Friday 26 May 2023

POLISI TANGA YAKUTANA NA WAENDESHA BODABODA,BAJAJI,WENYEVITI WA MITAA KUWAKUMBUSHA TARATIBU ZILIZOPO,,,


Pichani katikati ambaye amesimama ni Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe  akiwa katika kikao ukumbi wa bwalo la polisi ''Polisi Mesi''akiwataka Bodaboda inapaswa kufanywa kwa kuzingatia misingi ya sheria huku akiwataka ,kuzingatia suala la kufahamiana baada ya kuwa kila mmoja amesajiliwa katika Chama husika hatua ambayo itasaidia kudhibiti vitendo vya uhalifu akiwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya mkoa na wilaya.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

WAENDESHA Bodaboda mkoani Tanga wametakiwa kutii sheria na kutambua kuwa shughuli wanayoifanya ni halali kama ilivyo kwa kazi nyingine na kwamba kazi wanayoifanya siyo kama waganga wa kienyeji ambayo kila mmoja hutumia mtindo ‘Style’ ya aina yake katika kuagua.

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa waTanga,Henry Mwaibambe alitoa Wito huo Jana wakati akizungumza na wamiliki,waendesha bodaboda na bajaji,viongozi wa Serikali za mitaa na viongozi wa vyama vya waendesha Bodaboda katika ukumbi wa Polisi Mesi uliopo Jijini Tanga,

Katika kikao hicho kilicholenga,kukumbushana na kuelimishana juu ya umuhimu wa kuzingatia sharia za usalama barabarani na suala zima la ulinzi na Usalama Jijini Tanga,Kamanda Mwaibambe alisema Bodaboda na Bajaji wanapaswa kujitambua na kuzingatia Sheria zilizopo.

Alisema kwamba, kazi hiyo ya Bodaboda inapaswa kufanywa kwa kuzingatia misingi ya sheria huku akiwataka ,kuzingatia suala la kufahamiana baada ya kuwa kila mmoja amesajiliwa katika Chama husika hatua ambayo itasaidia kudhibiti vitendo vya uhalifu kwenye Jiji hilo la Tanga,

“Ndugu zangu Usalama kwetu Bodaboda ndio kila kitu, mshirikiane vizuri na wenyeviti hawa wa mitaa, msikae na wahalifu kwenye vijiwe vyenu…”alisema Kamanda Mwaibambe huku akilaani tabia za baadhi ya Bodaboda kujihusisha na vitendo vya uporaji wa Simu na uhalifu mwingine.

Kamanda huyo wa Jeshi la Polisi Mkoani Tanga,Pia aliwataka waendesha bodaboda hao kujali maisha yao kwa kutokubali kutumbukia kwenye vitendo vya uhalifu kwa maelezo kuwa wako wanaoingia bila kujua na hata pale wanapobaini wamekuwa wazito katika kutoa taarifa.

“ Tuishi maisha ya kufahamiana, tujali maisha yetu tunapokutana na mtu hatu muelewi kwenye vituo vyetu tuone taarifa. Uporaji Simu imekuwa ni changamoto hivyo tufahamiane na Tanga tuna deni kubwa kuendelea kudumisha amani na usalama”alisema Kamanda Mwaibambe.

Aidha,Kamanda Mwaibambe amewaasa waendesha bodaboda na bajaji hao kutohusika katika kusafirisha madawa ya kulevya kama vile Mirungi, Bangi na hata wahamiaji haramu na kwamba ikitokea vyombo vyao vikikamatwa kuhusika na matukio hayo ni Dhahiri kuwa vitataifishwa.

Ametumia nafasi hiyo kwa kuwataka wajasiriamali hao kujitahidi kuwa wakweli ili kuiwezesha Tanga kuzidi kustawi na kwamba wawe tayari kumfichua yeyote yule atakayekwenda kinyume huku akiahidi kushirikiana na kila mmoja kwa maelezo kuwa milango ya ofisi yake iko wazi muda wote.

Awali Mwenyekiti wa chama cha Bodaboda wilaya ya Tanga,Mohamedi Chande ulieleza kuwa kuna changamoto ubebaji wanafunzi zaidi ya wanne kwenye vyombo hivyo vya usafiri jambo ambalo ni hatari kwa usalama kero ambayo ilidaiwa kuchangiwa na wasafirishaji hao ikiwa ni pamoja na wazazi.

Katika hoja hiyo,Mkuu wa kitengo cha Operesheni polisi mkoa wa Tanga,Zakaria Bernard alisema, hali ngumu ya maisha isiwe kisingizio cha waendesha bodaboda ama wazazi kuruhusu watoto wao ambao ni wanafunzi kupakizwa mshikaki kwenye vyombo vya usafiri.

Awali waendesha bodaboda na bajaji walilalamikia kufanyiwa vurugu na madereva wa Hiace pindi wanapotaka kupakia abiria jambo ambalo limesababisha jamii hizo kupigana mara kwa mara ambapo wameliomba Jeshi la Polisi kuingilia kati ili kulipatia ufumbuzi suala hilo.

Changamoto nyingine waliieleza kuwa ni waendesha bodaboda kupigwa faini nyingi,kukamatwa kwenye maeneo yenye kona ambapo Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga SACP Henry Mwaibambe alisema amezichukua kero zote hizo huku akiahidi kwamba atazifanyia kazi.

Akijibu Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Tanga, Abel Nyalecha aliwataka Wenyeviti wa mitaa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria waendesha bodaboda ambao wanapasua bomba za pikipiki makusudi ili kupiga kelele.

Alisema kwamba, wenyeviti hao wanaweza kuwasiliana na Jeshi la Polisi pindi yanapotokea matukio ya aina hiyo ambayo husababisha vurugu kubwa miongoni mwa jamii akisema kwamba viongozi hao wanahusika katika kulinda usalama huku wakishirikiana kwa karibu na jeshi hilo.

Mwisho.


Kamanda Mwaibambe akiwaeleza waendesha bodaboda kuvaa kofia ngumu ni sheria ya kujikinga na majanga na sio matwakwa ya polisi hivyo muheshimu sambamba na wenyeviti wa mitaa waheshimiwe wanasaidia mambo mengi na ndio mkubwa wa usalama kwenye mtaa wake.


Pichani ni Mkuu wa kitengo cha Operesheni jeshi la polisi mkoa wa Tanga,Zakaria Bernard akieleza, hali ngumu ya maisha isiwe kisingizio cha waendesha bodaboda ama wazazi kuruhusu watoto wao ambao ni wanafunzi kupakizwa mshikaki kwenye vyombo vya usafiri.

Pichani ni Mkuu wa kituo cha polisi Chumbageni wilaya ya Tanga,Enosent Ngonyani akitumia kikao hicho kwa kuwataka wenyeviti wa mtaa kujenga utamaduni wa kuhoji wananchi wao pindi anapotaka barua ya kumdhamini mtu kumchulia dhamana polisi ili kuepuka kuwatoa wahalifu polisi wanaojihusisha na kutoa pikipiki namba na uporaji simu kwa jamii.

Pichani ni Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilayani Tanga, Abel Nyalecha akijibu maswali ya waendesha bodaboda yaliyowasilishwa kwenye kikao hicho.

Akijibu maswali hayo pia aliwataka Wenyeviti wa mitaa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria waendesha bodaboda ambao wanapasua bomba za pikipiki makusudi ili kupiga kelele.

Pichani ni kiongozi kutoka kitengo cha Upelelezi jeshi la polisi mkoa wa Tanga,Lwitiko Adam akiwataka waendesha bodaboda na bajaji kujenga utamaduni wa kutoa taarifa pindi wanapobaini kuna vitendo vya uhali katika maeneo yao ya kazi.

Pichani ni mkuu wa dawati la polisi jamii jeshi la polisi mkoani Tanga,Emmanuel Minja katika kikao hicho akiwataka waendesha bodaboda na bajaji kuhakikisha wanapata leseni ili kuzijua sheria za usalama barabarani na kuweza kuzitekeleza na kunusurika na majanga ikiwemo vifo.
Pichani ni Baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi mkoa wa Tanga, SSP Issa Chabu akiwaeleza waendesha bodaboda na bajaji kwamba kwenye jumuiya kuna watu wazuri na wabaya hivyo kuepuka kumika na wahalifu kupitia kazi zao ili kunusurika na matendo ya uhalifu.

Pichani ambaye ameshika kipaza sauti ni Meneja wa benki ya NMB tawi la Madaraka Jijini Tanga, Elizabeth Chawinga alitoa taarifa hiyo Jana kwenye kikao maalum kilichowahusisha viongozi wa bodaboda,bajaji na wamiliki kilichofanyika katika Bwalo la Polisi Mkoani Tanga.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

BENKI ya NMB tawi la Madaraka Jijini Tanga limeadhimia kuendelea kutoa Mikopo kwa waendesha Bodaboda na Bajaji kwa lengo la kuwaepusha kujiingiza kwenye mikataba ya kinyonyaji hatua ambayo imechangia kudhoofisha jitihada zao za kujikwamua kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Meneja wa benki ya NMB tawi la Madaraka Jijini Tanga, Elizabeth Chawinga alitoa taarifa hiyo Jana kwenye kikao maalum kilichowahusisha viongozi wa bodaboda,bajaji na wamiliki kilichofanyika katika Bwalo la Polisi Mkoani Tanga.

Katika kikao hicho, Meneja huyo wa NMB alisema kuwa benki hiyo tayari imeshaanza utaratibu wa kutoa mikopo kwa waendesha bodaboda hatua ambayo lengo lake ni kuwakwamua kiuchumi na kuwaondoshea changamoto ya kuingia kwenye mikopo yenye mikataba migumu.

“ NMB tunaendelea kutoa mikopo kwa bodaboda na bajaji, tayari tumetoa bajaji na guta, wahusika lazima wafuate taratibu ikiwemo kuwa na leseni ya kutumia chombo cha moto,uthibitisho wa wenyeviti wa mitaa na taratibu nyingine muhimu”alisema Chawinga.

Meneja huyo wa Benki ya NMB tawi la Madaraka aliendelea kusema kwamba, kupitia utaratibu huo wa utoaji mikopo ya vitendea kazi hivyo wataweza kuwakomboa wajasiriamali hao  huku akiwasihi kufungua Akaunti kwenye taasisi hiyo ya fedha ili kupata huduma stahiki kirahisi.

Kwa mujibu wa Chawinga alibainisha mikopo hiyo inaendelea kutolewa kwa waendesha Bajaji na Bodaboda ni yenye masharti nafuu na mkopaji atakuwa akilazimika kulipa kwa Wiki hadi pale atakapokuwa amefanikiwa kumaliza deni lake kwenye benki hiyo ya NMB tawi la Madaraka.

Aidha,Chawinga alisema kwamba,huduma hiyo kwa wajasiriamali hao itakuwa endelevu huku akitoa wito kwa kuwataka wajasiliamali kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo ambayolengo likiwa kuwakomboa Wananchi wenye kipato cha chini.

Hata hivyo,alisema mbali na kuhusika kuwawezesha kwa kuwapatia mikopo yenye Masharti nafuu wafanyabiashara wadogo lakni pia imekuja na huduma mbalimbali likiwemo suala la utoaji wa Bima hatua ambayo lengo lake ni kulipa fidia kwa wahanga pindi majanga yanapowakuta,

Mwisho.


Meneja huyo wa Benk ya NMB tawi la Madaraka Jijini Tanga,Elizabethkutoa Mikopo kw amesema mpango huo kwa waendesha Bodaboda na Bajaji ulishaanza lengo kubwa likiwa kuwaepusha kujiingiza kwenye mikataba ya kinyonyaji hatua ambayo imechangia kudhoofisha jitihada zao za kujikwamua kiuchumi.

Washiriki wa kikao hicho.


Pichani ni Mwenyekiti wa chama cha Bodaboda wilaya ya Tanga,Mohamed Chande awali alieleza kwamba waendesha bodaboda na bajaji walilalamikia kufanyiwa vurugu na madereva wa Hiace pindi wanapotaka kupakia abiria jambo ambalo limesababisha jamii hizo kupigana mara kwa mara ambapo wameliomba Jeshi la Polisi kuingilia kati ili kulipatia ufumbuzi suala hilo.


 

No comments:

Post a Comment