Sunday 2 July 2023

MAYELE KUTETEMA MWAMNYETO FOUNDATIO TANGA, PIA WAMO NYOTA SHABALALA, NYONI, FARID NA WENGINE WENGI.

Pichani ni Carlos Carlos ambaye ni Mratibu wa Mwamnyeto Foundation, taasisi ambayo imejikita kwenye misaada ya kibinadamu kwa Jamii ya Watoto wenye mahitaji maalum hususani  Yatima mara baada ya kikao akizungumza na waandi wa mkoa Tanga hawapo pichani juu ya ziara hiyo mikoani.


Na Sophia Wakati,Tanga
UZINDUZI wa Mwamnyeto Foundation unafanyika leo (Julai 2) Siku ya Jumapili katika Uwanja wa CCM Mkwakwani ambapo kutakuwa na mchezo wa Soka wa Hisani utakaoshirikisha Wachezaji wa wanaong'ara kwa sasa dhidi ya Tanga Combine.

Mchezo huo wa utawakutanisha Tanga Combine na Kikosi kitakachoongozwa na Mwamnyeto na Zawadi Mauya, Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba. 

Bakari Nondo Mwamnyeto beki Kisiki wa Dar Young African amesema kwamba, ameanzisha taasisi hiyo ikiwa sehemu ya kurejesha mchango wake kusaidia Watoto Yatima na shughuli nyingine za maendeleo ya kijamii.

"Awamu hii tunataka kuonesha upendo kwa watoto Yatima, ndiyo sababu tumeanzisha hili tamasha"alisema Bakari Nondo Mwamnyeto alipozungumza kwenye mkutano na Wanahabari Jijini Tanga.

Kwa upande wake Zawadi Peter Mauya alisema kwamba,  wamekusudia kurejesha jambo kwa jamii, hatua ambayo imewasukuma  kufanyika mchezo huo wa Hisani Mkoani Tanga.

Katika mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa CCM Mkwakwani majira ya Saa 10 Jioni, Wachezaji nyota wanaong'ara watakaokuwepo kwenye mchezo huo ni Erasto Nyoni, Faridi Mussa, Fiston Kayaka Mayele, Shabalala na wengine wengi.

Mratibu wa Mewamnyeto Foundation Carlos Carlos alisema kwamba, Nyota wengi wa Soka watakuwepo kwenye Mtanange huo ili kuunga mkono Uzinduzi wa Mwamnyeto Foundation taasisi ambayo imejipambanua
katika kuisaidia makundi maalum hususani watoto Yatima.

Katika Mkutano huo na Wanahabari uliofanyika Ukumbi wa Mkwabi Supermarket Jijini Taanga, Carlos alisema kwamba, baada ya mchezo wa Tanga wanatarajia kucheza Soka Mkoani Morogoro.

Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba 'Wekundu wa Msimbazi' Juma Mgunda, ambaye yupo Jijini Tanga kuhudhuria mchezo huo wa Hisani alisema, ni muhimu kwa Jamii kuwaunga Mkono Zawadi Peter Mauya na Mwamnyeto katika kufanikisha shughuli hiyo.
Mwisho.


Pichani Wadau wa Mwamnyeto Foundation wakiwemo Nyota mbalimbali wa Soka mara baada ya Asasi hiyo kutambulishwa kwa Wanahabari.Mkutano ambao ulifanyika katika Ukumbi wa Mkwabi Supermarket uliopo katika Halmashauri ya Jiji la Tanga.


Pichani ni Bakari Nondo Mwamnyeto akizungumza na Wadau kwenye Uzinduzi wa Mwamnyeto Foundation shughuli ambayo ilifanyika Ukumbi wa Mkwabi Supermarket Jijini Tanga.

Pichani ni Wadau wa taasisi ya Mwamnyeto Foundation walipokutana na Wanahabari.

Pichani Waalimu wa Soka, Juma Mgunda (Kushoto) na kulia ni Joseph Lazaro walipokutana Jana kwenye Uzinduzi wa Mwamnyeto Foundation katika Ukumbi wa Mkwabi Supermarket Tanga. 

No comments:

Post a Comment