Serikali imetoa ruzuku ambapo mjasiriamali akiweza kuthibitisha kama ni mjasiriamali kwa kushirikiana na taasisi kama SIDO Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vodogo  na TBS litatoa huduma ya kuthibitisha ubora wa bidhaa yake pasipokuwa na gharama yoyote.

"Natoa wito kwa wananchi waitumie fursa hiyo waje TBS wapitie SIDO ili tuweze kuwahudumia popote pale walipo bila gharama"alisema Mwaipaja akitanabaisha kuwa katika kipindi cha mwaka jana tayari Tanga wajasiriamali 30 wamethibitishwa ubora wa bidhaa zao.

Hata hivyo,Mhandisi Mwaipaja,amesema TBS inashirikiana na nchi wanachama za Afrika Mashariki huku akibainisha kuwa Tanga ni lango lililofunguka,ambapo ni fursa ambayo kama wajasiriamali wataitumia vizuri wataweza kuimarika kiuchumi.
Mwisho.

Mhandisi Mwaipaja amesema wanatumia maonyesho hayo kutoa wito kwa Wajasiriamali kutumia kutembelea banda la TBS ili kupata elimu namna ambavyo wanaweza kupata nembo ya ubora kwa kwa ajili ya bidhaa wanazozalisha.

Amesema kwamba, Serikali imetoa ruzuku ambapo mjasiriamali akiweza kuthibitisha kama ni mjasiriamali kwa kushirikiana na taasisi kama SIDO, Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vodogo  na TBS litatoa huduma ya kuthibitisha ubora wa bidhaa yake pasipokuwa na gharama yoyote.

"Natoa wito kwa wananchi waitumie fursa hiyo waje TBS wapitie SIDO ili tuweze kuwahudumia popote pale walipo bila gharama"alisema Mwaipaja akitanabaisha kuwa katika kipindi cha mwaka jana tayari Tanga wajasiriamali 30 wamethibitishwa ubora wa bidhaa zao.

Hata hivyo,Mhandisi Mwaipaja,amesema TBS inashirikiana na nchi wanachama za Afrika Mashariki huku akibainisha kuwa Tanga ni lango lililofunguka,ambapo ni fursa ambayo kama wajasiriamali wataitumia vizuri wataweza kuimarika kiuchumi.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment