Sunday 2 July 2023

JESHI LA POLISI TANGA,,,JINSI LILIVYOJIPANGA KUTUMIA MASHINDANO YA ULINZI CUP KUELIMISHA JAMII KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA UHALIFU,,,,,

Pichani katikati ambaye anaongea ni Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe akiwataka viongozi wa vilabu vya soka kuyatumia mashinda ya Ulinzi Cup kujenga urafiki na imarisha ulinzi katika maeneo yao ili kuendeleza amani iliyopo. 


 NASOPHIA WAKATI,TANGA

Wanamichezo wilayani Tanga wameaswa kuepuka kujihusisha na matumizi ya dawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na zile za kuongeza nguvu jambo ambalo linaweza kusababisha kuathiri afya na hivyo kuputeza ndoto zao za baadae.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Henry Mwaibambe ametoa Rai hiyo kwenye kikao cha kwanza maalum kujadili mashindano ya Ulinzi Cup 2023 yaliyoandaliwa na jeshi la polisi mkoani hapo.

Kamanda Mwaibambe alisema kwamba matumizi ya dawa za kulevya yana athari kubwa huchangia kudhoofisha ndoto za Vijana walio wengi ambao ni nguvu kazi ya taifa letu hapa nchini.

Alisema kufanyika kwa mashindano hayo ni njia ya kutoa elimu kwa jamii ili kusaidia kuwawezesha kujiepusha na kuwafichua wanaojihusisha na vitendo hivyo katika maeneo yao na kuwachukulia hatua za kisheria.

 Aidha,Kamanda Mwaibambe alitumia nafasi hiyo aliwataka Wanamichezo kuzingatia Sheria, kanunu na taratibu zilizopo lengo likiwa kuwanusuru ndugu,jamaa na vizazi vyetu kujiingiza kwenye vitendo viovu.

Alisema kwamba, michezo ni furaha na ajira eneo ambali pia Jeshi la Polisi Mkoani Tanga imeamua kulitumia katika kuelimisha Jamii kuepuka sanjari na kufichua vitendo vya uhalifu.

Frank Kipengele kutoka dawati la Polisi Jamii Mkoani Tanga,alisema kwamba mashindano hayo ya Ulinzi Cup kwa mwaka huu ufunguzi wake utafanyika kwenye Uwanja utakaoweza kukusanya idadi kubwa ya Wananchi.

Aidha,Afande Kipengele alisema kwamba,ratiba ya michezo hiyo itakayofanyika kwa mtimdo wa mtoano itatoka mara baada ya vilabu kukamilisha taratibu za ushiriki.

Mratibu wa mashindano hayo ya Ulinzi Cup kwa mwaka 2023, Sophia Wakati alisema, maandalizi yanakwenda vizuri huku akizitaka timu zenye nia ya kujitokeza kuthibitishwa ushiriki wao.
Mwisho.

Pichani ni Mratibu wa mashindano hayo ya Ulinzi Cup kwa mwaka 2023, Sophia Wakati akielezakwamba maandalizi yanakwenda vizuri huku akizitaka timu zenye nia ya kujitokeza kuthibitishwa ushiriki wao.

Pichani ni vingozi wa vilabu vya soka wilaya ya wakimsikila Kamanda wa jeshi la polisi katika kikao tendaji kujadili mashindano ya Ulinzi Cup 2023 jijini hapo.


No comments:

Post a Comment