Sunday 4 June 2023

WAMILIKI WA HOTEL WAPOMGEZA FILAMU YA ROYAL TOUR,IMERUDISHA SEKTA YA UTALII NCHINI NA KUWASUKUMA KUSHIRIKI MAONYESHO YA BIASHARA JIJINI TANGA,,,,,

Pichani ni Mwakilishi wa Hoteli za Kitalii za Nyumbani Hotel nchini, Ramson Kisanga katika maonyesho ya biashara Mwahako jijini Tanga,akizungumza na waandi wa habari akieleza kuwa sekta ya utalii imeendelea kuua  kupitia Filamu ya Royal Tour iliyotengenezwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. 

 NA SOPHIA WAKATI,TANGA

SEKTA ya Utalii imeendelea kuimarika hatua ambayo inaelezwa kuchangiwa na hamasa iliyopatikana kupitia Filamu ya Royal Tour iliyotengenezwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Mwakilishi wa Hoteli za Kitalii za Nyumbani Hotel nchini, Ramson Kisanga jana alisema kuwa kipindi kilichopita utalii uliathiriwa na ugonjwa wa Korona kupunguza wageni na kwamba filamu ya Royal Tour imeanza kuwarejesha.

"Korona iliathiri wageni kupungua ila kwa sasa afadhali,pia Royal Tour ya Rais Dk Samia inaonesha kurudisha wageni,soon hali ya uchumi itakuwa better"alisema Kisanga.

Kuhusu Nyumbani Hotel, Kisanga alisema, wamekuwa wakitoa huduma bora katika mikoa ya mbaslimbali ikiwemo Kilimanjaro na Tanga.

Alisema, kwamba wamejikita kwenye sekta hiyo ya utalii lengo likiwa kuhudumia wageni wa ndani na nje ya nchi wakiwa na gharama rafiki.

"Tunatoa huduma za malazi na chakula kwa wageni wa ndani na nje ya nchi, Tanga tupo Independence Avenue na Moshi tupo Mita 500 kutoka kituo kikuu cha mabasi"alisema Kisanga.

Kwa mujibu wa Kisanga, huduma nyingine zinazopatikana Nyumbani Hotel ni kumbi za mikutano za kisasa ambapo pia wamekuwa wakiwatengenezea wateja wao mazingira ya kufanya semina, harusi na hata get together party.

"Bei zetu ni resonable, event yeyote tunaandaa lakini pia tunaweza kukuunganisha na rafiki zetu kutembelea Mlima Kilimanjaro na maeneo mengine"alisema Kisanga.

Kisanga aliongeza kusema kuwa, huduma tarajiwa kwao ni uwepo wa night club kwa rika mbalimbali, modern sport bar, shisha lounge na spar massage.

Mwakilishi huyo wa Nyumbani Hotel anatumia maonyesho hayo kuwakaribisha wadau mbalimbali kufika kwao ili kujipatia huduma bora zinazotolewa na Watanzania waliobobea kwenye medani ya Utalii.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment