Thursday 1 June 2023

TAKUKURU TANGA JINSI ILIVYO FANIKIWA KUMBAINI WAKALA KUKUSANYA MADUHURI YA SERIKAL ZAIDI YA MILLIUON 83 BILA KUINGIZA BENK,,,

Pichani ni Kaimu Mkuu wa Takukuru mkoa wa Tanga ,Mariam Mayaya akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Tanga''hawapo pichani'' jinsi ilivyofanikiwa kumbaini wakala aliyekusa zaidi ya million 83 bila kuingiza benk. 

NA SOPHIA WAKATI,MUHEZA
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa Mkoani Tanga ''TAKUKURU'' imefanikiwa kumbaini Wakala wa makusanyo ya ushuru wa maduhuli ya Serikali aliyekusanya million  83,709,953.52 bila kuingiza fedha hizo benki kwa kipindi cha Julai 2021 hadi novemba 2022.

Taarifa hiyo imetolewa jana  na  Kaimu Mkuu wa Takukuru mkoani Tanga ,Mariam Mayaya wakati akizungumza na vyombo vya habari Jijini hapo.

Alisema,kwamba Takukuru baada ya kubaini hilo ilishirikiana na ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa wilaya Muheza wakimtaka mmiliki wa kampuni ya uwakala kuingiza fedha hizo kwenye akaunti ya halmashauri ya wilaya ya Muheza.

Alisema kwamba,fedha hizo ambazo zilitakiwa kuingizwa benki ya NMB ndani ya miezi mitatu kuanzia Januari 2023 hadi machi 2023.

Aidha hadi kufikia Machi 27, 2023 tayari jumla ya shilingi million 69,506,327.82 zilikuwa zimerejeshwa kufuatia wakala huyo kutekeleza agizo la kuingiza benki fedha hizo.

Alieleza kuwa hadi kufikia mei 5 mwaka huu fedha zilizobaki ni shilingi million14,203,625.70 ambapo mpango uliowekwa ni kuwa zinapaswa kuingizwa kwenye Akaunti ifikapo June 2023.

Hayo yote yamefanyika ikiwa ni sehemu ya TAKUKURU kutekeleza jukumu la ufuatiliaji wa uzingativu sheria katika utekelezaji bajeti ya Serikali.
Mwisho.


 

No comments:

Post a Comment